Mimi nimeokoka, ndio mwaka WA 30 sasa nipo ndani ya YESU, ukubali ukatae hainihusu
Lakini sicho kilichonileta hapa, kilichonileta hapa ni hii kitu inaitwaga "NDOA"
Ndoa Bwana hainaga mwenyewe, Mungu aliotoa ndoa Kwa waliookoka, wapagani na wasiookoka, huu NI ukweli na hakuna upendeleo, kama vile mvua na jua vinavyowashukia watu wote Duniani, waovu na watakatifu
Nachopenda kushauri wale nduguzangu waliookoka tunaotarajia kwenda Mbinguni, ikija kuhusu Swala la "NDOA" bwana tumia akili Sana alizokupa mwenyezi MUNGU
Kwa Mfano:
1. Kabla haujaolewa kuna Yale mavazi ilikuwa unatupia mumeo akakutamani nayo anakuweka kichwani ukamchanganya mpaka akakuwowa! Yale mavazi skuhizi mbona hauvai, hata mkiwa na mumeo wawili?!
2. Yale mauno ulikuwa unayakata kabla hujaokoka Kwa mumeo, skuhizi mbona haumkatii unasema Mungu hapendi?
3. Yale maneno machafu yaleeee... Ulikuwa unamwambia mumeo mpaka anasimamisha mkiwa wawili chumbani, mbona skuhizi haumuongeleshi tena?! Kisa umeokoka au?! Jamani mnafeli wapi wenzetu??
4. Ule utundu utundu ule WA tendo la ndoa, ulokuwa unaufanya sebuleni, kwenye gari, jikoni, bafuni, ulikuwa ukimchanganyia NAO mumeo katika kukoleza penzi Lenu, mbona skuhizi hauufanyi?? Shetani gan amekubadilisha?
Ndio Biblia umesema Ndoa na iheshimiwe na watu wote, lakini haijasema uonekane mchovu na kilaza WA Mapenzi au ukaushe "OUR SEX LIFE katika ndoa yetu au uanze kunihubiria Kila unapoambiwa na mume umpe Haki yake pale linapokuja swala la Unyumba ndani ya ndoa.
Msimpe shetani nafasi walokole wenzangu, me kwenye swala la Unyumba na tendo la ndoa ulokole naeekaga pembeni Kwanza, staki mchezo kabisa





nipo serious

Tena nahakikisha kiuno nakikata kama feni mbovu




Au nakosea wajameni?!
Nipo hapa ofisini narekodi kipindi cha YouTube cha kuhusu ndoa ya waliookoka na wasiookoka ipi inapendeza zaidi??