Ndani ya CHADEMA: CCM anaingia, CCM anatoka

Kwa maoni yangu nadhani ni vzr kuwa na POLITICAL PARTY INTEGRATION. Kusiwe na uhasimu uliopindukia kati ya chama kilicho madarakani na kile cha upinzani kwani mwisho wa siku inapelekea uhasimu huo kuwa ndio lengo kuu la uwepo wa vyama vya siasa badala ya maendeleo ya nchi. Tusichoke kujifunza toka kwa wenzetu ambao siasa zao zimeshakomaa, Taifa kwanza halafu chama baadaye. Ndio maani ni ngumu kujua Rais wa Marekani au Waziri mkuu wa Uingereza au Rais wa Ufaransa anatoka chama gani, cha upinzani au Tawala? To me, hz movement za wanasiasa toka chama hiki kwenda kile zitapelekea tufike mahali na kuanza kusahau itikadi zetu za vyama na hivyo kujikita zaidi ktk kujenga nchi tukiwa wamoja!
 
Hayo mawazo sio ya siasa labda mshabiki wa mpira ndo atabaki kwenye timu anayoshabia...chama mkusanyiko wa watu waliojifanya humo kwa maslahi yao ndo maana hhaviishi misukosuko na migongano. Vyama tawala vinafaida tu ya kulindwa na dola lkn sio kwamba ndo viko makini katika mifumo ya uendeshaji wake. Bila dola hakuna vyama vyenye mifumo ya ovyo kama vyama hivyo hasa vyama vilivyoanzishwa kwa lengo la kupigania uhuru wa bendara. Ndo maana vyama tawala vya kiafrika vikitoka tu nje ya dola vinavurugika kabisa kwa sababu hawajui kuendesha siasa nje ya dola
 
Chadema wanapaswa kuwafanyia assesment wanaotoka CCM na kukimbilia kwao kabla ya kuwapokea na kuwapa nafasi nyeti kwenye chama.Pengo la vijana mahiri kama Mnyika,Zitto,Shonza,Heche,Sugu linaonekana waziwazi ile Bavicha imekufa kabisa sasa wanasubiri kupokea wazee wanaohama CCM
Mkuu ni muda mrefu tangu,
Tangu Tanzania ilipojiondoa isivyo rasmi katika Democrasia na ramsi katika Transparency.
Pia utawala wa sheria unaonyesha kukosa makali nchini..
Wasiojulikana wanaonekana kutamba kama vile wako kibiti...
Hao vijana wakina mnyika and the like, ni Brand muhimu sana kwa CDM na nguvu ya upinzani kwa ujumla.

Nguli Mmoja mjenga hoja, na mwanasheria ndugu Tundu Athipas Lisu wamempumzisha na bado hatujui kama walishamsamehe kile wanachotaka hata kupelekea kumiminia Risasi nyingi vile..

Godbless Lema, Mbilinyi wanahofu na mustakabali wao hapa nchini...alishalisema hili Tundu Lisu kabla maswahibu hayajamkuta. Na Joseph Mbilinyi pia anahofu.

Unaweza kua mahiri lakini Hofu ya ubinadamu ikakufanya ufikiri tena na tena kabla ya kuamua kushindana na Chuma cha Reli.
Ukitumia mdomo lakini adui anatumia kila silaha kukunyong'onyeza.
 
Kwa kweli sielewi ni nini kimewakumba vijana hawa wa BAVICHA!!
Tatizo wewe unajiona unajua sana na kujifanya 'mchambuzi' wa siasa.Kwa hiyo wewe unataka ccm ichukue wanachama wa chadema lakini chadema isichukue wanachama wa ccm! CCM kuchukua madiwani wa chadema na kuwapa nafasi ya kugombea tena udiwani kupitia CCM wewe unaona sawa.
 
Swali la kizushi

Hivi chadema wangekataa kuwapokea akina Lowasa, Sumaye, masha na Nyalandu kuwa wana makandokando mengi je wangeongeza umaarufu au umaarufu ungepungua?
 
These Rogojins...they believe they would become strong by taking the leftovers....Hakuna...inapendeza kama asemavyo Dr. Shika
 
Tatizo wewe unajiona unajua sana na kujifanya 'mchambuzi' wa siasa.
Nilichonukuu kinahusiana na hicho ulichoandika? Sisi na niliyekuwa nimemnukuu tulikuwa tunazungumzia utofauti wa BAVICHA ile ya kina Heche na hii ya kina Patrobas. Sasa kuona sawa au si sawa kuhusu kupokea wanaotoka CCM ama CHADEMA Kumekujaje!!

Usiwe unajibu hoja kwa kutumia hisia zako utachanganya mambo!


ile Bavicha imekufa kabisa sasa
Kwa kweli sielewi ni nini kimewakumba vijana hawa wa BAVICHA!!
 
Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.

Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
Umeandika kama mpenzi kweli wa Chadema lkn kwa jicho la tatu unataka Chadema waanze kuwabagua watu eti tu kwa sababu walikuwa CCM.Siasa ni watu yeyote akiona inafaa kuhama chama na afanye hivyo cha msingi havunji sheria za nchi!Ndiyo maana kuna chama cha siasa kinatuhumiwa kuwanunua wanachama wa vyama vingine,ulishawahi kujiuliza kwanini?
Kwa upande wa pili Masha alivyoona vyuma vimekaza na alichokifuata CDM kukikosa na salama yake ni kurudi kundini ili makaburi yamhusuyo yasifukuliwe!
 
Mkuu ni muda mrefu tangu,
Tangu Tanzania ilipojiondoa isivyo rasmi katika Democrasia na ramsi katika Transparency.
Pia utawala wa sheria unaonyesha kukosa makali nchini..
Wasiojulikana wanaonekana kutamba kama vile wako kibiti...
Hao vijana wakina mnyika and the like, ni Brand muhimu sana kwa CDM na nguvu ya upinzani kwa ujumla.

Nguli Mmoja mjenga hoja, na mwanasheria ndugu Tundu Athipas Lisu wamempumzisha na bado hatujui kama walishamsamehe kile wanachotaka hata kupelekea kumiminia Risasi nyingi vile..

Godbless Lema, Mbilinyi wanahofu na mustakabali wao hapa nchini...alishalisema hili Tundu Lisu kabla maswahibu hayajamkuta. Na Joseph Mbilinyi pia anahofu.

Unaweza kua mahiri lakini Hofu ya ubinadamu ikakufanya ufikiri tena na tena kabla ya kuamua kushindana na Chuma cha Reli.
Ukitumia mdomo lakini adui anatumia kila silaha kukunyong'onyeza.
Bavicha ilishakufa hata kabla ya Magufuli kuingia madarakani,Ukweli Dr Slaa alijitahidi sana kufanya uenezi wa chama kuanzia level ya chini.Uchaguzi wa 2015 uliwafanya Chadema wakasahau ile mipango endelevu ya miaka mingi wakachagua mipango ya muda mfupi ambayo kiuhalisia ni nguvu kutekelezeka kwa mazingira ya Tanzania
 
Marsha Mtoto wa mjini maisha ya mapambano hayawezi, Nilijua tu iko siku atarudi katika maisha yake ya zamani. Marsha ni Kama Lema tu.
 
Subiri uambiwe unasubiri teuzi na matusi. All in all umeongea ukweli kama alivyosema Masha.
 
Bavicha ilishakufa hata kabla ya Magufuli kuingia madarakani,Ukweli Dr Slaa alijitahidi sana kufanya uenezi wa chama kuanzia level ya chini.Uchaguzi wa 2015 uliwafanya Chadema wakasahau ile mipango endelevu ya miaka mingi wakachagua mipango ya muda mfupi ambayo kiuhalisia ni nguvu kutekelezeka kwa mazingira ya Tanzania
Haki kweli kabisa....

ukimrudisha Dokta Slaa leo kwa Ufalme huu unaotawala. Asingefanya Lolote la maana.
Mark my words...heri tumwache auze Supermaket uko canada. Manake ya huko yanaweza mshinda anytime..tena Sijui kwanini watu wanamkumbuka quiter aliekimbia changamoto?!!.

Yule alikua dhahifu kuliko Lowasa. Ndio maana alishindwa Siasa.
Huwezi kua Imara kisha akaja mtu mgeni nyumbani kwako akakutoa. Kisha ukaendeleea kujiita kuwa wewe ni Imara.?!!its absurd!!.

Dk. Slaa, Ameshindwa kilakitu katika maisha yake:-
1. Upadre..Kanisa katoliki lipo palepale bila dokta slaa.

2. CCM:-/tena ndio imekua mbaya kuliko ya JK.
3. CDM tena imekua inaogopwa na chama Tawala kuliko Ya enzi zake ikiwa na wabunge wengi na rekodi kubwa kuliko zote katika matokeo ya Uraisi tangu vyama vingi vianzishwe... Kelele za kuondoka kwake hazikuzuia watanzania kuwaunga mkono wapinzani.


Nitasema Kweli Daima.
Fitina kwangu Mwiko..
Siitashangaa nikisikia Dokta slaa akikimba na kuacha supermarket kwa madai hakukua na haki katika bei za mauzo na wateja huko Canada ameshindwa kuelewana na meneja. Kwa umri ule anything can happen.

Alishindwa kuthibitisha kua Kanisa katoliki lilihongwa na shahidi yake akawa mshenga Gwajima. Gwajima alimkatalia na akapiga double manifestation. Na akamwambia kama yeye slaa ni Mwanaume, ajibu. Slaa alipoona hali mbaya akakimbia bila kutolea ufafanuzi maelezo ya Gwajima.

Juzi gwajima alipokamatwa na serikali kwa kutajwa kwenye sakata la madawa ya kulevya. Slaa akaamua kumtumia slamu za Pole Gwajima. Na kujikomba kua anamfahamu gwajima wanamuonea. Nashangaa hakuna chombo cha habari kilichoonyesha doubt maneno yake...
Jinsi ninvyomuelezea nazidi kuona haina maana kumwita dokta... Aitwe slaa tu. Ndio jina linalomfaa.
Anaogopa hata kumpa Pole tindu lisu..yule ni puppets. Nuff said..
 
Hayo ni mawazo yako tu ndugu Petro E. Mselewa kila zama na kitabu chake na unalijua fika! Whatever utakavyoita kwa kutumia tumsamiati twako twa kisheria ila deep moyoni unafahamu vuguvugu la kisiasa nchini kwa sasa... ni wachache mna tena wenye mioyo mikuu wataendelea kuwa na misimamo ama udhaifu waliokuwa nao kwanza!
Ni mjinga tu anayefikiri chadema hii ya sasa itakuja shika nchi, wameongeza flava tu ktk chaguzi kuisindikiza sisiemu.
 
Sikio la kufa ....Mbowe ndiye mtu anayepaswa kujitafakari binafsi na kuchukua maamuzi magumu ...tusisubiri ya NCCR mageuzi maana naona kabisa Chadema inaenda shimoni na hasa moto utaanzia uchaguzi wa 2020 ....bado mapema kujipanga upya .....
Kuna point ya msingi ya CHADEMA kutafakari namna ya kupata wanachama wapya.

Ila upiga ramli wako, ni kiwango cha kipekee! Ulipiga ramli kwamba baada ya CHADEMA kumpokea Lowassa na kushindwa, ndiyo ungekuwa mwisho wa chama! Punguza upiga ramli ewe mfuta viatu wa Slaa!
 
Ni mjinga tu anayefikiri chadema hii ya sasa itakuja shika nchi, wameongeza flava tu ktk chaguzi kuisindikiza sisiemu.
Of course kwa mfumo wa siasa na uchaguzi uliopo sasa, ni vigumu kwa chama tofauti na CCM kushika dola! Utashindanaje na chama dola kweli?

CCM kama ina ubavu, iache mazingira ya ushindani yawe fair na transparent! Halafu tuone kama unaweza kusema ulivyosema.
 
Kwamba CCM ndo inamiliki hisa zote za taifa? Ama wameshikilia akili za wananchi wote?..Pambaff!
Usiogope, nimesema ni wajinga tu wanaofikiri chadema hii itashika dola, wewe unaamini na kufikiri hivyo, kwa hiyo upo kwenye kundi la niliosema hapa.
Usitoke povu.
 
Back
Top Bottom