GE2025 Kesho nitatiki, na hizi ndiyo sababu zangu

GE2025 Kesho nitatiki, na hizi ndiyo sababu zangu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Shiika

Senior Member
Joined
Aug 29, 2024
Posts
188
Reaction score
199
Heshima kwenu Waungwana
Naandika haya, ukiwa ni msimamo wangu binafsi.
Kwamba kesho nitatiki kwa Dr Samia Suluhu Hassani, Mbunge
wa Jimbo langu, na Diwani wa
Kata yangu.
Sababu ni hizi;

1. Maslahi kwa wafanyakazi.
Rais Samia ameboresha maslahi ya wafanyakazi kwa haki.
Tofauti na mtangulizi wake aliyeungana na wananchi wenye nongwa kutuchukia&kutusulubu wafanyakazi.

Kumbuka;
Wafanyakazi ni ndg zenu,jamaa zenu, waumini wenu,wateja wenu...nk

Kwa nini muone nongwa sisi kutendewa vyema?

2. Ni katika kipindi chake tunafanya kazi kwa amani bila vitisho, maslahi yakiwa juu.
Je, kuna muajiriwa hapendi kulipwa vizuri na kufanya kazi kwa amani ndg zangu?

3. Ongezeko la ajira nchini
Ni katika kipindi cha Samia ajira zimeongezeka hadi sekta binafsi.

Kumbuka;
Bomu la ajira alilitengeneza Jiwe wala siyo Samia.
(Na jiwe alikuwa hashauriki)

4. Amepunguza ugumu wa maisha, tofauti na mtangulizi wake aliyetaka watu waishi kama mashetani.

Wenye hela wafirisike
Wanene wakondeane
Pesa iadimike eti ili iheshimike.
Wakazi wa mijini warudishe mpira kwa kipa(Vijijini).

Wafanyabiashara walionwa kama maadui wa taifa.

5. Kaboresha sekta za umma&miundombinu mipya, na aliyoianzisha Jiwe.

Unafikiri angeamua kuipa kisogo SGR, STIGLERS, KIGONGO BUSISI BRIDGE, REA, MASHULE.... angeshindwa?

NB;
Hayo ni kwa uchache tu
Sikatai kuwa hana madhaifu, lakini Mnyonge Mnyongeni Haki yake Mpeni.
Hakuna mkamilifu
Kiongozi yeyote hulaumiwa
Hata kwa ngazi ya familia, viongozi hawapendwi(Mf Baba)

Nashauri, kabla hujamyima kura Samia, tafakari mazuri yake kwanza.... kwa haki.

Mwisho,
Sina ugomvi na Diwani mtarajiwa & Mbunge wangu mtarajiwa, mpya.

Hawa ni watu wema wasio na makuu.
Nitawapigia kura.
 
NAlala😴😴😴😴.

Kwanza sioni faida yake kwangu hasara kesho siingizi kitu. Halafu nikawape wenzangu maisha. ahaa wapi
 
Back
Top Bottom