Nahitaji kadi maalum VVIP ya kataa ndoa, nimechoka

sitagliptin

JF-Expert Member
Mar 10, 2023
1,080
2,308
Habari za jioni ndugu waumini wa kataa ndoa

Leo naleta kisa changu

Nivumiliwe ishu ya uandishi

Mimi ni kijana umri 34 nilibahatika kupata mwenzangu ambaye pia alikuwa mwajiliwa mimi nikiwa mfanya biashara mwaka 2017 akiwa ndo ajira mpya nikashoboka na mtoto kikaumana maisha yakanza

Tumeishi katika mahusiano ya mbali kama km 40 mpaka mwaka 2018 akahamia kituo cha karibu km 25

Maisha yakaendelea akapata mimba 2019 ambapo pia alifanikiwa kuhamia nilipo kabisa ambapo tayar nilikuwa nimeshajenga nyumba na kuhamia kwangu kutoka kuwa mpangaji

Maisha yakaendelea mimba ya kwanza ikaharibika mapambano yakaendelea

Mtoto wa kwanza kiume tukapata akafaitiwa na wa kike ambaye ndio wa mwisho

Kipindi chote hicho uchumi wangu ulikuwa kwenye pick sana

Maokoto ilikuwa yakutosha

Shetani huingia katikati ya safari ghafla mwaka 2022 nikashitakiwa baraza la kata

Nikaitwa nakuta amejaza fomu tuachane

Nikakubali nikasain bila kuwaza

Ile kitu ilimshtua sana mwenzangu na watu wa baraza

Palepale manake alimpigia simu mama yake mzazi

Kuwa amesain hata bila kusoma

Baraza likaamuru jambo liende mbele ambapo ni mahakamani

Nikaitwa mi na yeye

Hakimu baada ya kusikiliza maelezo ya mwanamke akatupilia mbali shauri mwanamke akashindwa

Baada ya hapo akarudi home analia na kuomba msamaha, baada ya muda nikasemehe maisha yakaendelea

Ila nilimwambia saiv unaomba msamaha kwa kuwa jambo lako limefel

Na alikiri kuwa mshaur wake mbaya ni mama yake mzazi, nilimuuliza mara mbili tatu unauhakika? Akajibu ndio nikaona basi kwakuwa amekiri

Nikurudishe nyuma kidogo msomaji

Tuhuma alizo toa ilikuwa kwamba sihudumii familia hivyo nimpe taraka

Tugawane mali

Ikapita hiyo

Tuendelee

Amani ikarejea kama mwanzo utulivu wa kutosha

Sekeseke likanza upya ghafla mwaka huu january

Ilianza tu nikimuingelesha haongei

Nikimtuma kitu haendi

Ghafla akasema anaenda mahakamani

Nikajibu sawa

Mahakama ya mwanzo kata nayoishi kule akagomewa

Akaenda ofisi ya kata nikaitwa nikaenda

Nikapewa mashtaka ya sihudumii familia

Nikayakana nikaeleza ukweli

Na ukweli ni kwamba mimi ndo nanunua vyakula na kuprovide mahitaji yote ya nyumbani

Mke wangu hata namba za luku hazijui

Lakin mtendaji alionekana kubase kwa mwanamke

Hivyo baadaye nikamua kuondoka

Siku ikafata nikaitwa polis

Akaleleza nikaeleza

Polis wakamshauri haya mambo mngekaa tu chini maana hakuna ishu ya maana

Hapa na imeshindwa kujibu maswali aliyokuuliza

Vyakula mnavyokula nani anatoa pesa?

Hujajibu

So polis wakampitezea

Wakati haya yote yanaendelea

Kashatoa taarifa nyumbani kwetu na kwao

Na kunichafua sana na akaaminika sana

Mwenzangu ana wazazi wote wawili

Mi wote wawili walishatangulia mbele za haki

Baba toka 2002 mama amefariki nikiwa chuo mwaka 2014

Lakin nimeishi sana kwa ndugu

Katika hili wote walikuwa uapnde wake

Ila nikaza sana na msimamo wangu

Ok

Ikatokea ghafla akaondoka nyumban siku 5 bila kuaga

Narud nakuta hayupo na simu hapatikani

Muda huo tayar nishagombana na ndugu zangu kuhusu kusikiliza upande mmoja

Hili lilienda sanjar na kwa wazazi wake

Kuwapanga vya uongo

Siku amerudi kafikia kwa jirani yangu na sio nyumban

Sikuona haja ya kumfatilia nikajua tayar huyu sio wangu

Huku na huki akatorosha watoto kupeleka kwao ngara huko

Karudi kafungua kesi

Leo imesomwa nikasomewa mashtaka

Dai lake

Sihudumii familia

Nimemfukuza

Namnyanyasa

Haya yote nikayakataa kwakuwa sio kweli

Kibaya sana nyuma yake kuna kundi la watu wanamjaza sana upepo hakim amemtaka jumatano afike na mashahid wake

Lengo au hitaji lake ni taraka na mgawanyo wa mali

Nimelia sana wiki hii mpaka basi kila nikiwaza lakini

Sijui mwisho wangu

Na isitoshe kwa sasa pia uchumi wangu umeshake kwa kiasi flani

Nasunir kuwaona mashahid siku husika

Sijajua nini kitatokea

Ila mungu asimame kwenye haki

Naichukia sana ndo kwa kweli

Japo sikuwahi funga naye kupata chet ila zile kimila tu manake mpaka mali nilitoa

Nakataa ndoa

Nakataa ndoa

Nakataa ndoa

Asanteni
 
Mkuu hili liwe aomo kqako na wanaumw qote.

Mwanamke anaondoka siku 5 hautoi taarifa hata polisi ni kujitakia kesi ya kubambikizwa.

Pili wewe kubali yaishe, achana naye na ikiwezekana hama kabisaa huo mji. Nduguzo piga marufuku kukutembelea kwa sababu ni maadui zako namba mbili.

Jambo la tatu, hata alie machozi ya kumeta meta usirudi kwake.

Tafuta hela. Saka pesa yaani pambania maokoto usiwaze maujinga ya huyo shori
 
Swali je wataki unamuowa ulikuwa ushajenga??

Hapa mjini pesa ndio kila kitu chukua hati ya nyumba badilisha jina, andika hivi,

Mfano mm juma husi matola nimenunua kiwanja kutoka kwa ndugu haji musa ngalawa, kwa shilingi fulani, hili jina la mmiliki tafuta mtu ambae kwanza awe na uwezo pili awe mbali na eneo hilo tatu mpange kabisa afahamu,, alafu pale chini ya hati utaandika hivi sahihi ya manunuzi imewekwa na mm hapo unaandika jina lako kwa niaba ya fulani ambae mwenye kiwanja ambae hakuwepo siku ya manunuzi, ukifanya hivi nyumba itaonekana ni mali ya mtu mwingine ambae sio ww kwa maana nyumba haitakuwapo kwenye mgawanyo wa mali, kingine kama una vibiasha vidogo vidogo tafuta namna ya kubadilisha umiliki kabla mambo hayajakuwa mengi, mwisho sema mm bado ninampenda mke wangu ninaomba arudi nyimbani tuendelee na maisha kama yeye ameamua kuondoka aniandikie talaka yangu,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom