Ndege zinamsaidia nini bibi yangu kule kijijini?

Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Ndugu.
Umeongea hoja nzuri ya multiplier effect lakini kwa ununuzi wa ndege the strength of multiplier effect ni ndogo sana ukilinganisha na sectors zeingine ulizotaja!

Kwa mfano, umetaja hatimae ATCL inaweza kuajiri wafanyakazi 18 kutokana na investment ya 61bn plus! Kwenye uchumi huko huko kuna kitu kinaitwa opportunity cost! Multiplier effect ya ununuzi wa ndege 2 itakuwa economically viable endapo no best alternative na hapa concentration ikiwa kwenye hiyo hiyo hoja yako ya multiplier effect.

Ona sasa, multiplier effect yako imeanzia kwa wafanyakazi 18... and it's true, itaanzia hapo! Kinyumee chake, tuchukue sekta moja wapo ya ulizotaja... bandari. Assume pametokea upanuzi. Kwanza kabla ya kuajiri hao wafanyakazi 18; kwenye upanuzi wa bandari utaanza na ununuzi wa sement, nondo, misumari na makororokoro mengine! Hivyo ndivyo hiyo 61 billion itakavyoanza kuwa multiplied kwamba viwanda vyote hivyo vita-pool in revenues from hizo 61bn. Baaada ya hapo, kutakuwa na magari kadhaa yatakayosafirisha hivyo vifaa kwenda bandarini... magari yatakuwa yamejazwa mafuta hapa na pale... mulitiplier effect inaendelea hapo!! Vifaa navyo vitakuwa vimepakiwa kwenye magari na vibarua ambao nao watalipwa ujira na kwenda kula mama lishe, kununua maji ya kunywa, kununua sigara n.k... hiyo ndiyo multiplier effect! Vifaa hivyo vikifika bandarini vitapakuliwa tena na vibarua na kutokea yale yale ambayo yalitokea viwandani... hiyo ndiyo multiplier effect!

Hapo bado hata ujenzi haujaanza lakini angalia 61 billion investment ilivyoathiri economic activities positively!

Ujenzi ukishaanza, hapo tena kutakuwa na vibarua, wauza vyakula, wauza maji n.k! Hiyo ndiyo multiplier effect. Ujenzi ukishakamalika ndo watu wanaanza kufikiria suala la wafanyakazi wa kudumu wakati hiyo 61 billion imeshakuwa reflected in the economy from day one! Na kama itakuwa umejenga container terminal, hapa tena tunatarajia vibarua wa kumwaga, tunatarajia magari yakayoleta na kufuata mizigo ambayo nayo yatakuwa na madereva na matingo... magari ambayo nayo yatakuwa yameshakunywa mafuta ya kutosha na hivyo kuendeleza biashara za wauza mafuta ambao nao watakuwa wanahakikisha ajira za wafanyakazi wao... mlongo mlongo ni mrefu!

Now tell me kwenye hizo ndege katika taifa ambalo lina limited resources ambazo, from economic point of view, hapo unatakiwa ku-invest kwenye the best alternative!
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Msaidie jwanza kutumia kompyuta kwa juhudi zako
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Mkuu Juve, msaada wa hizo ndege kwa bibi yako kule kijijini ni siku ya siku zitakuwezesha wewe kupata usafiri na kuiwahi ile shughuli ya ile sherehe yake maana kufuatia kuwepo kwa usafiri wa ndege wenye fedha zao hamtagombania nao mabasi hivyo kutokana na udharura wa huo mwaliko umeweza kwenda Ubungo na kupata tiketi ya kuiwahi hiyo shughuli kwa sababu abiria wamepungua kufuatia wengi kupanda ndege, kwenye kajamba nani tumebaki mimi na wewe hivyo nafasi bwerere, isn't that good? . Maana vinginevyo mabasi yangeendelea kujaa na wewe ungekosa nafasi, na kule kijijini ni hakuna kulaza!.

Tena kufuatia jamaa kuwa ni Msukuma, tutamshauri kuwafanya Watanzania wote waige tabia za Kisukuma za kuwa na upendo na roho nzuri kwa wote. Msukuma akipata anafurahi, akikosa anafurahi, akipata mwingine anafurahi! . Watanzania tuwe tunapaswa kufurahia kila mafanikio ya yoyote hata kama sio wewe na bibi yako kule kijijini kwenu, furahi hata kwa ajili yangu mwenye pesa za kupanga hiyo ndege hivyo kukupisha wewe ukipata kiti kwenye basi! .

Kuna wenzetu wana tabia za "umimi" na roho ya "kwanini" , umimi ni kila kitu kizuri ni lazima apate yeye, akipata mwingine ananuna, anakasirika wengine hadi anasusa kwa kuumia roho, ya kwanini? .

Nchi yetu ilikuwa haina ndege yetu sasa tumepata ndege badala ya kushukuru ndio kwanza wenye "umimi" na roho ya kwanini wanaendelea kuuliza ndege hiyo itamsaidia nini bibi yake kijijini!. Usikute huyu muuliza muuliza swali ndio wale wale wapanda ndege kila usiku na bibi zao halafu mchana ndio anakuja kuuliza ndege itamsaidia vipi bibi yake!.

Kwenye madudu tulaumu lakini kwenye mazuri tupongeze!.
Pasco
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Lowassa alikuwa sahihi. Mfumo wetu wa elimu ni mbovu vinginevyo hoja zisizo na hoja kama hii zisingekuwa zinaanzishwa.

Hebu tutajie mambo ambayo we na bibi yako mnaweza ku-afford ndiyo tufanye kiwe kipaumbele cha taifa letu.

Huko nyuma wajanja wangekuwa wametia mfukoni pesa hizi na ndege hizi usigeziona. Ufisadi ule wa kutisha ulikuwa unakusaidiaje we na bibi yako?
 
Barabara ya Mbeya -Tabora daa ni kiama lakini et ndege!!!!
 
ama kweli kuna watu na viatu, mtoa mada ni kiatu tena cheusi, kwani bibi yako ni nani hasa mpaka kila lifanyikalo nchini afaidike?
Vipaumbele kwanza vitekelezwe. Hospitals bora tupate afya, Elimu bora, Kilimo bora na Masoko ya kuuzia mazao yetu, Mishahara bora kwa watumishi, Viwanda tupate fedha na ajira walau hata cha kusindika nyanya pale Kilolo.
 
ACHA UBINAFSI MKUU....JIONGOZE....UJIFUNZE KWA KUPITIA WACHANGIAJI WA POST YAKO...
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Kama ukiona hauna unavyotakiwa ili uweze kupanda ndege, ujue sio kwa ajili yako, hata marekani sio wote wenye uwezo wa kupanda ndege, ndege hizi sio lazima upande ndo ufaidike nazo, watu wanaopanda wanaongeza kwa kiasi fulani pato la taifa ambalo baadae hupelekwa ktk huduma za jamii.
Ps: Hongera kwa kuanzisha uzi.
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Walitangaza ajira?
Hapa mm napita tuuu
Cna wadhamin
 
Mkuu kwan lazima bibi yako apande hzo ndege iyali ya kuwa hata huko alipo hakuna uwanja wa ndge..,swali dogo tu ww unasmartphne inamsaidia nn bibi yako kule kijjn?kaka s kila kipatikanacho ktk maendeleo kina msaidia kila mti
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Kwa ufafanuzi wako kuhusu huyo jamaa aliyeuliza ndege inamsaidia nini bibi yake aliyeko kijijni,naomba nikuoe offer ya kinywaji unachotumia mkuu.
 
Zitaleta Wawekezaji, Watajenga Viwanda Na Kuwekeza Mitaji Ya, Ww Mtoto Pori Utapata Ajira Ya Ulinzi Getini, Siku Bibi Akiumwa Utakodi Bajaj Kwa Mshahara Huo Kumkimbiza Hosp.na Hata Kumuhudumia!!! Note Usipende Kuhoji Kila Kitu, Silent Ni Jibu Zuri Pia
 
Nadhani anajuta....kuuliza swali lake hilo bila kushirikisha ubongo! Inatakiwa tufikiri nje ya box...mbali zaidi! Amejuta
Duh! siamini kama kuna mtanzania bado anaweza kuzungumza hivyo, yaani hata shule kidogo hamna. hebu jiulize kwanza serikali inapata wapi fedha kwa ajili ya maendeleo? unadhani ni kodi tu? kalagabaho wewe!!
 
ama kweli kuna watu na viatu, mtoa mada ni kiatu tena cheusi, kwani bibi yako ni nani hasa mpaka kila lifanyikalo nchini afaidike?
Kiatu cheusi ndo kinavaliwa jeshini....nahisi mleta uzi ataeleweka na wachache sana of whom hawatachangia!
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Kwani hii JF inasaidia nini? Wananchi huko vijijin au kila lifanywalo na serikali limesaidia wote vijijin
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Huo ubalozini ubinafsi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom