Naomba ushauri: Nafanya biashara lakini sina amani ndani yangu. Natamani kwenda mbali lakini sijui naenda kuanzia wapi

Lakabu

JF-Expert Member
May 26, 2023
330
766
Ndugu wanajukwaa, mabibi na mabwana, habari za leo? Namshukuru Mungu kwa kupata nafasi ya kukuandikieni hapa JamiiForums.

Kilichonifanya niandike hii post ni hali ninayopitia sasa hivi ambayo sielewi kabisa. Nafanya biashara lakini nikiwa katika hii biashara sipati utulivu kazini, nahisi sina amani ndani yangu, natamani kwenda mbali lakini huko mbali sijui naenda kuanzia wapi.

Nakuombeni msaada wa mawazo maana nimefika mahali nikaona sina faida tena katika hii Dunia. Maana nimevulia lakini kila siku inakuwa hali mbaya kuliko ile ya jana. Nina hofu iliyoambatana na hasira na maumivu ndani yangu. Sina amani kabisa.
 
Mi naamini kila mtu mwenye ndoto kubwa kubwa, hupitia hio stage.
Hio ni stage ya majaribu
Maandiko yanasema kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe.

Kwanza, ushinde moyo wako usikubali kuendeshwa na mapenzi ya moyo, maandiko yanasema (moyo hu mdanganyifu kuliko vitu vyote)

Pili, usijifananishe hamna kitu kinaongoza kuumiza vijana kama kuji compare na watu wengine, kila mtu ana riziki yake hapa duniani

Tatu, usijipangie: ushawahi kuusikia msemo unasema "wewe unapanga na Mungu anapanga?",
Mtafute Mungu ujue anataka ww uwe nani na ufanye nini hakika ukishaitambua purpose yako hapa ulimwenguni...lazima upate amani ya moyo ko uskate tamaa kama kuna kijana ambaye haumii na kuwazia maisha yake atakuwa ana shida kichwani.
 
Ungetoa maelezo zaidi mkuu tukupe ushauri , unataman kwenda mbali kivip ?

Nini kinakukosesha utulivu ?

Kitu gani kinakufanya ujihisi hauna aman ndani yako?

Kwanini umejiona hauna faida duniani?

Umevumilia kitu gani mkuu?

Kwa sababu kwa ulivyo andika ni kama unalalamika tu binafsi sijui nianzie wapi kukushauri.
 
Unafanya biashara gani kwanza

Je biashra inatoka ?

Je uoni faida ?

Hofu yako inachangiwa na nn ?

Je una mtaji Kia's gani?

Nijibu kisha njoo pm tuyajenge nikupe mbjnu ninazo Tumia mm kuover come hyo situation
 
Binafsi naelewa hali unayopitia,kwanza pole na tutiane moyo...Binafsi Tanzania ni nchi ambayo inauwa vipaji,malengo na ndoto ya vijana wengi..Tanzania ni kama kuzimu ukifanya biashara shida,ukisoma shida...chakukushauri kama unaweza kwenda nchi za Scandinavia huko kuna maisha..sasa hivi vijana tuwe na mpango wa kutafuta fursa nje ya nchi..nchi ambayo inaongwa na akina mwigxlu unategemea nini?
 
Ungetoa maelezo zaidi mkuu tukupe ushauri , unataman kwenda mbali kivip ?

Nini kinakukosesha utulivu ?

Kitu gani kinakufanya ujihisi hauna aman ndani yako?

Kwanini umejiona hauna faida duniani?

Umevumilia kitu gani mkuu?

Kwa sababu kwa ulivyo andika ni kama unalalamika tu binafsi sijui nianzie wapi kukushauri.
Kukosa utulivu na amani inatokea nikiwa katika hii biashara lakini nikiwa mbali nakuwa na amani,Sasa sielewi ni kitu gani kinaninyima amani nikiwa kazini .
 
Kukosa utulivu na amani inatokea nikiwa katika hii biashara lakini nikiwa mbali nakuwa na amani,Sasa sielewi ni kitu gani kinaninyima amani nikiwa kazini .
Jitahidi ufanye maombi, huenda Kuna nguvu hasi.
01, Wana taka waku to mchezoni, tafuta kiongozi wa dini yako piga maombi
 
Kama umeifanya muda mrefu utakua unapitia burnout, kufanya ratiba moja miaka na miaka kunachosha, tafuta namna upumzike au ubadilishe eneo, au ubadilishe namna unavofanya biashara

Biashara sio hela tu, pia unatakiwa uridhike na unachofanya
 
nimefanya karibu miaka 16 eneo hili hili,ila Sasa hivi nahisi Hali zingine ambazo sijawai kuhisi kabisa.
 
nimefanya karibu miaka 16 eneo hili hili,ila Sasa hivi nahisi Hali zingine ambazo sijawai kuhisi kabisa.
chukua ushauri huo

ukiamini umelogwa, sijui mungu kafanya hivi unakuza tatizo tu utaenda kuambiwa flani kakuloga au ukoo wako una laana.... mambo ya kishamba yaani
 
Back
Top Bottom