Ndoa ndoano

Ndoa ndoano

laussane

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2009
Posts
255
Reaction score
132
JERUHIWA BAADA YA KUMWAGIWA MAFUTA YA KULA MWILINI KUTOKANA NA MGOGORO WA NDOA

Lugano Mwambuja(50) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya. akiwa amelala nyumbani kwake akiuguzwa majeraha ya moto

Mama mzazi Lugano akimuuguza mwanae

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mwanamke mmoja Mkazi wa Mtaa wa Ilembo kata ya Iyela Jijini Mbeya amemjeruhi mume wake baada ya kumwagia mafuta ya moto kichwani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ndoa baina yao.

Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Beatrice Lusamba (37) alitenda tukio hilo mwishoni mwa wiki majira ya saa saba mchana ambapo alimwagia mafuta hayo Mume wake Lugano Mwambuja(50) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.

Akizungumzia tukio hilo Mhanga wa kisa hicho alisema yeye makazi yake yako Wilayani Ileje lakini Mkewe pamoja na baadhi ya watoto wake huishi Jijini Mbeya hivyo hufika nyumbani hapo mara chache kwa ajili ya kutembelea familia na kupeleka huduma mbali mbali kama baba wa familia.

alisema siku ya tukio alialikwa na Mkewe huyo kula chakula cha mchana ambapo baada ya kukaribishwa ndani mwanamke huyo aliingia jikoni akiwa na mayai matatu na galoni la mafuta ya kupikia, ambapo yeye alibaki Sebureni akisubiri chakula alichokaribishwa apikiwe.

Alisema baada ya dakika kumi Mkewe huyo alirejea Sebuleni akiwa ameshika kikombe chenye mafuta yaliyochemshwa ambayo alimwagia mwilini na kisha kukimbilia nje akimwacha mumewe akiugulia maumivu makali yaliyotokana na kuungua na mafuta ya moto mwilini mwake.

Mwalimu huyo aliongeza kuwa baada ya kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo alipojitokeza jirani yake aliyefahamika kwa jina la Andamisye Kajange ambaye baada ya kumuona katika hali hiyo alimkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya alikopatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Mjumbe wa Mtaa Ilembo, Philly Mwakapimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kabla ya kupeleka Hospitali Mhanga waliripoti Kituo cha Polisi na kupewa fomu namba tatu (PF3) pamoja na kufungua faili namba IR/2253/2014 na kuendelea kutibiwa.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa hajakamatwa hadi leo baada ya kutorokea kusikojulikana huku lawama likipewa Jeshi la Polisi kutokana na kushindwa kumkamata mtuhumiwa kwa wakati hadi anapata mwanya wa kutoweka katika eneo la tukio.

Akizungumzia mahusiano yake na mkewe Mwalimu huyo alisema alioana na mkewe mwaka 2007 kwa ndoa ya kimila baada ya kufiwa na mkewe wa awali mwaka 2006 alimyemwachia watoto wawili ambao ni Doris(20) na Happy Mwambuja(21) ambapo aliamua kuoa mke huyo kwa ajili ya kusaidia malezi ya watoto hao.

Alisema akiwa kazini mara nyingi alikuwa akipata taarifa za mgogoro kati ya mkewe huyo na watoto jambo lililosababisha usuluhishi wa mara kwa mara kufanyika ukiongozwa na Serikali ya Mtaa huku sababu ikibainika kuwa ni tamaa ya mwanamke huyo kutaka kumiliki Nyumba ya Mwalimu huyo ili iwe mikononi mwake na siyo Familia.

Alisema mara nyingi Mwanamke huyo amekuwa akijaribu kuiba hati ya nyumba ili abadilishe majina na umiliki lakini anashindwa hali iliyoml;azimu Mwalimu huyo kuamua kununua eneo lingine na kujenga ili kumtengnisha mkewe pamoja na watoto lakini hali bado ilikuwa tete baada ya mwanamke huyo kutaka amilikishwe yeye nyumba.

hadi sasa Mwalimu huyo anaendelea kupatiwa matibabu Nyumbani kwake huku Jeshi la Polisi likiendelea kumsaka mtuhumiwa kwa ajili ya kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu shtaka la kujeruhi kwa makusudi.

mwisho.
 
mmh jamani,hivi kwa nini usiruhusu kuachana than kujitafutia kifungo au kufa
 
Hatari hii...lazima kuna tatizo kubwa kati yao.
 
^^
Haya wanawake shangilieni, mwenzenu kafanya mpendayo
^^
 
Nia ilikuwa amuue ili arithi hizo nyumba, jamani :A S 13:
 
ni wanawake wachache sana wenye roho mbaya ya namna hii kati ya wanawake 100 watapatikana 3 tu, kwaiyo hatuna cha kushangilia

^^
Kipo cha kushangilia kwa sababu, humu jukwaani ikija mada ya mwanamke kupigwa hata kofi, thread nzima itajaa kwa kashifa na laana za kutosha kana kwamba wanawake wote ni innocent !! Mf. Kuna mada ya Ablessed amewahi kuleta hapa, ni mimi peke yangu niliyesimama kusema wazi matendo kama haya hata wanawake hufanya. Sasa leo mfano huu hapo juu, wanawake wapo kimya, wanasoma na kutoweka! Ndio maana nasema, shangilieni maana mmepata wa kuwakilisha mawazo yenu kwa vitendo
^^
 
Last edited by a moderator:
Huku sio kutafuta haki, huu ni uuaji kwakweli....
Haki tunayotaka wengine si ya kumiliki nyumba iliyojengwa na mwanaume, NEVER...

^^
Lakini si mnasema hata mwanamke kumpikia mume tu ni mchango tosha wa kugawana mali? Na asipokubali kuitoa, roho yake halali yako?
I think its your time to celebrate, Women !!
^^
 
ni wanawake wachache sana wenye roho mbaya ya namna hii kati ya wanawake 100 watapatikana 3 tu, kwaiyo hatuna cha kushangilia

I think, the opposite is true...............am sorry
 
^^
Kipo cha kushangilia kwa sababu, humu jukwaani ikija mada ya mwanamke kupigwa hata kofi, thread nzima itajaa kwa kashifa na laana za kutosha kana kwamba wanawake wote ni innocent !! Mf. Kuna mada ya Ablessed amewahi kuleta hapa, ni mimi peke yangu niliyesimama kusema wazi matendo kama haya hata wanawake hufanya. Sasa leo mfano huu hapo juu, wanawake wapo kimya, wanasoma na kutoweka! Ndio maana nasema, shangilieni maana mmepata wa kuwakilisha mawazo yenu kwa vitendo
^^

Hakuna cha kushangilia hapo tunahuzunika tu maana hii kitu mbaya na na si ya kuishangilia, kama issue ni kuja juu sababu ya wanawake kupigwa acheni kutupiga, mwanamke hupigwa ka kanga sio makonde, mikanda, mateke aaah hapo lazima tutakemea kama tunavokea tendo la picha hapo juu
 
^^
Lakini si mnasema hata mwanamke kumpikia mume tu ni mchango tosha wa kugawana mali? Na asipokubali kuitoa, roho yake halali yako?
I think its your time to celebrate, Women !!
^^

Swala la kugawana mali za mwanaume hata kama ni wanandoa, sio swala la kutazama juu juu tu kama wanawake wengi wanavyofikiria.
Unaweza ukaolewa na usipate chochote.
Wengine hatuhitaji mali ya mwanaume ama shilingi zake, we need respect. Nyie wanaume mnatuhumiliate sana kivitendo na kimaneno. Huyo mwanamke akikamatwa, si ajabu kutakua na mengi zaidi ya nyumba and at the end, she was provoked though simsupport kwa alichokifanya.
 
mwanamke kamili yukoje?

Kwanza mwanamke ni lazima hajieshimu na pia haeshimu jamii inayomzungua, pili ni lazima ajue responsibilities zake akiwa kama mama, mke, mtu anaetegemewa kuwa kioo kwa jamii nzima, mtu anaetegemewa kuwa mwalimu kwa generation inayokuja... tatu...
Hiyo yatosha kumfanya mwanamke aweze kufikiri kabla ya kutenda...
 
Je wewe ni mwanamke "kamili"?
 
Hakuna cha kushangilia hapo tunahuzunika tu maana hii kitu mbaya na na si ya kuishangilia, kama issue ni kuja juu sababu ya wanawake kupigwa acheni kutupiga, mwanamke hupigwa ka kanga sio makonde, mikanda, mateke aaah hapo lazima tutakemea kama tunavokea tendo la picha hapo juu

^^
Eti mwanamke hapigwi kwa makonde ila kwa kanga?? Mwanaume yeye ndo hupigwa hivyo??? Kuna wanawake hapa jukwaani isije mada ya mwanaume kumpiga mkewe, watatoa maneno mpaka unaogopa!
UKWELI NI KUWA
Wanawake nyie ni viumbe wa ajabu sana, hapa mnajifanya kuingiwa na huruma, upole, masikitiko n.k lakini alichotenda mwanamke huyu hapo juu, ndio uhalisia wa wanawake wengi waamuapo kutetea mnazoita haki zenu. Heri huyo kaacha majeruhi, kuna wengine wanaua kabisa.
Ikowapi timu ya utetezi wa wanawake waje wafanye Party hapa?
Munkari Husninyo Heaven on Earth Lala 1 ladyfurahia badiebey Evelyn Salt Kaunga venine n.k Njooni mtoe pongezi zenu kwa mwanamke mwenzenu
^^
 
Last edited by a moderator:
Swala la kugawana mali za mwanaume hata kama ni wanandoa, sio swala la kutazama juu juu tu kama wanawake wengi wanavyofikiria.
Unaweza ukaolewa na usipate chochote.
Wengine hatuhitaji mali ya mwanaume ama shilingi zake, we need respect. Nyie wanaume mnatuhumiliate sana kivitendo na kimaneno. Huyo mwanamke akikamatwa, si ajabu kutakua na mengi zaidi ya nyumba and at the end, she was provoked though simsupport kwa alichokifanya.

^^
Awe mwanaume au Mwanamke, hapa tumeletewa endresult ya maamuzi yake, na hoja yangu hapa ni kuwa, SHANGILIENI maana mmepata mfano wa kuepuka humiliation za maneno na matendo ya wanaume
^^
 
Back
Top Bottom