Ndege ya Rais wetu ipo Wapi?

waziri alisema ikibidi wananchi watakula nyasi ila ndege itanunuliwa
 
Jamani ile ndege ilinunuliwa ikiwa mpya, ilikuwa imeshatumika miaka 20 tu, ambayo kwa ndege bado tunaiita mpya !
 
utabaki hapohapo ulipo wenzako wanasonga mbele wewe baki kuzua umbea tu,utakonda kwa umbea.
ah aaaaaaah taratibu mzazi usije mtoboa macho mwenzio!, istoshe umbea siku hizi mpango mzima kwani unasadikika kuondoa msongo wa mawazo, so kam dauni mzazi:peep:
 
Kuna mwarabu amewa convince kwamba badala ya kukaa tu inachakaa bora aikodi ili serikali iingize mapato, ikaonekana ina make sense.... lakini sasa kwenye mkataba kumbe alichomeka kipengele cha "lease to buy" na anataka kuikatalia...
 
Ni Gulfstream 5, mimi sikuelewa wale waliokuwa wanapinga isinunuliwe, sasa Mkuu wa Nchi angesafiri na nini? Juzi nilisafiri na Quartar Air tulikuwa tumebanana kama ndizi, hata KLM kule economy hakuna ahueni, ile miaka ya 1980 ndege zilikuwa hazijai lakini sasa hali ni mbaya, dala dala kwa kwenda mbele. Labda usafiri Business Class au First Class, kwa gharama zipi?
 
Searching..................................................................................................................
 
Nenda terminal one kwa viongozi utaikuta. Tatizo akisafiri hatangazi anatumia ndege ipi, Ni vigumu kwako kujua, lkn inatumika sn tu
 
wakuu, bado sijapata jibu la kurudhisha juu ya hatma ya hii ndege. mbona watanzania hatuna uchungu ma mali zetu? Nasikia ndege imepaki tu ha haijatumika muda mrefu kwa nini watanzania tusihoji?
 
Poleni na mjadala wa Katiba; mimi leo nimeota rais akiwa anapanda ndege imeandikwa Tanzania Air Force One; akielekea nje ya nchi; Nikiwa njiani kuja hapa kibaruani kwangu nikawaza maswali mengi tu bila kupata majibu sahihi; Je ndege hii ipo wapi? Je ina hali gani kwa sasa? Je ilishawahi kufanya safari ngapi nje na ndani ya nchi? ilinunuliwa bei gani? Nikifika aiport yetu huwa najitahidi sana kuangaza angaza ili walau niione lakini wapi? anyejua anijuze maana mali hii ni yetu sote watanzania.
images
images
images

Mbona sijakuelewa hapo pekundu
 
Back
Top Bottom