Ndoa imenizawadia kiharusi

Ndoa imenizawadia kiharusi

Pole sana mkuu.
Changamoto za ndoa huwa kubwa zaidi pale unapokuwa na watoto.
Ni vipi utawaacha watoto wawe na mzazi mmoja baba au mama , hii kidogo ina leta shida.

Kama wanaume tunapaswa kujua wenzetu ni dhaufu kwa baadhi ya mambo hivyo tunapo lalamika matokeo ya udhaifu wao sisi nasintuna hesabiwa dhaifu pamoja nao.

Kumkimbia mwanamke kisa ana changamoto hizi na zile ni udhaifu, kuathirika kwa sababu ya changamoto za mwanamke ni udhaifu.

Kumfukuza mtu asiye na nidhamu kwenye taasisi yoyote ni uamuzi wenye Tija siku zote.

Kama Mungu alitufukuza Edeni Kwa upuuzi tulioufanya Nini kinamzuia Mwanaume kumfukuza Mwanamke asiye na adabu? Watoto sio kizuizi.

Ndoa ni taasisi kama taasisi zingine inakamuni na taratibu zake.
Huko Kanisani Kwenye kuna mapadri wanafukuzwa wakikosa Maadili, huko serikali Kila siku tunaona. Kwenye vyama vya siasa halikadhali.

Kumfukuza mtu asiyemeet mahitaji ya taasisi sio udhaifu wa mtawala Bali ni majukumu ya mtawala.

Na ndio maana unaambiwa Mwanaume ni mtawala. Hilo neno mtawala ukianzisha hata Kampuni au ukiwa na uongozi mkubwa katika serikali utalielewa linamaana Gani.
 
Great Thinkers
Kama heading inavyojieleza; mimi Msanii nimeoa na pia tumejaliwa watoto 2. Ninawapenda sana hawa watoto. Naamini ni zao la ndoa yetu.

Wengi wanaonifahamu, wanajua mapito ninayoyapitia kwenye hii ndoa. I tried so hard to humble myself na kuwa kiongozi wa familia kwa kutotumia misuli ya mwili dhidi ya matumizi ya akili kwenye hii ndoa.

Kwanza kabisa, naomba kudeclare my position kwamba, matendo au matukio ya mwanamke mmoja au mwanaume mmoja siyo justification ya tabia za jumla kwa wanawake ama wanaume wote.

Kikubwa ni kwamba nawaasa vijana wanaotaka kuingia kwenye mahusiano ya ndoa, wajitahidi kutafuta wenza wanaoendana nao. Usisite kuachana na toxic relationship. Ni bora usieleweke na jamii lakini ukaelewa kile unachokifanya kwa manufaa ya nafsi yako. Bahati mbaya sana tumezitosa mila na tamaduni zetu tumezipiga chini kwa ujumla wake. Badala ya kuchagua desturi nzuri na kuachana nazo zile mbovu.

Ndoa yangu haipo katika good shape. Mitikisiko ninayokumbana nayo imenipatia stress na sasa ninaishi kwa Neema za Mungu baada ya kupigwa stroke (kiharusi). Bado ni mwanaume kamili lakini nimejirudi ktk abstaining lane kwa sababu kwa sasa nailinda sana nafsi yangu over tamaa za mwili. Mwaka wa nne sasa nimemuweka mbali shemeji na wifi yenu. Sijaachana naye lakini nina amani yupo mbali kwa sasa.

Niliamua kuwa mkimya kwa muda mrefu sana, Namshukuru binafsi rafiki yangu Dr. Mariposa kunichomoa mafichoni.

For the sake of humility and long healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu.

Msanii wa JF
Picha pls
Sio kisendoff
 
Pole sana mkuu. Shida uliruhusu kusomeka. Uliruhusu huo upole. Uliruhusu wema kupitiliza ukampa nafasi ya kuijaribu nafsi yako.

Wakati mwingine huwezi kujua kuwa mwanamke uliye naye kabla ya ndoa anaweza kuwa sumu, ila pia kwa nyakati tofauti huwa tunapuuzia ishara fulani fulani ambazo zingetuepusha na wenza sumu.

Nimeandika kitabu ambacho kitatoka soon. Kinaitwa Ndoa na Kanuni zake. Hiki kinajribu kuangazia masuala ya awali kabisa ambayo kama aidha yakiepukwa au kufuatwa yatawezesha kwa asilimia kubwa kurekebisha ndoa zetu
 
Mkuu pole sana! Haya mambo wanasema yasikie kwa mwingine! Mimi binafsi namshukuru Mungu mambo yanaenda,mimi Mnyakyusa huyu wangu Muhaya,mwanzoni mwanzoni alileta za nshomile,nikampiga matukio mawili matakatifu akatulia...saiz adabu ipo tunasonga yuko very submissive
Leta somo mkuu, ulimpiga matokeo gani.

Au uliiamsha sub ipashe misuli?
 
Ndoa nyingi zinanmisukosuko lately ila niluambie mimi yangu hiyo misukosuko nilishaikataa tangu mwanzo niliamini katika kumcha Mungu ukipata mwenza mcha Mungu mwenye hofu na Mungu umepata chombo chema na hakika mtabarikiwa especially mkianzia chini kabisa pamoja.

Ndoa yangu ni kama ya Peter Msechu, yani ukiangalia hile ndoa ni kama yangu huwa mimi huwa siruhusu misukosuko ikae na kudumu mimi huwa natatua jambo kabla jua halijazama,ndoa ukitaka iwe nzuri ikabidhi kwa Mungu utaokoa hasara nyingi sana
Tumkabizi Mungu.

Asante sana mkuu.
 
Rafiki yangu Msanii pole sana kwa kila kilichokutokea, tumeongea mengi, zaidi ni kuilinda afya yako ya mwili na afya ya akili,
Hongera kwa uzi huu naimani umewafunza kitu na wengine ambao wanataka kuingia kwenye taasisi ya ndoa,

Wana Jamii Forum tuzidi kumuombea mwanachama mwenzetu afya yake iimarike na kwa wale watakaoguswa kumchangia chochote muongozo utatolewa na uongozi wa Jamii Forum ili tumpige tafu mwenzetu kwenye kipindi hiki kigumu anachopitia.
 
Vijana wa sasa ,wote ,wakike na kiume hawajaandaliwa kwa ajili ya maisha ya ndoa ..Huu ni ukweli mchungu ,sehemu za mafundisho ya dini zinaandaa hizi mada ila hawapati mtu.

Kiukweli ,elimu yetu sio nzuri katika kufikia malengo ya ndoa ..Zile elimu za zamani zinaonekana kama mila potofu ....Vijana wakakutana hapo Dar chuo ,baadaye wanaanza harakati za ndoa hapo washafanya mapenzi mpaka mimba au mtoto.
 
Back
Top Bottom