Ndege inaweza paa injini ikizima angani??

Ndege inaweza paa injini ikizima angani??

Unachosema ni sahihi mana ndege wameweka engine zifanye kazi kila moja kwakutegemea energy or power source yake, kwahiyo ni ngumu sana engine zote zikazima.

Na kama ikitokea zote zimezima ndege inakuwa nzito ila inaweza kwenda upande wowote isipokuwa kwenda juu tena, lakini itaendelea kumove kulingana na its initial velocity.
Siku hizi ndege zinabackup system inayoweza kupressurize system nzima.

Kulikuwa na leakage ya mafuta ndio maana injini zote zilizima
 
The Tomorrow People, ymollel kakujibu vizuri.
Ni kama vile gari ikizima ingine katikati ya safari, depending on the acceleration speed iliyokuwepo ni ujanja wa dereva tu kuisukuma mbele zaidi na kama hamna jam basi ndo kabisaaaa unaburuza tu mpaka mbele zaidi.
Ni hayo tu

Sawa...ila hofu yangu.. Ni kwamba ndege inawezaje kukaa angani isidondoke.....??? Mfano kunguru asipopiga mabawa akaganda tuu si anadondoka?
 
Last edited by a moderator:
Ndege yoyote ile inapaa kwa uwezo wa engines zake.Kama engines hazifanyi kazi haitapaa kamwe.Hapa lazima kutofautisha ndege ikiwa angani ambapo tayari inakuwa kwenye mwendo na ndege ikiwa kwenye runway tayari kuruka.Kinachoipaisha ndege angani ni msukumo wa engines zake kwa kuhusisha shape ya ndege ambayo imetengenezwa ili iweze kuelea hewani (aerodynamic) na zaidi sana flaps zinazodhibitiwa na rubani ili ndege iwe kwenye mwelekeo unaotakiwa.Ndege iwapo angani huwa inasukumwa na engines zake,Kama engines zote zikiacha kufanya kazi inaweza kuelea hewani kwa muda kwa kutumia ile speed iliyotengenezwa na engine zake kabla ya kuzimika.Hii ina maana rubani anaweza kutumia speed hiyo kuishusha ndege na kutafuta sehemu ya kutua kwa dharura.Kuna kitu kinaitwa ''Gliding'', Hiki ni kitendo cha ndege kuelea angani kwa muda fulani bila kuwa na msukumo wa engine.Mfano mzuri wa Gliding ni kama uonavyo yule ndege 'eagle' anapokuwa juu sana angani huwa hapigi mbawa zake ila huwa anaelea angani kwa kutumia ile momentum aliyoitengeneza awali ili kufika juu.Kurudi chini anatumia utaratibu wa kurekebisha mbawa zake za mkiani ili aweze kutua kwa usalama.Ndege (airplane) pia hutumia flaps ambazo utaziona kwenye mabawa yake pamoja na Rudder ambayo iko kwenye mkia wake kwa ajili ya kudhibiti mwelekeo kulia au kushoto.

Asante.. Kwa maelezo mazuri sana... Sasa mfumo wa break wa ndege hutegemea sana nishati inayozalishwa na injini.. Inamaanisha rubani aliishusha ndege ikakimbia yenyewe kwenye running way na kusimama Kwa uwezo wa upepo?
 
kuna kichumba special kwa rais,ndege ikipata hitilafu na haiwezi okolewa wanamkimbizia humo,kisha chumba kinajidetach(kujitenga) na ndege na kuanguka pekee yake kikiwa suppoted na miamvuli kupunguza kasi ya impact kitapoanguka chini.

Ni kweli. Ndege zote, hata bombers na fighter jets zina almost the same limitations kama ndege zingine. Tofauti ni kwenye emergence evacuation process. Fighter jets in case of any problem, pilot anaweza kujiokoa kwa kutumia Ejection seat ie ile seat ya pilot inajinasua kwenye ndege kama alivyokaa na ina uwezo wa kudeploy parachutes za kumsadia kutua vizuri with no or minimum damage. AirForce One pia, though ni ndege za kawaida kama the normal pessenger plans unazofahamu, ziko equipped na systems kibao za kuhakikisha safe passage for all the passengers on board, especially the president.
 
Sawa...ila hofu yangu.. Ni kwamba ndege inawezaje kukaa angani isidondoke.....??? Mfano kunguru asipopiga mabawa akaganda tuu si anadondoka?

Zile bawa za ndege zimeundwa in such a way that ndege inapopata momentum zinazalisha upthrust force (kani mnyanyuo) inayoiwezesha ndege kupaa na kuendelea kuwa hewani. Kazi ya engine ni kuhakikisha ndege inamsukumo wa kutosha kwenda mbele ila ni mabawa ndio yanasababisha iendelee kuelea angani. Ndio maana hata engine zote zikizima, haimanishi ndege itaanguka instantly. Ni mpaka ile force (momentum) iliyokua nayo iishe kabisha. So kama ilikua na momentum kubwa, ilaweza kuendelea kukaa angani kwa muda mrefu tuu. Mabawa ndio kila kitu kwenye ndege, hata kwenye kutua, pilot huwa anayabadilishia uelekeo ila kupata down force ya kuiwezesha ndege kupungua altitude na hatimae kutua. Engine inawezwa kuzimwa any time, mfano fighter jets huwa zinatumia system ya kuzima engine ili kujiepusha na mabomu yenye uwezo wa kusense joto la engine. Ila kunakua na back up generators zinazozalisha umeme na kusaidia operation ya hizo bawa ziendele. Maana bawa zikifail, ndege itaanza kushuka instantly tena kwa kasi ya ajabu hata kama engine zote zinafanya kazi vizuri.

Kitu kingine, 100km kwa ndege ni kitu kidogo saana, hasa kwa ndege kubwa. Ni sawa na karibu 54 Nautical miles, kipimo cha urefu kinachotumika kwenye aviation. e.g Ndege kubwa haiwezi kutoka Dsm kwenda Zanzibar, which is about 86km, sababu ni karibu mno, kwa umbali huo ndege inakua bado inanyanyuka (gaining altitude). So with enough momentum, inauwezo wa kuelea hewani na kumaliza umbali wa 100km kutegemea na ukinzani wa upepo, ingawa uwezo wa kukaa hewani inakua unapungua kwa kasi sababu bila msukumo kutoka kwenye engine, uwezo wa bawa kugenerate upthrust unapungua. So pilot anaanza kutafuta njia (emergence landing) inayoweza kupugunza athali zaidi.
 
hizi daladala zetu zinazopiga ruti za Dar-Zanzibar-Pemba-Tanga ambazo nyingi zina injini moja ni shida!
Siku zote huwa nawaza siku kainjini kakizima itakuwaje
Bcc ZanAir, Auric, Asalaam, Coastal etc!
 
Naomba kuchangia kidogo katika mambo haya
Kuna aerodynamic, kuna four forces thrust-drag, lift-weight
pia kuna Bernoulli principle inayosema as the velocity of fluid(air) increase, its internal pressure decrease, A wing is shape to take advantage of this principle, this reduce the pressure above the wing while the pressure under the wing remain constant, this pressure diff create lift,
pia kuna Newton 3rd law of motion inayosema for every action there is an equal and opposite reaction, the forward motion of the wing and shape of the airfoil create a downwash of air behind the wing

Ukifuatilia hayo utajuwa vipi ndege in a glide, kila ndege ina glide speed yake kulingana na utengenezaji wake
 
Asante.. Kwa maelezo mazuri sana... Sasa mfumo wa break wa ndege hutegemea sana nishati inayozalishwa na injini.. Inamaanisha rubani aliishusha ndege ikakimbia yenyewe kwenye running way na kusimama Kwa uwezo wa upepo?
Ni nadra sana engine zote kuacha kufanya kazi,na hata ikitokea kinachofuata ni kwa rubani kutafuta mahali pa kutua kwa dharura.Mahali panapofaa ni sehemu yoyote iliyo tambarale,baharini,ziwani na wakati mwingine kwenye highways.Kinapotokea kitu kama hicho huwa hakuna ujanja tena zaidi ya ujasili tu na hasa rubani kukumbuka kutumia ujuzi aliojifunza katika drills za kutua kwa dharura wakati wa hatari.Kama ni uwanjani lengo ni kuielekeza ndege sehemu iliyo tambarale ili isereleke kwa kutuma tumbo mpaka hapo itakaposimama yenyewe(berry landing).Hii unaweza kuifananisha na gari,baskeli au pikipiki,inapo-fail breki,huwa hakuna ujanja tena isipokuwa ushujaa wa dereva kuendelea kulimudu gari hadi litakapogonga mahali na kupinduka.Huo ndio unakuwa mwisho wa ajali.:shock:
 
nimeshindwa kuku-quote mkuu hapo juu kidogo.
Nimekuelewa vizuri ila uliposema ndege inaweza kutafuta uwanja yenyewe na kutua hapo umeniacha njia panda kidogo.
Kuna rubani mmoja tulifahamiana mwaka jana kuna maswali kadha wa kadha niliwahi kumwuliza, pamoja na kuwa lugha ya mawasiliano kati yetu ilikuwa ngumu (lugha ya malkia), lakini alisema ndege haiwezi kutua yenyewe bila pilot kwa sababu anapoondoka kwa mf. From point a to b, anapotoka airpot ya point a, kuna form 2 anajaza, 1 (inaitwa notam form) anaijaza na nakala moja inabaki airpot.
Pamoja na mambo mengine atajaza anatoka saa ngapi na atafika saa ngapi, atatumia njia zipi (wana njia zao kama k/koo-makumbusho via tandale uzuri road au kawawa road).
Pia atajaza vituo atakavyopitia na muda atakaopita na kama anaenda nje ya nchi ataeleza mpaka wa tz atauacha saa ngapi, pia ataeleza point b atafika saa ngapi lakini atajaza ikishindikana kutua point b kwa sababu za kiufundi atatua wapi (point c) kwa hiyo hata mafuta anakuwa nayo ya kutoka a-b-hadi c.
mkuu anazungumzia ''kuutafuta uwanja ulipo''
kwa mfano.
Kuna ''key holder'' ukipiga mluzi nayo inaitikia beep beep,hivyo basi kama ilikuwa chini ya gazeti utaiona...ndio sayansi kama hiyo imo ndani ya midege ya kisasa(rubani huweza kutua hata kama kuna hali ya hewa mbaya ...hasa ukungu)
 
Kulikuwa na leakage ya mafuta ndio maana injini zote zilizima

Ndomana siku hizi hata kuwe na leakage gani ya mafuta, engine zote hazizimi, mana kila moja inayegemea source yake ya mafuta.
Kwahiyo ni ngumu sana hiyo leakage itokee kwote.
Ndege hizi kubwa mfano kama ile ya Obama, engine zake zinajifanyia diagonisis kila interval flani na kama kuna tatizo zinasema zenyewe kabla ya hatari kubwa.
 
Momentum yake iliiwezesha kuendelea na safari, pia kiwanja kilikuwa karibu. Pia kufeli kwa injini hakumaanishi kwamba kila kitu kinafeli.

Hapo hatakuelewa unless kapitia yale Masomo yetu. kama alikimbia hatakuelewa
 
Naomba kuchangia kidogo katika mambo haya
Kuna aerodynamic, kuna four forces thrust-drag, lift-weight
pia kuna Bernoulli principle inayosema as the velocity of fluid(air) increase, its internal pressure decrease, A wing is shape to take advantage of this principle, this reduce the pressure above the wing while the pressure under the wing remain constant, this pressure diff create lift,
pia kuna Newton 3rd law of motion inayosema for every action there is an equal and opposite reaction, the forward motion of the wing and shape of the airfoil create a downwash of air behind the wing

Ukifuatilia hayo utajuwa vipi ndege in a glide, kila ndege ina glide speed yake kulingana na utengenezaji wake

Kaka wale vijana wetu wanaokimbia yale Masomo yetu wataelewa ,tumia Lugha raisi kuelewesha kaka.
 
Ni nadra sana engine zote kuacha kufanya kazi,na hata ikitokea kinachofuata ni kwa rubani kutafuta mahali pa kutua kwa dharura.Mahali panapofaa ni sehemu yoyote iliyo tambarale,baharini,ziwani na wakati mwingine kwenye highways.Kinapotokea kitu kama hicho huwa hakuna ujanja tena zaidi ya ujasili tu na hasa rubani kukumbuka kutumia ujuzi aliojifunza katika drills za kutua kwa dharura wakati wa hatari.Kama ni uwanjani lengo ni kuielekeza ndege sehemu iliyo tambarale ili isereleke kwa kutuma tumbo mpaka hapo itakaposimama yenyewe(berry landing).Hii unaweza kuifananisha na gari,baskeli au pikipiki,inapo-fail breki,huwa hakuna ujanja tena isipokuwa ushujaa wa dereva kuendelea kulimudu gari hadi litakapogonga mahali na kupinduka.Huo ndio unakuwa mwisho wa ajali.:shock:

Mkuu hujajibu swali ladada pale juu, mana yeye alichohitaji ni power inayotumika katika mfumo mzima wa landing include brake.

Ndege nyingi zinapotua hazitumii ile power inayotokana na engine, lakini zinatumia power ya APU battery iliyo kwenye turbine engibe ya nyuma, mfano li Boeing 787 angalia Boeing wenyewe walivyosema.

"Other power sources for the 787 include the main battery, used primarily for brief ground operations and braking"
 
Kaka wale vijana wetu wanaokimbia yale Masomo yetu wataelewa ,tumia Lugha raisi kuelewesha kaka.

Dada yani mambo ya momentum na Newton laws yanayofundishwa form one na two, leo hii mtu ndo asielewe, labda punguza kujikuta.

Ungenambia mambo ya Bernoulli principle sawa mana yanapatikana form V kwa elimu yetu hii duni.

Na ukifuatilia vizuri alichokisema mkubwa hapo juu ata aliyesoma mwenyewe ataona ni hakuna alicholenga zaidi ya showOff.
 
mkuu wengine tulikimbia hayo masomo toka tupo form one. kwa shule zenu sawa .topic nilisoma mimi ni Measurement tu. sijui zaidi ya hapo kaka .
 
Hayamambo.ndioyanafanya wafanya biashara wa bongo kujaza hirizi kwenye mabegi kuepuka injini kuzima
 
Back
Top Bottom