ARUSHA: Waziri Mkuu Majaliwa awataka wataalamu wa Mipango nchini kutekeleza Majukumu waliopewa kwa kuwa wao ni kiingo mujimu chama maendeleo nchini

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Na Joseph Ngilisho Arusha

WAZIRI mkuu,Kassimu Majaliwa,amewataka Wataalamu wa mipango Nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu waliyopewa Kwa kuwa wao ni kiungo muhimu katika maendeleo ya nchi.

Majaliwa ameyasema hayo kwenye hotuba yake ilitosomwa na Naibu wake,dkt Doto Biteko,wakati wa kufungua kongamano la Wataalamu wa mipango Nchini linalofanyika Ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC Jijini Arusha

Alisema kuwa hilo ni kongamano la kwanza kufanyika Nchini tangia kuanzishwa Kwa tume ya mipango pamoja na Wizara ya mipango hivyo akaipongeza Tume hiyo Kwa kuwakutanisha pamoja wataalamu wa mipango kwenye kongamano hilo.

Alisema kuwa kongamano hilo la siku nne ni muhimu kwa kupanga na kutekeleza kulingana na kauli mbiu ya kongamano hilo ambalo litafikia Kikomo Novemba 30 lenye kauli mbiu isemayo "fikra za pamoja na utekelezaji ulioratibiwa kwa ufanisi '.

Alisema kuwa mipango wanayoipanga iwe ndio dira ya taifa na mwelekeo wa nchi na kwa kukuza Uchumi.

Kutokana na umuhimu wa mipango Serikali imeweka msukumo wa pekee inayoweza kutekelezeka ambapo Katika hatua nyingine Serikali imeanzisha Vitengo vyenye tathimini na ufuatiliaji na tathimini na kuongeza uwajibikaji Katika Wizara zote nchini.

Wanamipango wawe mstari wa mbele mipango wanayoipanga ndio iwe Sera ya kuifanye Serikali itekeleze majukumu yake Kwa kuzingatia mipango na sio fikira za mtu

Alisisitiza mambo kadhaa ikiwemo Washiriki hao watumie maarifa kuboresha utendaji wao.wahakikushe wanapeleka Dhana ya ushirikishwaji inayowahusu wananchi,Wakurugenzi wa mipango wazingatie utamaduni wa kuwa na mawazo ya pamoja Katika kupanga mipango ya Maendeleo ya nchi.

Awali Wazirii wa mipango Profesa Kitila Mkumbo,alisema ,kuwa wataalamu wa mipango wanapaswa kujitambua kuwa wao ndio watekelezaji Wakuu wa mipango Nchini.

Aliwataka wapange mipango hiyo mapema Ili ifuatiwe na utekelezaji wake badala ya kutanguliwa na wananchi na taifa lipo katika kuandika dira ya Maendeleo ya taifa .

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida alosema kuwa Kongamano hilo la Wanamipango ni la kwanza tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipounda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na kutungwa kwa Sheria ya Tume ya Mipango ya mwaka 2023.

Aliongeza kuwa Kongamano hilo linalokutanisha Wanamipango kutoka katika nyanja mbalimbali linafanyika wakati ambao uwepo wa Tume ya Mipango utawezesha namna ya kuunganisha mawazo katika utekelezaji wa shughuli za upangaji wa pamoja hasa ikizingatia kuwa kauli mbiu yake ni ‘Fikra za Pamoja na Utekelezaji Ulioratibiwa kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi’.

Ends...

IMG-20231127-WA0029.jpg
 
Na Joseph Ngilisho Arusha

.

Aliongeza kuwa Kongamano hilo linalokutanisha Wanamipango kutoka katika nyanja mbalimbali linafanyika wakati ambao uwepo wa Tume ya Mipango utawezesha namna ya kuunganisha mawazo katika utekelezaji wa shughuli za upangaji wa pamoja hasa ikizingatia kuwa kauli mbiu yake ni ‘Fikra za Pamoja na Utekelezaji Ulioratibiwa kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi’.

Ends...

View attachment 2826900

Screenshot_20231127_200937_Samsung Internet.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom