Ndani ya CHADEMA: CCM anaingia, CCM anatoka

Kufikia uwezo wa kushawishi kigogo wa CCM kuhamia Chadema ni mafanikio sana kwa Chadema na upinzani kwa ujumla..Haijalishi huyo kigogo atakuja kurejea ccm hapo badae.. Chadema ina umaarufu huo kwa sababu kuna watu wamepambana sana kwa kujitoa maisha yao. . Na hao watu si wa aina ya Masha
 
Katika ufuatiliaji wangu wa siasa za Tanzania nimegundua kuwa kuna sababu kubwa ya kusema wapinzani wanafeli a big time. Turudi nyuma tangu tangu kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 kumekuwa na wimbi kubwa la kuhama kwa baadhi ya watu maarufu kutoka chama kimoja kwenda kingine.
Imekuwa ni desturi kwa upinzani kukaribisha watu kutoka chama tawala na kusema kuwa ni haki yao kikatiba kuhama chama tawala na kutoa sababu kuwa chama tawala kimepoteza mwelekeo. Lakini katika kitu ambacho kimeonekana kuwa ni kituko cha mwaka ni pale ambapo mtu anahama kutoka upinzani kwenda CCM, watu hao wamekuwa wakibezwa kwa kusema kuwa njaa zinawasumbua.

Napata shaka sana juu ya upinzani huu! Mbali na hilo kunatuhuma nyingi sana zilizotolewa na upinzani kuhusu ufisadi na ufujaji wa mali za umma unaofanywa na baadhi ya viongozi lakini pindi watu hao wanapoanza kuchukuliwa hatua huamua kukimbilia upinzani ili kutaka huruma ya wananchi kuwa wanaonewa kwasababu wamekihama chama tawala.
kama fisadi Nyalandu
 
Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.

Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
Hii ni hofu tu uliyonayo.
 
SINA MASHAKA NA WANACCM WALIOPO CHADEMA

Na Thadei Ole Mushi.

Wazungu wana kamsemo kanasema easy come easy go wakiwa na maana ya kwamba ulichokipata kwa urahisi huondoka pia kwa urahisi. Msemo huu unatuongoza kutafakari uhamaji wa wanaccm kwenda ukawa na namna wanavyorudi.

Laurence Masha huyu alikuwa wa mwisho kuondoka katika mtiririko ule wa kuhama kwa kujitangaza.

Waliokuwa wamemtangulia walikuwa ni

Kingunge

Sumaye

Lowassa.

Kingunge atarudi baada ya Masha, Alitaka kukosoa utendaji kazi wa magufuli akasema ngoja ampe siku mia. Zilipotimia hakutaka kusema chochote. Kama ilivyo kwa Masha huyu mzee hajui chochote kuhusu chadema huyu naye hakufuata sera na falsafa ya chadema bali alifuata mtu (Lowassa).

Mzee huyu kalelewa na kakulia Tanu na Ccm huyu kurudi ni lazma alipokataa kumkosoa Magufuli alikuwa na maana yake.

Sumaye yeye naye si mwanachadema alichukia Kadi tu baada ya tetesi kuvuja kuwa atapewa ukatibu mkuu. Akachukua kadi haraka haraka ili akamilishe dili lake tukumbuke alikaa muda mrefu sana bila kujiunga chadema baada ya kujitoa ccm.

Kama ilivyo kwa Sumaye na kwa Lowasa hawa wana interest kubwa zaidi na Serikali kuliko Chadema. Hawa mpaka leo shughuli zao zote huratibiwa na serikali kupitia walinzi wanaowalinda.

Kazi aliyokwenda kuifanya Sumaye huko chadema ilikuwa ni kuwafundisha uongozi kama alivyodai alivyohamia kuwa anawafundisha namna ya kuongoza kama ukawa watachukua nchi. Ukawa hawakuchukua nchi hivyo hana haja ya kuendelea kutoa mafunzo ... kilichokuwa kinamsubirisha hapo ni ukatibu mkuu nao kaukosa yupo njiani huyu kurudi.

Lowassa yeye kwa maelezo niliyonayo atabaki huko huko ili agenda ya ufisadi isiwanufaishe wapinzani. Hawatathubutu kuzungumzia ufisadi kabisa. Uwepo wa Lowassa Ukawa unazuia mtu mwingine msafi kujijenga na kuja kugombea mbeleni.

Wanachama wote wa ukawa kwa sasa hawana haki ya kugombea uraisi isipokuwa Lowassa tu. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa demokrasia na haya ni makubaliano yasiyokuwa rasmi wala hayapo ndani ya katiba.

Ruhusa ya wanachama wengine kama kina Lisu, Mnyika, na wengineo kuja hata kujaribu kugombea uraisi itategemea ni Lini Lowassa ataondoka Chadema. Kwa hiyo kubaki kwake Chadema kuna manufaa makubwa zaidi kuliko kurudi.

FAIDA YA KUWAFUKUZA.

Chadema inapaswa kuchukua uamuzi mgumu kukwepa mtego huu. Uamuzi wenyewe ni kuwafukuza kundi hili wote ili waanze upya wakiwa wamebeba agenda za wananchi.

Elimu ya uraia kwa sasa kwa wananchi ni kubwa sana hivyo kama wakichukua ujasiri huo na kuwaomba radhi wananchi bado naona nafasi kubwa ya kujijenga tena upya na kuwa tishio hapa nchini.

Ni wakati sasa wa chadema kuamini vijana kama kina Lissu kugombea urais ili waanze kuzoea mikikimikiki ya uchaguzi ili baadaye waje wawe wagombea bora. Si sahihi kwa Lisu kuja kugombea akiwa mzee huku akisubiri Lowassa kijaribu bahati yake.

Chadema waamini vijana waliokijenga chama kuliko kuasubiri mtu anayetaka kujaribu bahati......

UHUSIANO ULIOPO KATI YA MASHA NA CHADEMA.

Kuna kitu vijana wa Chadema hawajui nimewasikia wakisema kuwa Masha hana impact hata akiondoka. Vijana hawa ni wale waliokuwa wanadeki barabara badala ya kujikita kuuza sera.

Masha huyu ni mwanausalama alifikia kipindi akaanza kuhudhuria vikao vyote vikubwa vya Chadema kwa maana hiyo kuna Siri nyingi sana anaondoka nazo.

Huyu si mtu wa Kubeza kama vijana hawa waliokuwa wakideki barabara wanavyofanya kama hamuamini siku za usoni mtasikia mambo makuu toka kwenye kinywa cha Masha.

Ole Mushi.
 
Kufikia uwezo wa kushawishi kigogo wa CCM kuhamia Chadema ni mafanikio sana kwa Chadema na upinzani kwa ujumla..Haijalishi huyo kigogo atakuja kurejea ccm hapo badae.. Chadema ina umaarufu huo kwa sababu kuna watu wamepambana sana kwa kujitoa maisha yao. . Na hao watu si wa aina ya Masha
Kupambana kupi?
Kupambania madaraka na kusema kuwa wanapigania demokrasia?
Kama madaraka ndani ya CHADEMA tu yamekuwa yanagawiwa kwa matakwa ya mwenyekiti, sembuse wakipewa nchi?
Eti serikali inaleta ukanda, je CHADEMA na kaskazini unazitenganishaje?
 
Hayo ni mawazo yako tu ndugu Petro E. Mselewa kila zama na kitabu chake na unalijua fika! Whatever utakavyoita kwa kutumia tumsamiati twako twa kisheria ila deep moyoni unafahamu vuguvugu la kisiasa nchini kwa sasa... ni wachache mna tena wenye mioyo mikuu wataendelea kuwa na misimamo ama udhaifu waliokuwa nao kwanza!
Mioyo migumu ya kuwapokea kina Nyalandu?
 
Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salama kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.

Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
Soft people si rahisi ku retain na sio faida ila ni hasara kwa CCM na wangekuwa hasara kwa chadema km wangebaki. Pengine ndio kitu usichokijua, Masha kajianika sana,ila kizuri ni kwamba. Chadema wamefaidika kuliko CCM ktk kuhama kwa masha. Masha km Lipumba, kafanya timingi mbaya. Masha kasaidia kumfanya Lissue rais wa TLS, kisha anarudi ccm kwenda kujenga taswira mbaya.Kwamba sasa hivi watu wa kanda fulani sio wa kuaminika tena, kwa zuri au kwa baya,sasa hivi wapo busy ktk ukarimu.

Masha Katoka kwa sababua ya kijinga kweli, sasa km issue ni CCM ,na upinzani ulipaswa kujikomboa kutoka ccm.Yeye kujiunga na ccm kunamkomboa yeye na mtz vipi?Yaani kujikomboa na mamba ni kujitupa ktk maji alipo?Jamaa kawa Lipumba.Na kwa taarifa yako.Itammaliza sana kisiasa.Na kujenga pattern mbaya.Bora angesema kuwa anaachana na siasa.
 
SINA MASHAKA NA WANACCM WALIOPO CHADEMA

Na Thadei Ole Mushi.

Wazungu wana kamsemo kanasema easy come easy go wakiwa na maana ya kwamba ulichokipata kwa urahisi huondoka pia kwa urahisi. Msemo huu unatuongoza kutafakari uhamaji wa wanaccm kwenda ukawa na namna wanavyorudi.

Laurence Masha huyu alikuwa wa mwisho kuondoka katika mtiririko ule wa kuhama kwa kujitangaza.

Waliokuwa wamemtangulia walikuwa ni

Kingunge

Sumaye

Lowassa.

Kingunge atarudi baada ya Masha, Alitaka kukosoa utendaji kazi wa magufuli akasema ngoja ampe siku mia. Zilipotimia hakutaka kusema chochote. Kama ilivyo kwa Masha huyu mzee hajui chochote kuhusu chadema huyu naye hakufuata sera na falsafa ya chadema bali alifuata mtu (Lowassa).

Mzee huyu kalelewa na kakulia Tanu na Ccm huyu kurudi ni lazma alipokataa kumkosoa Magufuli alikuwa na maana yake.

Sumaye yeye naye si mwanachadema alichukia Kadi tu baada ya tetesi kuvuja kuwa atapewa ukatibu mkuu. Akachukua kadi haraka haraka ili akamilishe dili lake tukumbuke alikaa muda mrefu sana bila kujiunga chadema baada ya kujitoa ccm.

Kama ilivyo kwa Sumaye na kwa Lowasa hawa wana interest kubwa zaidi na Serikali kuliko Chadema. Hawa mpaka leo shughuli zao zote huratibiwa na serikali kupitia walinzi wanaowalinda.

Kazi aliyokwenda kuifanya Sumaye huko chadema ilikuwa ni kuwafundisha uongozi kama alivyodai alivyohamia kuwa anawafundisha namna ya kuongoza kama ukawa watachukua nchi. Ukawa hawakuchukua nchi hivyo hana haja ya kuendelea kutoa mafunzo ... kilichokuwa kinamsubirisha hapo ni ukatibu mkuu nao kaukosa yupo njiani huyu kurudi.

Lowassa yeye kwa maelezo niliyonayo atabaki huko huko ili agenda ya ufisadi isiwanufaishe wapinzani. Hawatathubutu kuzungumzia ufisadi kabisa. Uwepo wa Lowassa Ukawa unazuia mtu mwingine msafi kujijenga na kuja kugombea mbeleni.

Wanachama wote wa ukawa kwa sasa hawana haki ya kugombea uraisi isipokuwa Lowassa tu. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa demokrasia na haya ni makubaliano yasiyokuwa rasmi wala hayapo ndani ya katiba.

Ruhusa ya wanachama wengine kama kina Lisu, Mnyika, na wengineo kuja hata kujaribu kugombea uraisi itategemea ni Lini Lowassa ataondoka Chadema. Kwa hiyo kubaki kwake Chadema kuna manufaa makubwa zaidi kuliko kurudi.

FAIDA YA KUWAFUKUZA.

Chadema inapaswa kuchukua uamuzi mgumu kukwepa mtego huu. Uamuzi wenyewe ni kuwafukuza kundi hili wote ili waanze upya wakiwa wamebeba agenda za wananchi.

Elimu ya uraia kwa sasa kwa wananchi ni kubwa sana hivyo kama wakichukua ujasiri huo na kuwaomba radhi wananchi bado naona nafasi kubwa ya kujijenga tena upya na kuwa tishio hapa nchini.

Ni wakati sasa wa chadema kuamini vijana kama kina Lissu kugombea urais ili waanze kuzoea mikikimikiki ya uchaguzi ili baadaye waje wawe wagombea bora. Si sahihi kwa Lisu kuja kugombea akiwa mzee huku akisubiri Lowassa kijaribu bahati yake.

Chadema waamini vijana waliokijenga chama kuliko kuasubiri mtu anayetaka kujaribu bahati......

UHUSIANO ULIOPO KATI YA MASHA NA CHADEMA.

Kuna kitu vijana wa Chadema hawajui nimewasikia wakisema kuwa Masha hana impact hata akiondoka. Vijana hawa ni wale waliokuwa wanadeki barabara badala ya kujikita kuuza sera.

Masha huyu ni mwanausalama alifikia kipindi akaanza kuhudhuria vikao vyote vikubwa vya Chadema kwa maana hiyo kuna Siri nyingi sana anaondoka nazo.

Huyu si mtu wa Kubeza kama vijana hawa waliokuwa wakideki barabara wanavyofanya kama hamuamini siku za usoni mtasikia mambo makuu toka kwenye kinywa cha Masha.

Ole Mushi.
Msha katoka km Lipumba tuu. Sababu ya kutoka ime ji cancel out baada ya kujiunga na adui ambaye anawatuhumu wapinzani kutokuwa na nia ya kumwondoa.Chadema ni smarter than that mkuu tuu. Km wanawaweza kinga advantage na kumwachia mtu bila hasara. masha kaondoka ili akavune malipo kinyumabni mapema.Ila keshavuruga TLS vibaya, km lipumba laivyokuja kufanikisha ujio wa Lowasa kiesha akenda jiliza km mwehu.
 
Hoja yako haina mashiko,kwani mzee Mtei alikuwa chama gani kabla ya kuingia ccm?
 
Mimi mwenyewe bado nafsi yangu inakataa kujiunga na CHADEMA baada ya kuachana na CCM. Moyo unakataa kabisa yani. Bado niko neutral.

#otaligamba#
 
Wapi nimesema waanzilishi hawakuwa CCM? Kwahiyo mnaendelea na mazoea?
Siasa sio uadui mkuu siasa ni watu mkuu siasa si kama ushabiki wa mpira na ndio maana kila mtu anaweza kuwa mwanachama wa chama chochote bila kuvunja sheria sasa ww ndugu yangu unatakakutuaminisha yakuwa ikiwa ww ni ccm huwezi kushurikiana na watu kutoka cdm tafsiri yako ni mbaya sana mnaligawa taifa kwakutumia siasa kesho mbowe anaweza kwenda ccm hakuna shida cdm itapata viongozi wengine tu
 
Naamini, hata waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakulenga kinachotokea sasa. Akina Mzee Edwin Mtei, kama waanzilishi walilenga kuifanya CHADEMA iwe chama imara na mbadala. Si sehemu ya kutambia watakavyo wanaCCM.

Kwa uelewa wangu, waanzilishi wa CHADEMA walipanga na kufanya mpango wa kuijenga kwa kutafuta wanachama na hata kuandaa viongozi wa baadaye nje ya CCM. Wanachama walipaswa kusakwa, kulelewa na kukomazwa humo. Ni katika mfumo wa walivyopatikana akina Zitto na Mnyika.

Hivi sasa, mambo yamekuwa tofauti. CHADEMA sasa imekuwa sehemu salamChadema kwa wahamiaji na wahamaji wa CCM. WanaCCM sasa wanahamia na kuhama kadiri watakavyo ndani ya CHADEMA.

Ingekuwa kwenye uga wa masuala ya kodi, CHADEMA ingekuwa ni tax haven. Sehemu salama na ya kukimbilia kujificha.

Anaingia Lazaro Nyalandu, anatoka Laurence Masha. Anaingia mwanaCCM, anatoka mwanaCCM. Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajifariji kwa kusema kuwa eti chama ni watu! Nawahakikishia, wanaCCM watahamishia hata makundi yao CHADEMA. Wataanza kupigana vikumbo kama wapo kule.

CHADEMA, rudini kwenye misingi yenu. Sakeni wanachama wapya bila kusubiri wahamiaji na wahamaji wa CCM. Mkiendelea hivi, mtachaguliwa viongozi na kupangiwa cha kufanya na wanaCCM. Hamtaepuka kuwa CCM B. Msifanye chama chenu tax haven!
Chadema ya Mbowe ni kama kokoro baasi
 
Siasa sio uadui mkuu siasa ni watu mkuu siasa si kama ushabiki wa mpira na ndio maana kila mtu anaweza kuwa mwanachama wa chama chochote bila kuvunja sheria sasa ww ndugu yangu unatakakutuaminisha yakuwa ikiwa ww ni ccm huwezi kushurikiana na watu kutoka cdm tafsiri yako ni mbaya sana mnaligawa taifa kwakutumia siasa kesho mbowe anaweza kwenda ccm hakuna shida cdm itapata viongozi wengine tu
Shabiki nguli wa timu hawezi akahamishia ushabiki wake klabu nyingine huyo atakuwa sio shabiki bali ni mbeba jezi.shabili hasa wa Simba hawezi kesho akawa shabiki Yanga,huyo atakuwa ni mchezaji na sio shabiki.Duniani kote shabiki hahami wanaohama ni wachezaji wanaofanya mpira ni ajira sawa na wanasiasa wanaofanya siasa ajira na si kuwa siasa ni kutumikia chama na wanachama wake
 
Back
Top Bottom