Ndani ya CHADEMA: CCM anaingia, CCM anatoka

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.

Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
 
Sikio la kufa ....Mbowe ndiye mtu anayepaswa kujitafakari binafsi na kuchukua maamuzi magumu ...tusisubiri ya NCCR mageuzi maana naona kabisa Chadema inaenda shimoni na hasa moto utaanzia uchaguzi wa 2020 ....bado mapema kujipanga upya .....
 
Hayo ni mawazo yako tu ndugu Petro E. Mselewa kila zama na kitabu chake na unalijua fika! Whatever utakavyoita kwa kutumia tumsamiati twako twa kisheria ila deep moyoni unafahamu vuguvugu la kisiasa nchini kwa sasa... ni wachache mna tena wenye mioyo mikuu wataendelea kuwa na misimamo ama udhaifu waliokuwa nao kwanza!
 
Hii dhana ya "sehemu salama ya kukimbilia na kujificha" sio sahihi. Salama vipi wakati wapo Nchini na tuna mahakama ya mafisadi?

Hao wanaotoka huko, CCM haina moral authority ya kudeal nao effectively maana wanafahamu hawa mabwana wanajua na wamefanya mambo mengi kwa pamoja. Mtu kama Nyalandu amefanya mengi maovu na uongozi wa juu kabisa na ataachwa tu apete. Hata JPM analitambua hilo.
 
Utawatafutia wanachama sehemu gani? Jamaa kazuia mikutano na hata kwenye mikutano ya kampeni nako unapangiwa cha kusema..
 
Tatzo hawa jamaa wanajifanya hawaoni...hawasikiii...wala kuhisi ya kuwa ukishakuwa Yanga wewe ni Yanga tu hata huamie Simba....
Tutegemee makundi tiifu kwa LOWASSA kuvujisha siri za CHADEMA pale tu WAFIA CHAMA watakapo PIGANA kuona ni LISSU 2020 na si Mr white hair...
CCM kuweza kuongoza nchi kwa miaka yote hiyo si jambo RAHISI...Hapa ndio mnatakiwa mtambue kuna majitu yana AKILI NDANI YA CCM......
 
Naamini,hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei,kama waanzilishi,walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu,waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa,kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivisasa,mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA. Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi,CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu,anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM,anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia,wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA,rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi,mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!

Naomba nikuulize swali moja tu mfano leo lisu na mnyika wakaamua kurudi ccm do you think ccm watawakataa?
 
Acha uongo mtu mzima! Hakuna mwanzilishi ye yote wa CHADEMA ambaye hakuwa mwanachama wa CCM!

CCM ilihodhi wafanyakazi wote, wanafunzi wote na wananchi wengi wakiwemo wafanyabiashara na wakulima. Hivyo ni wazi wanachama wengi wa vyama vya upinzani lazima watoke CCM!
 
Acha uongo mtu mzima! Hakuna mwanzilishi ye yote wa CHADEMA ambaye hakuwa mwanachama wa CCM!

CCM ilihodhi wafanyakazi wote, wanafunzi wote na wananchi wengi wakiwemo wafanyabiashara na wakulima. Hivyo ni wazi wanachama wengi wa vyama vya upinzani lazima watoke CCM!
Wapi nimesema waanzilishi hawakuwa CCM? Kwahiyo mnaendelea na mazoea?
 
Hii dhana ya "sehemu salama ya kukimbilia na kujificha" sio sahihi. Salama vipi wakati wapo Nchini na tuna mahakama ya mafisadi?

Hao wanaotoka huko, CCM haina moral authority ya kudeal nao effectively maana wanafahamu hawa mabwana wanajua na wamefanya mambo mengi kwa pamoja. Mtu kama Nyalandu amefanya mengi maovu na uongozi wa juu kabisa na ataachwa tu apete. Hata JPM analitambua hilo.
Napo sikitika ni kumuahalatishia mtu kwa kuwa alikuwa ccm. Yani mnayatumia madhaifu ya ccm na kuyaiga mkuu. Ilitakiwa huu ndio mda wa kuwakazia uzi mpaka mwisho huku chama kikiimalika na kujipambanua zaidi ili kiwe m-badala. Sasa tatizo ni palr ambapo chadema inakosea na yenyewe haihitaji mawazo m_badala. Sasa hapa kuna tofauti gani na ccm?? Na kuna maana gani ya kuwa chama m_badala?? Jamani tuoneeni huruma watz, CHADEMA tulikotegemea na penyewe mambo kama CCM??

CHADEMA inapaswa kuwa na mlengo wa tofauti na CCM. Sio ccm ikikosea chadema anajitetea mbona ccm wenyewe walifanya hivi?? Maana ya kuwa kimbilio la watu haitakuwepo aseee
 
Sikio la kufa ....Mbowe ndiye mtu anayepaswa kujitafakari binafsi na kuchukua maamuzi magumu ...tusisubiri ya NCCR mageuzi maana naona kabisa Chadema inaenda shimoni na hasa moto utaanzia uchaguzi wa 2020 ....bado mapema kujipanga upya .....

Kwamba mboe afukuze watu wote ambao walikuwa ccm before then chama kitabaki na watu gani? Hao watu watakuwa na impact gani ? Chama chochote duniani lazima kiwe na watu kutoka chama kikubwa
 
Back
Top Bottom