Ndani ya muda mfupi nimekosa Imani na tume ya mipango

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Juzi nilimsikiliza waziri wa mipango akiongea clouds nilishangaa sana waziri wa mipango anaongea habari ya ajira kama ambavyo kila layman anaongea. eti anasema serikali haitoi ajira watu wajiaijri.

Mimi siamini kama vijana wanakosa ajira, wanakosa kwa sababu ya kukataa ajira za sekita binafsi wanataka kuajiriwa serikalini. Lakin pia siamini kama kuna kijana anaona kuna shughuli ya kumuingizia kipato lakini anaikataa akisubiri kuajiriwa.

Sisi ma layman katika mipango hizo ndizo hadithi zetu kuwasingizia wenye kukosa ajira kuwa wao ndiyo wenye tatizo lakini serikali kwa kuwa ina watu wenye busara wakaona hapa kuna tatizo linaloweza kuwa linatokana na mipango. Wakashauri iundwe tume ya mapango.

Lengo la kuunda tume na wizara ya mipango ni kukusanya ma "guru" katika mipango wakae watafute majibu.

Maana yake waziri wa mipango unapokwenda kuongea kwenye media huwezi kuja na hadithi ambazo hata ukimchukua msukumawa darasa la saba anaongea hayo hayo ya serikali haitoi ajira bali unakuja na,mkakati wa kumaliza tatizo la Akira. Kama kiongozi wa mipango hauna majibu pengine hakuna haha ya kuwa na wizara au time ya mipango kutatua matatizo yasiyokuwa na majibu.

Sasa Leo waziri kaibuka anaunganisha na kufuta mashirika.

Sisi wahandisi huwa ukimkabidhi mtu site ya ujenzi, akakimbia kuchimba msingi na kujenga nyumba au akaanza kukarabati bila ya kuwana plani nzima ya kile anachotaka kufanya huwa tunatilia shaka.

Huwezi kuja unaniambia unaunganisha tume ya karanga na utafiti wa karanda kea Gia ya kupunguza gharama nikakusifu wakati tume ya vitunguu haipo.

Maana yangu tupeni dira ya sekita ya kilimo mnataka ielekee wapi maana ninyi ndiyo mnatupangia.

Alafu mtwambie ili tufike huko tunahitaji taasisi hizi zenye majukumu haya, twatu binafsi na mashirika mchango wao au majukumu yao yatakuwa hivi.

Yani tupate Ile chain Nzima ya uzalishaji katika kilimo na kila mdau ajione mahitaji na majuku. Ndipo tuanze utekelezaji.

Kwamba kwa mujibu wa mango wetu, tume ya nyanya, tume ya maharage na bilinganya zinavunjwa lakini mazao yote yenye jamii fulani yatakuwa chini ya huyu. Huyu kazi yake ni kudhibiti labda ubora wa mbegu, kmatumizi sahihi ya mboleavna viuatilifu, kuhamasisha utunzaji sahihi na uchakataji....

Yani tunachotaka ni mpango iliyokamilika halafu tuingie utekelezaji, siyo leo mnapanga na kupangua mashirika na mpango ukikamirika mnakuta hata mliyounganisha hamyahitaji.

Ushauri wa bure ni kwamba hii wizara na tume yake hiyo ndiyo uti wa mgongo wa taifa.

Hiyo wizara na tume ajirini wachumi wastaafu kutoka asian tigers ambao walishiriki kuzitoa nchi zao hatua ya kwetu kufika walipo sasa na kwa sasa wamestaafu, wachanganye na wabongo vijana. Kwa nini vijana? ni kwa sababu vijana bado wako ready kujifunza, siyo wabishi na kijana hajisikii vibaya kukosolewa. Sisi wazee tushakuwa samaki wakavu, ni ngumu kutubadiri mindset, unaweza kuleta wataalamu bado watahodhi maamuzi na kutumia wageni kama muhuri tu.

Ndani ya miaka 10 tutajenga a new culture ya kupanga katika nchi.

Lakini kuunda taasisi tukaweka watu walewale tutaendelea kufanya yaleyale kwa tittle tofauti.

Just thinking loud kwa maana ninachokiona kikifanyika chini ya time ya mipango hakina tofauti na yale tuliyokuwa tukiyafanya siku zote isipokuwa tunayafanya kwa msukumo tofauti
 
Uamuzi wa kuungasha NIDA na RITA ni wa busara sana kudos Kwa serikali... Kwanza NIDA ingefutwa kabisa wale watoa vyeti vya kuzaliwa yaani RITA wangepewa kazi ya kutoa national ID. NIDA ilikua taasisi ya hovyo kuwahi kufahamu wapo wawili wao na takukuru
 
Hakuna Nchi Duniani Imewahi maliza tatizo la Ajira.Kasome Labour Economics na Unemployment problem kwenye uchumi utapata jibu
Kama mimi ningekuwa nafanyisha usali wewe kwa jibu hili ungekuwa umefeli interview.

watanzania wanachokitaka kusikia kutoka watu wa mipango ni kwa namna gani tutatengeza ajira.

Kitabu kimeandikwa na mtu mwenye mindset kama ya kwako na hao Sisi hatuwahitaji tunachotaka ni wanaosema it is possible na wapo.

Cha msingi ni kutushawishi how na tuone kama tunakubaliana nao
 
Hakuna Nchi Duniani Imewahi maliza tatizo la Ajira.Kasome Labour Economics na Unemployment problem kwenye uchumi utapata jibu
Jibu la mpumbavu..nature, causes, size, outcome na intensity ya tatizo la ajira ni tofauti kwa kila nchi, na hivyo namna ya kutatua ni tofauti kulingana na parameters hizo..utasemaje habari ya kumaliza tatizo km kuna tofauti km hizo, zipo nchi zina tatizo la ajira lkn halina madhara kwa uchumi ndio maana wanaweza kulipa posho za mwezi kwa wasio na kazi..
 
Uamuzi wa kuungasha NIDA na RITA ni wa busara sana kudos Kwa serikali... Kwanza NIDA ingefutwa kabisa wale watoa vyeti vya kuzaliwa yaani RITA wangepewa kazi ya kutoa national ID. NIDA ilikua taasisi ya hovyo kuwahi kufahamu wapo wawili wao na takukuru
Achana na fikra za kutazama maamuzi kwa kutizama utendaji wa NIDA yawezekana kuna taasisi nyingine inahitaji kuingizwa au tunahitaji approach mpya.

Sasa hivi tulitegemea kumsikia waziri akifafanua sera mpya za mpango ambazo ndiyo approach tutakayotumia kwa wataalamu kukaa kusema hili liwekewe utaratibu huu.
 
Back
Top Bottom