Tatizo ni kwamba mm nilisaidia pia
Na mimi najua hilo, wala sikulaumu wewe, kwa sababu wewe hukuanzisha mfumo huu, umeukuta.
Ila ni mfumo mbovu.
Nimekaa na watu wa mataifa mbalimbali nikagundua kwamba wenzetu kama Marekani wanaheshimu sana mambo ya mtu mwingine.
Yani mtu mmoja kumuwekea mzigowake mtu mwingine kizembe zembe hivi ni kitu kinaonekana kamakumkosea heshima sana, halafu mtu kuweza kujilipia mambo yake mwenyewe ni kitu kinachoheshimika sana.
Kuna story moja ina elezea hili.
Rais Bush (Baba, H.W0 alikuwa anafanya kampeni za urais, akapita sehemu anapendwa sana, akawa anaongea na watu, ikatokea kama anataka kununua chakula sehemu. Alivyokuwa anapewa chakula, akawa anatoa hela alipe. Yule mama akawa anakataa ile hela. Rais Bush akawa anasema siwezikula bure, lazima nikulipe, yule mama akawa anasema haiwezekani mtu kama wewe ulipe. Rais Bush akasisitiza sana, mama akakataa. Mwisho ikabidi Rais Bush akubali tu, lakini alivyokubalikula bila kulipia, akasema, acheni rekodi zioneshe, nilijaribu kulipa, mama akakataa kabisa.
Sasa hapa tuna mafunzo mawili.
1. Watu wana ukarimu wa kualika watu chakula,wanatoa chakula bure.
2. Watu hao wenye ukarimu, wanakuta wale walioalikwa kula bure, hawako comfotable na kula bure, wenyewe wanatakakuchangia.
3. Hata hivyo, watu wenye ukarimu wanakataa kulipwa.
Zamani mbona hatukuwa na michango? Harusi ziliendaje?
Watu wachache wa familia walikaa, wakanunua chakula kidogo, wakachagua kwa ndugu mwenye sehemukubwa, wakajumuika.
Lakini je, jamii si inataka wanaokula wafanye kazi? Hapo ilikuwaje? Watu walialikwa tu kama mabwanyenye na kula tu bila kufanya kazi?
La hasha, walioalikwa hao hao walikuwa na wawakilishi kutoka familia zaowalioshiriki kuandaa chakula, kupika, kusafisha uwanja etc.
Kwa hivyo, ilikuwa perfect system. Watu walichangia, kuchangia hakukuwekapesa mbele, kuliweka shughuli na kusaidiana kazi mbele, watu hawakuwa na gharama zisizo za lazima za kumbi, catering, DJ.
Ukumbi ni kwa ndugu mwenye uwanja mkubwa, chakula watapika ndugu jamaa na marafiki, DJ kuna uncle mwenye mziki mkubwa atapiga muziki.
Harusi ilifanywa kinyumbani zaidi.
Siku hizi tunashindana nani kavaa zaidi, nani kakodi ukumbi ghali zaidi, nani kafanya catering ya bei mbaya zaidi etc.
The cost is bloated, so unnecessarily, we make this a normal thing. Like it was always like this.
It wasn't. It need not be.