Poleni na mjadala wa Katiba; mimi leo nimeota rais akiwa anapanda ndege imeandikwa Tanzania Air Force One; akielekea nje ya nchi; Nikiwa njiani kuja hapa kibaruani kwangu nikawaza maswali mengi tu bila kupata majibu sahihi; Je ndege hii ipo wapi? Je ina hali gani kwa sasa? Je ilishawahi kufanya safari ngapi nje na ndani ya nchi? ilinunuliwa bei gani? Nikifika aiport yetu huwa najitahidi sana kuangaza angaza ili walau niione lakini wapi? anyejua anijuze maana mali hii ni yetu sote watanzania.