Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.
Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.
Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.
Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.
Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.
CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
Umetumia vipimo/vigezo gani wewe "wakili msomi" kufikiri, kuandika na kuja na hitimisho la namna hii?
Nadhani ktk mada zote ulizowahi kuposti, hii ni mojawapo ya mada zako nyingi dhaifu zisizofanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kuiachia iruke hewani...
Nakuambia hivi kwa sbb zifuatazo:
Mosi, ni makosa kuilinganisha CHADEMA ya sasa na kizazi hiki na NCCR Mageuzi ya kizazi kile na ya wakati ule kwa sbb ya wakati...
Kwamba, hata hutambui kuwa, time changes na watu Siku zote hujifunza na hubadilika pia kimbinu, kimkakati na kimaono.....
I'm not sure kama wewe unaamini kuwa makosa waliyoyafanya NCCR Mageuzi yaweza kufanywa na CHADEMA hii ya siasa za kisasa ya kizazi cha dot.com...
Kama unadhani Magufuli huyu mshamba wa mikakati ya kisiasa za kileo aweza kuua siasa za vyama strong vya upinzani, nakushauri urudi chumbani mwako ukae na ufikiri tena mara mbilimbili, kisha njoo tena uandike upya...
Pili, hebu rudi nyuma kidogo miaka 8 au 10 nyuma wakati wa JK.
Una reflect kitu gani?
Yawezekana umesahau. Naomba nikukumbushe.....
Kwamba, huko kwenu CCM ndiyo ilikuwa rising generation ya kina Mwigulu Nchemba chini ya katibu mkuu wake Wilson Mkama na yule mzee wa fitna Steven Wassira a. k. a Tyson....
Ndicho kipindi ambacho kauli kalikali kabisa kuliko hii yako kuwa, CHADEMA by 2013 ama 2015 ingekuwa ni historia kabisa....yaani ingekufa kifo cha mende!!
Haikuwa inaeleweka exactly, walikuwa na mikakati gani ya kuua.
Labda kupitia njia za kina Mwigulu Nchemba kuandaa video za kigaidi kwa ambazo in return zili back fire vibaya sana....
Do you remember, what happened eventually? I hope, jibu unalo ktk mtima wako....
Lakini kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa, ngoja nikukumbushe....
Wakati majigambo haya ya kuua vyama mbadala hususani CHADEMA kabla ya 2010 na baadaye wakaja kubadilika na kuwa itakufa kabla ya 2015....
Kumbuka wakati huo CHADEMA ilikuwa ina wabunge wasiozidi 42 na wakati huohuo wakiongoza baadhi ya halmashauri kadhaa kama tatu ama tano hivi nchi nzima...
Hayawi hayawi uchaguzi mkuu 2015 hip ukafika.....
Unajua matokeo yake?
For the first time ever in its history, CHADEMA ikatoa upinzani mkali kupita kipimo cha CCM ktk kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani....
For the first time ever, CHADEMA pamoja na mfumo mbaya wa uhesabuji kura za urais chini ya NEC - CCM sambamba uchakachuji (wizi) ikapata kura za urais karibu 7,000,000 tofauti ya kura karibu 1.5m tu za mshindi wa CCM.....
For the first time ever, CHADEMA ikashinda majimbo ya ubunge mengi zaidi na kupata wabunge mara mbili kuliko wale ktk uchaguzi uliopita i. e 2010....!!
For the first time ever, CHADEMA sambamba na vyama washirika wenzake wa UKAWA ikatwaa na kuongoza halmashauri nyingi zaidi kuliko ktk uchaguzi uliopita wa 2010 likiwemo majiji matatu DSM, Mbeya na Arusha....!!
Ndiyo for the time ever CCM Zanzibar inashindwa mchana kweupe na CUF ktk sanduku la kura na kwa ubabe wa kijeshi inapindua matakeo na kuzua mgogoro wa kikatiba mpaka leo...!!
Kwa maelezo haya, ndiyo maana nimetangulia kukuuliza umetumia vigezo gani kuja na post dhaifu wewe "verified user" kabisa yenye conclusion ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia wa mambo?
Je, ni kwamba unataka kuanzisha kauli zile za miaka ile za akina Mwigulu Nchemba na akina Steven Wassira za kwamba watauteketeza upinzani kabla ya 2010 na baadaye wakageuka ikawa kabla ya 2015?
Je, ni kwa sbb baadhi ya wanaCCM wanaachana na chama chao na kujiunga na upinzani hususani CHADEMA?
Alaa, sasa hii yaweza kuwa sbb kweli ya kuiona CHADEMA kuwa inakosa mwelekeo? Kwani ni wanaChadema wangapi wangapi wanakwenda CCM bwana? Je, ndiyo tuseme kuwa CCM inakosa mwelekeo kwa sbb wanapokea wanachama toka CHADEMA??
Mimi, sikubaliani na wewe kwa sbb inaelekea hata hujui CHADEMA inaingiza wanachama wapya wangapi kila siku. Na likely huna ufahamu wa mikakati waliyo nayo hawa jamaa kukabiliana na CCM iliyokwisha kufa chini ya Magufuli....
Mimi ninakuhakikishia, 2020 itakupa majibu kuwa your perception kuhusu CHADEMA na upinzani kwa ujumla is wrong kwa matokeo ya uchaguzi huo....!!
Ushahidi mwingine ulio wazi kuwa CCM hii chini ya Magufuli ni mfu, ni jinsi tu wanavyoendesha mambo yao na nchi kwa ujumla....
Wanatumia nguvu kubwa kuliko akili. Wanajihami zaidi kwa kila kitu kuliko kuonesha jinsi wanavyotekeleza mipango na sera zao....
Huu ni ushahidi dhihiri kuwa, CCM imekabwa koo kuliko udhaniavyo. Angalia tu ujinga wanaoufanya dhidi ya Lazaro Nyalandu yaani utadhani huyu jamaa ni mwizi na fisadi kuliko hata John Pombe Magufuli mwenyewe....kitu ambacho ni kinyume chake...
Wanafanya yote haya wakiwa na akili na fikra kama zako, kwamba watanzania wa leo ni wajinga jinga tuuu sawa sawa na wale wa miaka ya 1995 enzi za NCCCR Mageuzi ya akina Agustino Lyatonga Mrema...!!