Kama nitakuwa nimemuelewa Dr Mkumbo, ujasiri huu wa Mseveni ungetakiwa pia uonekane katika kushughulikia matatizo makubwa na sugu ya nchini kwake kama vile RUSHWA na wizi wa RASILIMALI. Ushoga ni si jambo ZURI na si sehemu ya utamaduni wetu na kwa hivyo lazima upigwe vita, lakini itakuwa ni ajabu tukitumia nguvu kubwa katika kupambana na ushoga wakati matatizo mengine ambayo ukiyatazama ni makubwa kuliko hata ushoga tukizembea au kuyapuzia katika kuyapunguza na kuyamaliza.
Alichomaanisha Dr. Kitila, pamoja na kwamba Mseveni anachukizwa na ushoga, lakini anataka kuitumia vita ya ushoga kama mtaji wa kisiasa kwa kurejesha imani yake kwa waganda. Lengo lake hilo la kuhakikisha jamii ya kiganda inaishi bila ushoga lingeenda sanjari na kupambana na umaskini na umaskini wa kipato na pia serikali ingejitahidi kuhakikisha kipato chake na ulinzi wa fedha za umma unakuwa kwa kiwango kikubwa. Hivi kama tungejiweza kiuchumi MAREKANI ingesema yote hayo au ingetudindisha na misaada yake?
TUPAMBANE NA USHOGA LAKINI PIA TUIMARISHE UCHUMI WA NCHI ZETU.
Kwa maelezo hayo Dr. Kitila hakuna mahala alipotetea ushoga, Mseveni ameshindwa kutatua matatizo mengine sugu ya waganda na ya kwamba anatumia kete ya ushoga kuwapumbaza waganda, na katu kauli hii haimaanishi msemaji anautetea USHOGA, angesema MASHOGA wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa hapo kweli tungeweza kusema anautetea ushoga. Kumtaka rais wa Uganda na serikali za Afrika zitambue kuna matatizo makubwa kuliko hata ushoga huko si kutetea ushoga, kwani ni kweli yapo matatizo makubwa kuliko hata ushoga, kama vileHIV na UKIMWI, RUSHWA, vifo vya watoto chini ya miaka 5, malaria, ujangiri na umaskini uliokubuhu.
Serikali shupavu isiishie kupambana na ushoga tu, bali pia ioneshe nia ya dhati ya kupambana na matatizo mengine hayo ambayo kimsingi yanaathiri maisha ya taifa na kila mmoja wetu moja kwa moja kuliko hata ushoga.
ASANTE DR.KITILA NA POLE YA WALE WASIOKUELEWA.