Ndoa ya wake wengi iruhusiwe kwenye ukristo kuokoa kizazi cha wanawake ambao wanazeeka makanisani bila waume

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Ndoa ya wake wengi inahusu zaidi kumsitiri mwanamke awe na ndoa ajulikane ni mke wa fulani kuzidi mwanaume kuwa na wake wengi.

Leo hii wanawake wengi wa kikristo ni kawaida kuwakuta wanazeekea makanisani huku wakiomba wapata waume kitu ambacho ni kigumu kwasababu wanaume tupo wachache na wenye uwezo wa kuoa wapo wachache zaidi na sheria ni kuoa mke moja, hao wanaume wengine mnategemea watokee wapi?

Wakristo wa kiafrika walikosea sana kufuata mitazamo ya ulimwengu ya wamishonari wa Ulaya walioleta Ukristo barani Afrika na kuacha mitala na mila ambayo ilikuwa imeenea kipindi cha manabii wa kwenye Biblia. kina Esau, Musa, Daudi, Elkana, Mfalme Solomon, n.k.

Kuna sehemu hata moja Mungu alipinga ama kuchukizwa na wao kuoa zaidi ya mke moja ?

wakristo wapitie upya mafundisho ya ndoa ya mke mmoja maana hakuna mstari nabii yoyote alietumwa na Mungu kukataza jambo hili.

Ni muhimu ili "kuokoa kizazi cha wanawake ambao wanazeeka kanisani bila waume"

Mitala ilizoeleka na jamii nyingi za kitamaduni za Kiafrika na tamaduni ya Kiyahudi pia ilikuwa ya wake wengi, ilianza kufifia baada ya kuanzishwa kwa Ukristo ulioegemea zaidi tamaduni za kizungu ambako waligeuza sheria zifuate zaidi tamaduni zao za kuo mke moja.
 
Naomba andiko lolote lenye mamlaka ya Mungu kukataza kuoa wake wengi ?
Wakristo Sio wayahudi.

1 Wakorintho 7

Neno: Bibilia Takatifu

Kuhusu Ndoa​

7 Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. 2 Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
 
Ndoa ya wake wengi inahusu zaidi kumsitiri mwanamke awe na ndoa ajulikane ni mke wa fulani kuzidi mwanaume kuwa na wake wengi.

Leo hii wanawake wengi wa kikristo ni kawaida kuwakuta wanazeekea makanisani huku wakiomba wapata waume kitu ambacho ni kigumu kwasababu wanaume tupo wachache na wenye uwezo wa kuoa wapo wachache zaidi na sheria ni kuoa mke moja, hao wanaume wengine mnategemea watokee wapi?

Wakristo wa kiafrika walikosea sana kufuata mitazamo ya ulimwengu ya wamishonari wa Ulaya walioleta Ukristo barani Afrika na kuacha mitala na mila ambayo ilikuwa imeenea kipindi cha manabii wa kwenye Biblia. kina Esau, Musa, Daudi, Elkana, Mfalme Solomon, n.k. kuna sehemu hata moja Mungu alipinga ama kuchukizwa na wao kuoa zaidi ya mke moja ?

wakristo wapitie upya mafundisho ya ndoa ya mke mmoja maana hakuna mstari nabii yoyote alietumwa na Mungu kukataza jambo hili.

ni muhimu ili "kuokoa kizazi cha wanawake ambao wanazeeka kanisani bila waume"

mitala ilizoeleka na jamii nyingi za kitamaduni za Kiafrika na tamaduni ya Kiyahudi pia ilikuwa ya wake wengi, ilianza kufifia baada ya kuanzishwa kwa Ukristo ulioegemea zaidi tamaduni za kizungu ambako waligeuza sheria zifuate zaidi tamaduni zao za kuo mke moja.
Mzee Mwinyi alisema mke mmoja anasababisha BP bure!

Ila ukweli ni kuwa uislamu unayaishi maisha ya manabii na mitume wa Mungu, Suleiman na Daudi hawakuipiga kufuli miili yao ilipodemand kipozeo still Mungu hakuwachukia
 
NDOA KIBIBLIA

NDOA YA MKE MMOJA NA MUME MMOJA NI AGIZO NA NI SHERIA YA MUNGU​



UTANGULIZI:
Kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa katika swala la ndoa kati ya ndoa ya mke mmoja na mume mmoja na ndoa ya mume mmoja na wake wengi (ndoa ya mitala). Katika hili kuna baadhi ya watumishi ambao wamediliki kusema hadharani kuwa, ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ni agizo la wanadamu na sio la Mungu na hakuna katazo lolote katika Biblia la ndoa ya mitala. Hii SIO KWELI KABISA NA NI KINYUME CHA BIBLIA NA MPANGO WA MUNGU KATIKA NDOA TANGU MWANZO.

Kwa sababu ya mkanganyiko huo, nimeona ni vyema nikaandika somo hili ili kuwatoa watu katika mkanganyiko huo.

Biblia imesema wazi kuwa, Katika siku za mwisho kutatokea manabii wengi na walimu wengi wa uongo, na roho zidanganyazo ili kuipindua Kweli ya Mungu kwa kusudi la kuwadanganya wengi. Kwa kuwa ndoa ni kitu nyeti sana na kina muunganiko wa moja kwa moja na maisha ya mtu ya rohoni, shetani anataka kuiharibu ndoa huku akijua kuwa, atakapoiharibu ataharibu maisha ya wengi.

Nilikuwa nasoma somo moja katika mitandao ya kijamii, nikiwa nasoma mapendekezo (comments) ya watu nikaona baadhi ya watu wanaojiita wameokoka wakihoji ni wapi ndoa ya mitala imesemwa kuwa ni dhambi katika Biblia. Na kwa haraka haraka kwa kuchunguza maandishi yao nilitambua fikra zao kuwa ndoa za mitala sio dhambi kwa sababu hata Yakobo, Ibrahimu, Daudi, Sulemani na wengine wengi walikuwa na ndoa ya mitala. Ndipo nilipotambua kuwa kweli tunahitaji kujua ni nini Mungu alikuwa anawaza wakati anakusudia ndoa na ni nini anawaza juu ya ndoa hata leo. Na ndio maana ya somo hili ili tujue wazi kwa mujibu wa maandiko ya Biblia mpango na kusudi la Mungu katika kuanzisha ndoa.

NDOA YA MKE MMOJA NA MUME MMOJA NI MPANGO WA MUNGU.
Hii ni pamoja na kusema kuwa ndoa ya mitala si mpango wa Mungu kabisa na kwa sababu hiyo ni makosa na dhambi kuwa na wake wengi kwa mwanaume mmoja. Tutaanza kwa kuangalia sababu za kwa nini ndoa ya mke mmoja ni mpango wa Mungu na si ndoa ya mitala.

SABABU YA KWANZA:
Sababu za kiuumbaji wa Mungu tangu mwanzo.

Tangu mwanzo Mungu alimuumba mwanamume mmoja na mwanamke mmoja. Mungu alitwaa ubavu mmoja katika mbavu za mwanaume akaufanya mwanamke na sio wanawake. Alitwaa upande mmoja wa mwanaume akaufanya mwanamke na sio wanawake. Ingemlazimu Mungu kutwaa mbavu mbili au zaidi toka kwa mwanaume kumfanyia mwanaume wake zaidi ya mmoja. Lakini haikuwa wazo la Mungu tangu mwanzo kuwa mwanaume awe na wake zaidi ya mmoja na ndio maana hayakuwepo majadiliano yoyote katika Utatu wa Mungu ya ni ndoa ya aina gani wamfanyie Adamu, ya mke mmoja au ya wake wengi. Hawakufanya uchaguzi wowote kwa sababu ndoa ya mitala haikuwa katika wazo la Mungu (it did not and it doesn't exist in the mind of God). Ndoa ya mke mmoja ni ndoa ambayo ndio ilikuwa katika wazo la Mungu, na Mungu alikuwa na mpango nayo wa milele. Na si ndoa ya mitala, hii haipo kabisa katika wazo la Mungu. Na hii imeakisi hata uumbaji wake kwa mwadamu (wote mwanamke na mwanaume). Mwanamke hana uwezo wa kupenda wanaume wawili kwa wakati mmoja, na mwanaume hawezi kupenda wanawake wawili kwa wakati mmoja, ila kwa upande wa mwanaume anaweza kutamani wanawake wengi kwa wakati mmoja na hii ni baada ya dhambi kuingia dunia. Kabla ya dhambi haikuwa hivyo.

Mwanzo 2:18,21-24

[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

(Mungu hapa hakusema kuwa nitamfanyia WASAIDIZI bali alisema nitamfanyia MSAIDIZI wa kufanana naye. Kwa hiyo Mungu hakumkusudia mwanaume awe na mke zaidi ya mmoja.)

[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

(Mungu alitwaa ubavu mmoja toka kwa Adamu kumtengeneza mwanamke (msaidizi) mmoja wa Adamu. Kwa nini? Kwa sababu mwanaume anahitaji mwanamke mmoja tu kukidhi hitaji lake la mwambata, zaidi ya hapo ni tamaa tu, na tamaa si uhitaji)


[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

(Mungu hakuleta kwa Adamu wanawake, alileta kwa Adamu mwanamke kwa sababu anachohitaji Adamu si wanawake ni mwanamke ambaye amefanywa kuwa msaidizi. Mungu aliyemuumba mwanaume Adamu ndiye aliyemuwekea hitaji la msaidizi mwanamke ndani yake na Mungu huyo huyo ndiye aliyemtimizia Adamu hitaji hilo kwa kumfanyia msaidizi mmoja tu. Na Mungu alifanya hivyo kwa sababu ndilo alilokusudia tangu mwanzo. Haikuwa bahati mbaya na wala haikutokea tu pasipo kusudi, ilikuwa ni kwa kusudi maalumu na mpango maalumu wa Mungu)

[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

(Adamu anaridhika na kutosheka na mwanamke mmoja kwa sababu anakidhi hitaji lake la ndani ambalo ni hitaji la moyo wake na si tamaa za mwili wake au tamaa za macho yake.)

[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

(Kauli hii Adamu anaisema akiwa na ufahamu wa wazo la Mungu ndani yake huku akizingatia uhitaji wa ndani wa wote wawili mwanaume na mwanamke katika swala la ndoa. Kauli hii inaonyesha wazi kuwa ili kukidhi uhitaji wa ndani mwanaume anahitaji mwanamke mmoja na mwanamke anahitaji mwanaume mmoja zaidi ya hapo ni tamaa ambayo iliingia na kuanza kutawala baada ya dhambi kuingia na kutawala. Adamu anasema, Mtu (mwanaume) atawaacha wazazi wake naye ataambatana na mkewe (na sio wake zake) nao (mwanaume mmoja na mwanamke mmoja) watakuwa mwili mmoja. Kauli hii ni Kauli ya Mungu mwenyewe kwa kinywa cha Adamu na ndio maana Yesu anairudia, na Mtume Paulo anairudia (Mathayo 19:4-6; 1Korintho 7))

Maandiko hapo juu yanaonyesha mapenzi ya Mungu katika ndoa ni mke mmoja na mme mmoja zaidi ya hapo si mapenzi ya Mungu. Na chochote ambacho si mapenzi ya Mungu ni dhambi mbele za Mungu. Kwa sababu ndoa ya mitala si ya Kimungu imegubikwa na matatizo mengi yanayoharibu maisha ya wahusika, na daima hakuna amani na upendo zaidi ya wivu na magomvi tu.

WAKATI GANI NDOA ZA MITALA ZILIINGIA.

Baada ya Anguko la mwanadamu kila kitu kisichokuwa cha kimungu kiliingia katika maisha ya mwanadamu. Kabla ya Anguko hapakuwepo na ndoa ya mitala. Tunaona ndoa ya mitala inaingia baada ya Anguko. Na mtu wa kwanza ambaye ametajwa na Biblia kuwa na ndoa ya mitala ni Lameki mtoto wa Henoko mwana wa Kaini ambaye aliasi mbele za Mungu. (Mwanzo 4:19). Huu ulikuwa ni mwanzo wa taasisi ya ndoa kupoteza mwelekeo na kusudi la Mungu.

Hata hivyo kwa kadiri dhambi ilipoingia duniani uasi ulizidi kuongezeka na hofu ya Mungu kutoweka kabisa. Taratibu jambo hili la ndoa ya mitala lilianza kuonekana ni jambo la kawaida katika jamii zile na likaonekana kama ni sehemu ya maisha yao ya kawaida. Mtindo huu wa maisha uliathili hata maisha ya watu wa Mungu. Mungu kwa kipindi hiki cha Agano la Kale kulinyamazia jambo hili haikuwa na maana kuwa ni sawa mbele zake. Kwa kuwa yeye ni mvumilivu na mstahimilivu aliwavumilia watu wa kizazi hiki huku akiandaa mpango wa kuwatoa wanadamu katika upotevu huo.

Hata hivyo katika Biblia kwa upande wa watu wa Mungu inaonyesha wazi kuwa kila penye ndoa ya mitala ilipoanza, chanzo chake ilikuwa ni tatizo fulani hivi. Kwa mfano Ibrahimu, yeye na mke wake walishindwa kusubiri ahadi ya Mungu kwa kuangalia mazingira. Ikabidi Sara amwambie mumewe ajitwalie mjakazi. Na huu haukuwa mpango wa Mungu bali wa shetani ili kuzuia ukombozi wa mwanadamu.
Mtu mwingine ni Yakobo, yeye hakukusudia kuwa na ndoa ya mitala ila kwa sababu ya udanganyifu wa Labani ilimlazimu awe na ndoa ya mitala. Na daima hapakuwa na amani katika ndoa hiyo. Wivu ulitawala na magomvi ya hapa na pale.
Angalia na uchunguze vizuri watu wote katika Biblia wenye ndoa ya mitala kama zilitokana na Mungu. Wote walichepuka na kwa sababu hiyo kulikuwa na matatizo aidha ya kuipotosha kiimani kama mfalme Sulemani au migogoro ya wao kwa wao. Hii inatufundisha kuwa ndoa za namna hii si mpango wa Mungu kabisa.

Kwa hiyo ndoa ya mitala ni matokeo ya Anguko la mwanadamu na si mpango wa Mungu kabisa. Chochote ambacho kimezaliwa na anguko la mwanadamu si cha kimungu kwa sababu kinatokana na MWANADAMU KUPUNGUKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU.

Warumi 3:10-18,23
[10]kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
[11]Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
[12]Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
[13]Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
[14]Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
[15]Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
[16]Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
[17]Wala njia ya amani hawakuijua.
[18]Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;


Katika sehemu ya pili ya somo hili tutaangalia sababu ya pili hadi ya tano ya kwa nini ndoa ya mke mmoja ndio ya Kibiblia na ya kimungu na sio ndoa ya mitala.

Mungu akubariki sana. Kama una swali unaweza kulihifadhi mpaka nitakapomaliza somo. Kama litakuwa halijajibiwa ndani ya somo ndipo utauliza.
SABABU YA PILI:
Ni kwa sababu ya maagizo ya YESU KRISTO NA MITUME WAKE katika AGANO JIPYA kuhusiana na ndoa.


Yesu Kristo pamoja na mitume wake katika kutoa maagizo kuhusiana na ndoa hawajawahi kabisa kutoa maagizo kuhusiana na ndoa ya mitala wala kuizungumzia kwa sababu katika mawazo ya Mungu na mpango wake haipo kabisa (polygamy does not exist in God's mind and it's not God's plan since the beginning, that's why it doesn't exist in the New Testament. Jesus did talk nothing about it nor His disciples). Hii inaonyesha kuwa swala la ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ndilo Biblia inatambu na ndio mpango na kusudi la Mungu na wala si jambo ambalo viongozi wa kikristo walikaa na kujitungia na wala si jambo la kimapokeo, ni jambo la Kimungu kwa asilimia zote.

A). Bwana Yesu Kristo alisema nini kuhusu ndoa.

Mathayo 19:3-9

[3]Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
(mkewe na si wakeze, ni mmoja na si wengi)


[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
(mke mmoja na mume mmoja. Si swala la kibinadamu ni swala la Kimungu ndoa kuwa ya mke mmoja na mume mmoja. Ni Mungu mwenyewe ndio aliyekusudia iwe hivyo tangu mwanzo na haikukusudiwa kubadilika kutoka kuwa mke mmoja kwa mume mmoja na kuwa wake wengi kwa mume mmoja)

[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

(wawili (mke mmoja na mume mmoja) watakuwa mwili mmoja. Ni mke mmoja na mume mmoja ndio wako katika nafasi ya kuwa mwili mmoja na si vinginevyo)

[6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

(muunganiko wa kindoa wa mume mmoja na mke mmoja ni swala la Mungu mwenyewe na si la mwanadamu. Ni mke mmoja na mume mmoja)

[7]Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
(Ni Musa na sio Mungu)

[8]Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

(Biblia inarudia tena kwa kinywa cha Yesu mwenyewe kuwa ruhusa ya kuachana (mtu kumwacha mkewe na kuoa mke mwingine) ilitolewa na Musa na sio Mungu. Kumbuka Yesu ni Mungu na alikuwepo tangu mwanzo, na hata wakati wa Musa alikuwepo. Kwa hiyo ruhusa iliyotolewa na Musa haikutokana na sababu za Kimungu, ilitokana na sababu za kibinadamu (ugumu wa mioyo ya wanadamu) yaani kutokuwa tayari kufuata mapenzi ya Mungu na kuyafanya. Kwa sababu Yesu anajua kusudi la Mungu tangu mwanzo hapa anatoa ufafanuzi wa kilichosababisha ilikuwa sio Mungu bali ugumu wa mioyo. Na aliyetoa agizo hakuwa Mungu bali Ni Musa)

[9]Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

(Isipokuwa kwa sababu ya uasherati yeyote amwachaye mkewe kwa sababu nyingine na kumpa hati ya talaka, akioa mke mwingine anakuwa anazini, na mke akiolewa na mume mwingine naye azini. Hii ni kwa sababu kwa Mungu bado wao ni mke na mume halali. Hebu fikiria, hawa wameachana na kila mmoja kaingia kwenye ndoa nyingine na mtu mwingine lakini bado kwa Mungu wanahesabika kuwa ni wazinzi, je, vipi kuhusu wale walio kwenye ndoa ya mitala? Hao nao wazini isipokuwa mke wa kwanza wa mume husika)

Haya ni maneno ya Yesu kuhusiana na ndoa. Katika maneno yake hautakuta anazungumzia ndoa ya mitala kwa sababu katika ulimwengu wa roho wa Kimungu haipo kabisa, haijawahi kukusudiwa na kwa sababu hiyo mbinguni haitambulikani na kwa sababu haitambulikani ni dhambi kwa sababu wahusika wanazini. (Soma pia Marko 10:2-12)

B). Mtume Paulo alisema nini kuhusu ndoa.

Mtume Paulo naye anazungumzia ndoa ya mke mmoja na mume mmoja. Hazungumzii ndoa ya mitala kwa sababu haipo kabisa katika ulimwengu wa roho wa Kimungu.

1 Wakorintho 7:1-4,10-11,33,39
[1]Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.

[2]Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.


(kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na sio wake zake mwenyewe, ni mke mmoja na vivyo hivyo kwa upande wa mwanamke awe na mume mmoja aliye wake mwenyewe si wa kuchangia na wanawake wengine. Hii ina maana asiingilie ndoa ya mtu mwingine kwa kukubali kuwa mke wa pili. Ni vyema akawa na mume wake mwenyewe. Zaidi ya hapo ni uzinzi)

[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

(ni mke mmoja na mume mmoja)

[4]Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.

(ni mke mmoja na mume mmoja)

[10]Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

[11]lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.


(kwa sababu akiolewa au kuoa mtu mwingine azini)

[33]bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

(ni mkewe na sio wakeze)

[39]Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.

Waefeso 5:31,33
[31]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.

[33]Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.


Katika maagizo yote ya Mtume Paulo kuhusiana na ndoa yanalenga ndoa ya mke mmoja na mume mmoja yakiwa na mmsisitizo mkubwa. Moja ya mkazo aliouweka ni mume kuwa na mke wake mwenyewe kwa maana ya kuwa isitokee anakuwa na mke anayechangia na wanaume wengine au yeye kuwa na wake zaidi ya mmoja. Mkazo wake mwingine kwa upande wa mke ni kuwa na mume wake MWENYEWE ambaye hachangii na wanawake wengine ni yeye mwenyewe na yeye tu, Wao wawili tu na si zaidi ya hapo.

Akiwa anatoa maelekezo ya mtu yeyote ambaye anataka uongozi wa mambo ya Kiroho, anasisitiza kuwa ni lazima mtu huyo awe na ndoa ya mke mmoja tu.

1 Timotheo 3:2,12
[2]Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;

[12]Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.

Tito 1:5-6
[5]Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
[6]ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.


C). Mtume Petro anasema nini kuhusu ndoa.

1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Na kumpa mke heshima na sio mume mmoja kuwapa wake zake heshima, ni mume mmoja ampe mkewe heshima.

Ushahidi huu wa kimaandiko tukianza na Yesu kisha mitume wake waliozungumzia maswala ya ndoa unaonyesha wazi wazi na kuzungumzia wazi wazi ndoa ya mke mmoja na mume mmoja kuwa ndio ndoa iliyokusudiwa. Mtume Paulo anasema, anatoa agizo hilo kama alivyopokea kwa Bwana.

1 Wakorintho 7:10
[10]Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

Kwa hiyo, mimi nashangaa sana kusikia kauli za baadhi ya watumishi wakisema kuwa ndoa ya mke mmoja ni utaratibu wa watu fulani na sio wa Kibiblia na ya kuwa Biblia inaruhusu ndoa ya mitala. Jamani, tunakwenda wapi? Ikumbukwe kuwa hata hao walioandikwa katika Biblia kuwa walioa wake zaidi ya mmoja haukuwa mpango wa Mungu. Ukweli ni kwamba pamoja na kuwa walikuwa ni watumishi wa Mungu bado walipofanya hivyo walikosea. Na habari zao zimeandikwa ili kutufundisha ili kwamba na sisi tusirudie makosa hayo hayo waliyoyafanya wao. Habari za mambo hayo hazikuandikwa kwa sababu ni sahihi ziliandikwa ili tujifunze kufanya lililo jema kutokana na makosa yao.

Ibrahimu alimtwaa Hajiri kwa sababu alitindikiwa imani yeye na mke wake, haikuwa agizo la Mungu na ndio maana alifukuzwa.
SABABU YA TATU:
Lugha iliyotumika katika Biblia kuelezea ndoa ni lugha ambayo haiwezi kuelezea ndoa ya mitala.


Biblia imetumia lugha ya mfano kuelezea uzito wa ndoa, na lugha hii kutumika kuelezea ndoa ya mitala ni kitu kisichowezekana kabisa.

Lugha ya kwanza ni lugha iliyotokana na tamko la kwanza na kuu ambalo ndilo msingi wa ndoa ya kimungu lililotamkwa na Adamu mara tu baada ya Mungu kumleta msaidizi huyu kwa Adamu.

Mwanzo 2:24
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Watakuwa MWILI MMOJA: Tamko hili halikuwa kwa ajili ya Adamu tu, lilikuwa kwa ajili ya vizazi vyote vya Adamu. Na ndio tangazo la sheria ya ndoa (the declaration of the law of marriage).

Kwa hiyo ni vigumu lugha hii ya WAWILI KUWA MWILI MMOJA kuitumia kuwaunganisha mwanaume mmoja na wanawake wengi kuwa MWILI MMOJA. Kwa sababu hii ndoa ya mitala si ya Kibiblia kwa sababu haikukusudiwa na Mungu.

Mathayo 19:5-6
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
[6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.


Yesu Kristo Bwana wetu na Mwokozi wetu pia akizungumzia sheria ya ndoa (the law of marriage) anatumia lugha iyo hiyo ya WAWILI KUWA MWILI MMOJA. Anasema kuwa, Hata wamekuwa SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA. Hapa si swala la mwanaume mmoja wanawake wengi ni swala la wawili tu, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.

Waefeso 5:31
[31]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.

Mtume Paulo naye akielezea sheria ya ndoa (the law of marriage) anatumia lugha iyo hiyo ya WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA. Anasema, Mwanaume atawaacha wazazi wake, naye ataambatana na MKEWE, na hao WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA. Hii lugha haiwezi kutumika katika ndoa ya mitala kabisa.

Biblia inasema kuwa Neno huthibitika kwa vinywa vya watu watatu, kauli hii au tangazo hili limesemwa na vinywa vya watu watatu na wote hawa walitamka wakiwa katika uvuvio wa Roho Mtakatifu.

WA KWANZA: Huyu alikuwa ni Adamu mara tu baada ya kuletewa mwanamke na Mungu, alitamka tamko hili. Huyu anawakilisha Agano la Kale.

WA PILI: Huyu alikuwa ni Yesu Kristo, alitamka tamko hili akiwa anajibu swali la Mafarisayo. Huyu anawakilisha mbingu kwa sababu yeye ni Mungu.

WA TATU: Huyu alikuwa Mtume Paulo. Yeye alitamka Neno hili akiwa anafundisha unyeti na uzito wa ndoa akiuhusianisha uhusiano wa mke na mume na uhusiano wa Yesu na kanisa lake. Huyu anawakilisha Agano Jipya.

Kwa hiyo, Lugha hii ya WAWILI KUWA MWILI MMOJA imetumiwa na 1. Agano la Kale, 2. Mbingu kwa maana ya Mungu, na 3. Agano Jipya. Ina uwakilishi kutoka Agano la Kale, Agano Jipya, Na Mbinguni. Hii yote inathibitisha uhalali wa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja na si uhalali wa ndoa ya mitala.

Pengine hujanielewa, hebu tuingie ndani kidogo kwa kuangalia lugha nyingine iliyotumika kuelezea ndoa kwa ujumla wake.

MUME NI KICHWA CHA MKEWE NA MKE NI MWILI WA MUMEWE:

Waefeso 5:22-23,28-29
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
[23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
[28]Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
[29]Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.


Daima hakuna kichwa chenye miili miwili au zaidi. Kila kichwa kina mwili mmoja. Wawili hawa mke na mume wanapokuwa mwili mmoja, Mume huwa kichwa na mke huwa mwili. Lugha hii haikutumika kwa bahati mbaya, ilitumika kwa makusudi ili kuelezea sheria ya ndoa ambayo ni Mungu mwenyewe amehusika. Kwa hiyo Biblia haitambui ndoa ya mitala. Ni kweli unaweza kuniletea orodha ndefu ya watu wakuu katika Biblia waliokuwa na ndoa ya mitala, bado hii haithibitishi kuwa ni halali kwa Mungu. Wao walikuwa ni wanadamu na sioni haya kusema kuwa walimtenda Mungu dhambi. Lakini kwa sababu Mungu alikuwa yuko kwenye mchakato wa kumleta Mwokozi alijifanya kana kwamba haoni, akawa mvumilivu kwa hao.

Matendo ya Mitume 17:30-31
[30]Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
[31]Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Kunyamaza kwa Mungu wakati wa Agano la Kale kusiwe sababu ya kuhalalisha baadhi ya makosa waliofanya wazee wetu katika imani waliotutangulia. Dhambi zao zilizonyamaziwa zisihesabike kwetu kuwa ni haki. Zamani hizi si kama zamani zile. Zamani zile zilikuwa zamani za ujinga lakini sasa Mungu anamwagiza kila mmoja atubu.

SABABU YA NNE:
Uhusiano wa ndoa umefananishwa na uhusiano wa Yesu na Kanisa lake.

Waefeso 5:22-33

[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
[23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
[24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
[26]ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
[27]apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
[28]Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
[29]Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
[30]Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
[31]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
[32]Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.
[33]Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.


Ukisoma kifungu hiki cha mistari hii utaona Mtume Paulo kwa uvuvio na ufunuo maalumu wa Roho Mtakatifu anaelezea kwa ujasiri wote kuwa uhusiano wa Yesu Kristo na Kanisa hauna tofauti na uhusiano wa mke na mume katika ndoa. Katika kifungu hiki cha maandiko ametajwa mke kama mfano wa kanisa. Hakuna wake wala hakuna makanisa, bali kuna mke na kuna kanisa. Mke akiwa mwili wa mumewe na kanisa likiwa mwili wa Kristo. Hakuna miili mingi ya Kristo bali mwili mmoja wa Kristo, na vivyo hivyo haipasi mume akawa na miili mingi bali mwili mmoja. Kama uhusiano wa Yesu na kanisa ulivyo wa pekee na mtakatifu ndivyo uhusiano wa mke na mume unapaswa kuwa wa pekee na mtakatifu, uasherati na uzinzi haupaswi kuingilia kati kabisa. Mke amtii mumewe na kumuheshimu na mume ampende mkewe na kujitoa kwa ajili yake tu. Hii ndio sheria ya ndoa na ndio ndoa iliyokusudiwa na Mungu.

HITIMISHO:
Ndoa ni kitu kitakatifu kilichoanzishwa na Mungu mwenyewe kwa kuwaunganisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kuwa mke na mume na hao wawili kuwa mwili mmoja. Namna Mungu alivyomuumba mwanamke inasadifu na kuakisi kusudi la Mungu katika swala la ndoa. Mungu alitwaa ubavu mmoja akaufanya mwanamke na sio wanawake na kisha kumleta kwa Adamu, na akawa mkewe Adamu. Na uhusiano huu unapaswa kuheshimiwa na watu wote kwa sababu unaaksi uhusiano wa Yesu Kristo na Kanisa lake lakini pia ni uhusiano ambao Mungu aliufanya kwa kusudi la kujifanyia familia ya jamii kubwa ya watu wake watakaokaa naye milele wakifurahi pamoja.


Waebrania 13:4
[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.


Ubarikiwe sana
 
Ndoa ya wake wengi inahusu zaidi kumsitiri mwanamke awe na ndoa ajulikane ni mke wa fulani kuzidi mwanaume kuwa na wake wengi.

Leo hii wanawake wengi wa kikristo ni kawaida kuwakuta wanazeekea makanisani huku wakiomba wapata waume kitu ambacho ni kigumu kwasababu wanaume tupo wachache na wenye uwezo wa kuoa wapo wachache zaidi na sheria ni kuoa mke moja, hao wanaume wengine mnategemea watokee wapi?

Wakristo wa kiafrika walikosea sana kufuata mitazamo ya ulimwengu ya wamishonari wa Ulaya walioleta Ukristo barani Afrika na kuacha mitala na mila ambayo ilikuwa imeenea kipindi cha manabii wa kwenye Biblia. kina Esau, Musa, Daudi, Elkana, Mfalme Solomon, n.k. kuna sehemu hata moja Mungu alipinga ama kuchukizwa na wao kuoa zaidi ya mke moja ?

wakristo wapitie upya mafundisho ya ndoa ya mke mmoja maana hakuna mstari nabii yoyote alietumwa na Mungu kukataza jambo hili.

ni muhimu ili "kuokoa kizazi cha wanawake ambao wanazeeka kanisani bila waume"

mitala ilizoeleka na jamii nyingi za kitamaduni za Kiafrika na tamaduni ya Kiyahudi pia ilikuwa ya wake wengi, ilianza kufifia baada ya kuanzishwa kwa Ukristo ulioegemea zaidi tamaduni za kizungu ambako waligeuza sheria zifuate zaidi tamaduni zao za kuo mke moja.
Hao wanaozeekea makanisani wameyataka wenyewe
 
Idadi itapungua kwasababu kama kanisani kuna wawanawake 100 hawana ndoa, wanaume hata 10 tu wanaweza kuounguza idadi iwe 75
Wanawake wengi hawaolewi sababu ya tamaa ya mali kanisa likiruhusu kila mwanamke atakuwa anafukuzia mzee mstaafu tutajenga jamii gani italeta mifarakano pale vifo vinavyotokea mwisho kila mtu anataka mgao wake

Hao wanawake ambao wanasema hawaolewi wewe ungewaacha tu wana mapungufu mengi waache tu nazani itakuwa funzo kwa kizazi kijacho
 
Back
Top Bottom