Ndoa yangu haina amani

Amanikullaya

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,120
2,000
Ukweli nimechoka nahitaji kusafiri mbali na nyumbani kwangu kila mtu aishi maisha yake maana tunakaa muda wote kama mtu na mke mwenza.

Ndoa yangu ina miaka 5 tuna watoto 2. Nilikuwa nafanya Biashara vizuri nikafanikiwa kujenga nyumba ya Familia na kumfungulia wife biashara naye ili asinitegemee kila kitu.

Bahati mbaya biashara yangu ikayumba nikawa nakomaa nayo ila yeye muda wote ni kunikatisha tamaa niachane nayo.
Nikapata dharura ya kusafiri kwanda mkoani kwa wazazi nikamwacha kijana.

Huku nyuma wife akamsonga songa kijana mwisho Biashara yangu ikafugwa nikapigiwa simu na wife kijana anaingiza hasara nimefunga.

Niliporejea home uzi ni ule ule anataka niachane nayo. Kweli nikaamua kuachana nayo kwani kodi ya pango iliisha na pia palifugwa wateja wangekuwa wametuhama zaidi hivyo nikilazimisha naweza tengeneza hasara na madeni
nikahitimisha kufunga Rasmi.

Niko zangu home najipanga kutafuta mishe ya kufanya wife ndiye mwenye kazi ndiye kila kitu kinacho husiana na hela. Manyanyaso yakaanzia hapa,
kelele, kupangiwa anachotaka.

Jumamosi ya ngao jamii kati ya Simba na Yanga niliomba Elfu mbili tu nikakae kwenye kibanda umiza niangalie mechi nilitolewa nje.

Siku hiyo nilishinda home kuna kazi nilikuwa nafanya. Nilichoka kweli,
basi nikajirudia zangu home saa 18:00 kujilalia saa tatu na nusu akawa anaingia. Alipofika akanyosha moja kwa moja kitandani. Nikauliza “wife hupiki?” maana njaa inauma. Akasema sipiki na sijakununulia chochote tutakula kesho. Kila nikimwongelesha kimya basi kuepusha shari nikakaa kimya nikalala japo usingizi wa tabu uchovu + njaa + mawazo

Kuanzia siku hiyo ni kununiwa hakuna kusemeshana. Nimewaza niuze nyumba nipate mtaji naona ugumu biashara zikigoma.

Wazo langu kwa sasa kwa sababu sina thamani kwake niondoke nikatafute maisha mbali ata miaka 10 ili nipate amani na faraja. Nahofia nitakufa bure na mawazo naye abaki na amani yake anilelee tu wanangu.
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
10,441
2,000
Aiseee... Hizi nyuzi mwezi huu zimekua nyingi sana! Kila mtu anamlalamikia mkewe!!

Ila ni wanawake wachache sana wanaweza kuingia SUB baada ya Mwanaume kuyumba then wakaperform bila kuleta dharau..

Eee Mwenyezi Mungu tupiganie wanaume.
 

Castle_Lite

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
758
1,000
Aisee Polee Papaa.

Ila usikimbie nyumba.

Alaf Kwan hujui hela anaweka wapi? Ukiwa na shida unachukua na unamwambia kabisa na sio kuiba.
Anapofanya biashara huwez kwenda na kuchukua hela?.

Tafuta mishe nyingine,kopa hela kwa watu na nyingine kachukue kwenye biashara ya mke wako.

Hiyo kununa ipo tu, haitaisha kirahisi mpaka mambo yako yakawe sawa.

Alaf naona umezidi upole, dizaini kama mke anakupanda kichwani.

mwanaume mara nyingi unatakiwa uwe na roho na maamuzi magumu Mzee.
 

Kwisense

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
468
1,000
Mkuu Liverpool VPN njoo umshauri jamaa

BTW anayewadanganyaga eti mke anaweza mlea mume ni nani?

Yaan kweli unaomba hela kwa mke ukaangalie mpira .....yaan bila aibu kabisa unaomba
Inategemea na aina ya mke, niliwahi kufulia japo mke wangu hakuwa na kipato kikubwa sana lakini alisimama imara mpaka hapa nilipo na sikusikia jambo lolote la kudhalilisha utu wangu.
 

TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
746
1,000
Tatzo lilianzia hapo ulipoamua kumfungulia biashara na biashara yako ikaanz kuyumba na akawa anakazan kukwambia uache biashara lakn kama wew wa kiume ilibidi ukazane kuipamban hyo biashara isimame pamoja na changamoto

Sasa ukiendelea kuw nyumbn mtashindwan kbsa sasa sisimama upyaa Tafuta kazi/biashara maisha yaendelee na jitahd usimtegemee huyo mwanamke.
 

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
3,826
2,000
Make decision mkuu ww sio wa kwanza wala sio wa mwisho mkuu,
Soma kisa cha Emmanuel abue na mke wake.
Didier Drogba na mke wake.
Ndoa ya stamina na ndoa ya ben pol,
Usijione mnyonge wala usikate tamaa hata siku moja usishindane na mwanamke mkuu utakufa mapema bila sababu mapenzi yamemshinda bill Gates itakuwa ww mkuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom