Amekusikia na tumekusikia Mkuu, nini kifanyike?
Mwanamke keshazaa naye watoto wawili.
Huyu ni Mke wake kabisaa halali ( ukishazaa na mwanamke watoto wawili watatu wala usiumize kichwa tena juu yake ).
Kwa sasa Jamaa, Ajikite kurudisha Thamani yake .
( kihalisia na kama mwanamke angekua Muumini wa Utu, kwa sasa ndio ulikua wakati sahihi wa kusimama na Jamaa, kumpa moyo, kumuombea na KUMFICHIA AIBU JAMAA MBELE ZA WATU)
sisi wanaume kuna ule wakat unataka utoke kidogo, ukae na masela ,n.k, ni wakat wa mwanamke kumwambia " Hubby leo kachamke na wenzako, pesa hii hapa "..
Badala yake mwanamke anazidi kumnyonga jamaaa, Huyu jamaa muda mfupi ujao, ataanza kuona giza, yaan hata kichwa kufunguka ,kitashindwa ..nandio mawazo mabaya mabaya yataanza kumuijiaa...Mke ana mtu .mke amanisaliti..kisa sina hela..kisa hiki....
Lkn niseme ,Toka awali kuna kitu alishakikosea kukitengeza nacho ni HESHIMA.
NDUGU ZANGU, LAZIMA IFIKE MAHALI MWANAMKE AKUHESHIMU PASIPO KUJALI KIPATO CHAKO.
PESA HUJA NA KUONDOKA..LKN UTI WA MTU UTAISHI MILELE NAMILELE MPAKA KUFA KWAKO.
hii inamaana ,Mwanamke mke wako. Lazima auheshimu UTU WAKO wakati wote wa Pesa au kutokua na Pesa.
Tuachane na hayo
Nini Jamaa afanye ???

Jamaa ni mjuzi wa biashara nandio sehem ya maisha yake, watu biashara hkua na kushuka lkn husimama nakuendelea ( niliwah kufungua kabishara nikamuweka Ndugu yangu, alikula mpaka mtaji ,kakafa kote)
Ila sikuacha..

kwakua ana nyumba, na mjuzi wa biashara , Akakope Pesa anayojua inatosha kabisa kuanzisha bishara


Ni vema pia asikae kimya, awashirikishe wazazi, na ndugu zake wa damu, mawazo yao nayake ,ataondoka na kitu ( shida ya wengi ni kukaa na mambo moyoni)


Jamaa asikaee kumfatilia mwanamke, asikae kumuomba kitu kwa mwanamke.


Aanze mapambano , yaan huyo Mwanamke , Dawa yake ni sio kumkimbia, sio kumfukuza sio kuachana naye sababu HAMNA BAYA LA KUFANYA IVO ....LABDA KAMA KUNA USALITI ATAUFANYA KWA JAMAA , SABABU TU YA MAISHA YA JAMAA YA SASA.

Kuomba Mungu, kwa uwezo wetu ,kutoboa maisha ni kazi , unamuomba Mungu akupe njia na kubariki mikono yako.