Ndoa imenizawadia kiharusi


Kumfukuza mtu asiye na nidhamu kwenye taasisi yoyote ni uamuzi wenye Tija siku zote.

Kama Mungu alitufukuza Edeni Kwa upuuzi tulioufanya Nini kinamzuia Mwanaume kumfukuza Mwanamke asiye na adabu? Watoto sio kizuizi.

Ndoa ni taasisi kama taasisi zingine inakamuni na taratibu zake.
Huko Kanisani Kwenye kuna mapadri wanafukuzwa wakikosa Maadili, huko serikali Kila siku tunaona. Kwenye vyama vya siasa halikadhali.

Kumfukuza mtu asiyemeet mahitaji ya taasisi sio udhaifu wa mtawala Bali ni majukumu ya mtawala.

Na ndio maana unaambiwa Mwanaume ni mtawala. Hilo neno mtawala ukianzisha hata Kampuni au ukiwa na uongozi mkubwa katika serikali utalielewa linamaana Gani.
 
Picha pls
Sio kisendoff
 
Pole sana mkuu. Shida uliruhusu kusomeka. Uliruhusu huo upole. Uliruhusu wema kupitiliza ukampa nafasi ya kuijaribu nafsi yako.

Wakati mwingine huwezi kujua kuwa mwanamke uliye naye kabla ya ndoa anaweza kuwa sumu, ila pia kwa nyakati tofauti huwa tunapuuzia ishara fulani fulani ambazo zingetuepusha na wenza sumu.

Nimeandika kitabu ambacho kitatoka soon. Kinaitwa Ndoa na Kanuni zake. Hiki kinajribu kuangazia masuala ya awali kabisa ambayo kama aidha yakiepukwa au kufuatwa yatawezesha kwa asilimia kubwa kurekebisha ndoa zetu
 
Leta somo mkuu, ulimpiga matokeo gani.

Au uliiamsha sub ipashe misuli?
 
Tumkabizi Mungu.

Asante sana mkuu.
 
Rafiki yangu Msanii pole sana kwa kila kilichokutokea, tumeongea mengi, zaidi ni kuilinda afya yako ya mwili na afya ya akili,
Hongera kwa uzi huu naimani umewafunza kitu na wengine ambao wanataka kuingia kwenye taasisi ya ndoa,

Wana Jamii Forum tuzidi kumuombea mwanachama mwenzetu afya yake iimarike na kwa wale watakaoguswa kumchangia chochote muongozo utatolewa na uongozi wa Jamii Forum ili tumpige tafu mwenzetu kwenye kipindi hiki kigumu anachopitia.
 
Vijana wa sasa ,wote ,wakike na kiume hawajaandaliwa kwa ajili ya maisha ya ndoa ..Huu ni ukweli mchungu ,sehemu za mafundisho ya dini zinaandaa hizi mada ila hawapati mtu.

Kiukweli ,elimu yetu sio nzuri katika kufikia malengo ya ndoa ..Zile elimu za zamani zinaonekana kama mila potofu ....Vijana wakakutana hapo Dar chuo ,baadaye wanaanza harakati za ndoa hapo washafanya mapenzi mpaka mimba au mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…