Ndoa inayumbisha uchumi wa vijana

Ndoa inayumbisha uchumi wa vijana

Yawezekana umeoa na kujikweza (umeoa ambaye sio size yako, au ulijikweza kabla ya kuoa) na sasa unashindwa kuishi uhalisia.

Nashauri vijana ishini maisha ya uhalisia tu. Ishi na kula bata kwa namna ulivyojaliwa kipato chako.

Ikikubidi kupunguza bata, fanya hivyo. Maisha ya ndoa hayako ndotoni au katika mawazo...ni marahisi kama uko mkweli wa nafsi yako, kipato chako na wategemezi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madame Mwajumaaaaaa..... mimi nilioa Housewife kabla ya kuoa nilikuwa na kilo 67 ndani ya mwaka nikafika 78 nikaanza kupiga na Gym, nilikuwa nimechoka sana hata ukiniangalia usoni unaona kabisa huyo broo kachoka. Baada ya kuoa nikawa full handsome. Nilikuwa nafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana ambao sijawahi kuwa nao. Mabosi wangu walinielewa kwa utendaji kazi wangu wakanioa na cheo na mshahara ukawa double. Wafanya kazi wenzangu maofisini kila mara walinishangaa utendaji wangu. Wengine walidhani labda natumia Ndumba. Nilikuwa nang'aa kupita maelezo kuanzia mavazi unywele hadi unyayo. Kiufupi nikawa mtanashati. Mafisi( mademu wasangaji) wakaanza kunivizia kila mara ofsini na mitaani ilikuwa gumzo. Mafanikio yakaja haraka sana kuanzia kipato, kijamii, na kiprofessional.

Nilianza kufurahia maisha kuliko mwanzo. Mke wangu hakutaka kusikia H/girl ndani ya nyumba yake kwa kuwa nikuongeza gharama za bure wakati yeye ni H/wife.

Nilimpenda mke wangu kwa uchapakazi na mahaba aliyokuwa ananipa maana yameniletea mafanikio makubwa.

Wengi hawaelewi nilimpata vipi. Vijana wenzangu wakija kwangu wananiuliza eti vipi ulipataje Zali hivi ukapata mke huyu. Nikawambia sina fomula ni bahati tu. Lakini usije ukaoa na wew h/wife ukadhani ndio utafanikiwa , oa yeyote mwenye mapenzi mema utafurahia uumbaji wa Mungu duniano. Hapo sijataja neno lolote kuhusu mambo yaleeeeeee ya akina Madam Mwajuma.
ama kweli mabosi wako walikuoa
 
Back
Top Bottom