Nikiwa mmoja ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Kilimanjaro, nimekuwa nafuatilia utendaji wa wabunge waliopo, nilichogundua ni kwamba yale majimbo yalio na wabunge wazee yaani Ndesamburo na Lyatonga Mrema wananchi husika wanajuta kuwachugua kutokana na kutokutekeleza ahadi zao tangu wachaguliwe kuwa wabunge.Mfano mzee Ndesamburo aliahidi kuhakikisha kuwa hospitali ya Mawezi itaoboresha imekuwa ni kinyume chake, Lyatonga Mrema ameshindwa hata kufuatili ujenzi wa barabara ya lami kutoka uchira kupitia kirua hadi marangu.Rai yangu ni kwamba wanachi watumie fursa hii ya kuandaa upya katiba ili kuwezesha wananchi wa jimbo husika wapewe ruhusa ya kuwapigiwa wabunge kura ya kutokuwa na imani na mbunge hasa pale mbunge husika anaposhindwa kuhudumia wapiga kura wake.