Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Habari ndugu zangu,
Hivi karibuni nimeshuhudia mara kadhaa Rais Samia akitoa hamasa kwa timu za Simba na Yanga kwa kutoa zawadi ya pesa kwa kila goli linalofungwa na timu hizo.
Mara ya mwisho nimeona Rais Samia akitoa ndege ya Timu ya Yanga kusafiri mpaka Algeria na kuwarudisha Tanzania.
Jambo hii japo linazua maswali lakini nikalichukulia sawa kwa sababu ni timu zilizokuwa zinaiwakilisha nchi, kwa namna fulani suala la utaufa lilihusika.
Leo hii nimeona Rais wa Yanga Injinia Hersi akisema kwamba Rais Samia ametoa ndege kwa Yanga kwenda Mbeya kumalizia michezo yao ya ligi kuu dhidi ya timu za mkoa huo. Soma: Injinia Hersi: Rais Samia atoa ndege kuipeleka Yanga Mbeya
Je, hizi hela zinatoka kwenye mfuko gani? Je ni sawa Rais kufanya hayo? Na je kama suala ni kupata chakula cha jioni na timu hiyo kwanini asisubiri timu hiyo irejee kutoka Mbeya ili asiingie kutumia ndege ya nchi kuisafirisha timu katika michuano ambayo si ya kimataifa?
Naombeni ufafanuzi mnaojua, natamani kuelewa hili.
Pia soma: GOLI LA MAMA: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF