Ndoa ni baraka kwa walio na bahati nazo

Ndoa ni baraka kwa walio na bahati nazo

Vitu viwili tu kwenye ndoa vitasababisha ndoa kuvunjika au vitaamua hatma ya kila mmoja wenu,uaminifu baina ya mwenza na mwenza kingine heshima baina ya wanandoa hasa wanawake.

Mkivimudu hivyo mengine yote yanazungumzika so kijana unapooa au kuolewa jua nguvu zako nyingi utazielekeza humo kama sivyo lazima utatoa milio.
 
Kwanza pumzika, toka kwenye hizo bandika bandua. Hazikusaidiii
Pili take time upone kwanza, tatu jiangalie jikague ni tabia gani au udhaifu gani unao mpaka wakawa wanakupelekesha

Nne kama ulikuwa unaoa kwa sura , jitafakari upya kaka. Omba ushauri kwa watu wazima watakwambia mke yukoje

Ondoa matamanio ya mionekano
Ukweli nilikuwa naangalia sana sura, shape. Na nikawa najiamisha nitamudu.. ila wana heka heka. Asante sana kwa ushauri wako . Nipone kwanza
 
'Ushauri kwa wakaka mahusiano siyo hija mwanamke msafi yupo kwenye filamu za kuigiza, ndoa yako inapo yumba jiongeze mwanamke shetani ukitaka malaika mtengeneze'

DIZASTA VINA.
 
Ndoa inaweza haribu maisha ya mtu, ndoa inaweza fanya ukachanganyikiwa ( itategemea umenyooshwaje na mwenza wako ), ndoa inaweza fanya ukapata kiharusi au magonjwa ya moyo au depression.

Leo siamini amini, nimejikuta navizia kuchukua namba ya wahudumu kucheza na low profile , wakati nilikuwa napenda toto classic, sasa hivi naziogopa kama kifo dah .. inasikitisha sanaa . Ndoa noma sanaa, mapenzi ukijifanya unapenda unaweza kufa kabla ya mda wako
Na yanauma kweli kweli 😂😂
 
Nimekaa mahala hapa, nakunywa chai. Nimewaza mbali sana mkuu. Nilikuwa nimeoa, mwanamke mzuri sana, akazingua kinoma kidogo nichanganyikiwe.

Nikaja pata mwanamke mzuri sana mwingine nikaona huyu ananiponya maumivu nikakubali kuishi hadi nje ya nchi kwa ajiri yake, na rasta zangu nikanyoa.. lakini kaninyooshaa ananipelekesha.. hadi nimeamua kunyoosha mikono, katumia sana ndoa yangu iliyopita kunipigia
Yaani kama ulikubali kwenda nje ya nchi kulelewa lazima upelekeshwe tu
 
Back
Top Bottom