Dkt. Slaa, Mdude, Madereka na Mwabukusi kujumuishwa kwenye tume ya mipango?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,285
Kichwa cha habari kinajieleza. Wakati Rais Samia akipokea ripoti ya Tume ya Haki Jinai aliagiza kuwa watu wote wanaokosoa kwa hoja wajumuishwe kwenye tume ya mipango. Badala ya kutekeleza agizo la rais, polisi wamewakamata watanzania hawa na kuwafungulia mashitaka ya uhaini.

Tume ya Haki za Binadamu wanatafsiri uhaini kuwa ni kitendo cha kutishia au kutaka kumuua rais au kutaka kuvamia na kuipindua nchi. Kwa mujibu wa tafsiri hii, watanzania hawa wanne waliokamatwa hawajatenda kosa lolote la kiuhaini bali wamekamatwa kwa sababu ya kukosoa kwa hoja. Na hiki ndicho alichosema Rais Samia kuwa watu wanaokosoa kwa hoja wapewe kazi kwenye tume ya mipango ili wasaidie kuendeleza nchi kwa mawazo yao chanya.

Watanzania wote tunatoa wito kwa vyombo vinavyowashikilia watu hawa waawaachie mara moja na kuwaajiri tume ya mipango kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Nawasilisha.
 
Kukosoa kwa hoja kunapendeza lakini hoja hizi zisiwe za kumpinga Samia, kama ni za kumpinga na majibu yake yapo hakuna shida, lakini kama ni kumpinga na majibu hayapo kwasababu ameshakula vya watu, hapo wasitegemee kujumuishwa kwenye tume yoyote ile.
 
Kwa hiyo wewe mkuu unaona wanastahili kufunguliwa mshataka ya uhaini badala ya kujumuishwa kwenye tume?
 
Back
Top Bottom