Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
MBUNGE KWAGILWA: TUWE NA TUME YA MIPANGO YA KUDUMU
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga, Kwagilwa Ruben amesema, umefika wakati kwa Tanzania kuwa na Tume ya Kudumu ya Mipango ili kuwa na chombo cha kupanga maendeleo ya Taifa kwa kipindi kirefu tofauti na ilivyo sasa.
Akiwasilisha mada kuhusiana na Tume ya Mipango na namna bora ya kuwa na mipango ya kitaifa, Kwagilwa ambaye pia ni Mtaalam wa Mipango amesema, tume ya mipango imekuwa ikihama hama jambo ambalo halitoi nafasi kwa tume hiyo kupanga mipango ya kitaifa.
Kwagilwa amesema, kukiwa na Tume ya kudumu ya mipango kutarahisisha upangaji mipango ya maendeleo kwa kipindi kirefu na ufuatiliaji wake utakuwa rahisi kutokana na chombo hicho kuwa cha kudumu.
Kongamano la Wanamipango 2023 linafanyika kwa siku nne mkoani Arusha na linawakutanisha Wanamipango kutoka taasisi, idara, wizara na halmashauri zote hapa nchini.