akiojiwa na charles hilary wa bbc, amemponda mseveni kuwa ana mapungufu hivyo kataka apate umaarufu kwa kupinga ushoga. Mimi nimejiuliza maswali mengi, kwa kuwa mseven ni dhaifu kwenye utawala wa kidemokrasia, ni dikteta basi ata ushoga aukubali? Mimi binafsi nimemuona dr kitila hamnazo. Ata kama mseven ana mapungufu, je ili la ushoga kafanya vibaya? Nakumbuka humu jf, watu wengi tumekuwa tunamponda mh rais kwa mambo mengi, lakini alipomshauri kagame aelewane na wapinzani, watz wengi tulimsapoti na ata wanyarwanda walivoanza kumshambuli Rais, wengi tulikuwa nyuma ya rais wetu. Je kitila alitaka M7 aruhusu ushoga? Kwa ili ya ushoga dr kitila huko peke yako labda wale masalia wako.
Mbona sioni kuwa Dr kajibu vibaya? naona kuwa ametoa mawazo sahihi kulingana na swali aliloulizwa. Pia naona ufafanuzi wake kuwa ni sahihi kuwa na msimamo wa namna hiyo kwa msomi yeyote. Ni vizuri wakati mwingine kuwa katika ground ya neutral kuliko kuchukua upande wowote. Ukweli ni kuwa haki za wachache katika dunia ya leo zinapewa kipaumbele na Mataifa yaliyoendelea. Na hilo litagharimu serikali nyingi za afrika zinazosimamia msimamo kuwa hayo siyo maadili ya Kiafrika. Najiuliza maadili ya kiafrika ni yapi? ni rushwa, ni udicteta, ni ufisadi au ni nini?

Mtanzania kama Dr Kitila Kukosa msimamo dhidi ya ushoga ni jibu kuwa anaunga au ataunga mkono ushoga!
Kwa elimu yake ni lazima awe kwenye nafasi ya kutoa suluhisho au msimamo kuhusu ushoga.huu ni mjadala wa muda mrefu sitwgemei kwa mtu kama yeye kukosa jibu lenye msimamo na muelekeo.
Museveni alishapima madhara ya msimamo wake dhidi ya ushoga na ameamua kuupinga!angeukumbatia ushoga angepata umaarufu kama huu alioupata...angepewa misaada ya kuimarisha nchi na hali za wananchi na hatimaye angeshinda uchaguzi kwa kuboresha hali za wananchi...sasa yeye ameamua kutafuta ushindi bila kutegemea misaada..sioni tatizo bali namuona ni shujaa!
Kwa hili Kitila Mkumbo amechemka na amedhihirisha ni kwa nini chadema ilimtosa!

Kimsingi hakutakiwa kutoa msimamo wake. Na mtu msomi kama yeye naona amefanya sawa sana. Ukweli ni kuwa Museveni kachemka japo sentensi hiyo hutaipenda hata kidogo. Museveni alisema anasubiri taarifa za watafiti kuhusu jambo hilo. Lakini matokea ya utafiti wenyewe haukuchapishwa popote. Kama unao huo itanisaidia. Ukweli ni kuwa anatafuta umaarufu katika jambo lisilo na mashiko. Kuwepo au kutokuwepo kwa mashoga kumemsaidia maskini akapata sahani ya chakula walau kwa siku moja? Kuwepo au kutokuwepo kumesaidia maskini kuachana na umaskini wao? Nadhani agenda hiyo ni haina msaada wa maisha ya walio wengi kwa nchi yake.
utake usitake ushoga ulikuwepo! Upo! Na Utakuwepo! Hata tuweke sheria ima tusiweke! Alichofanya mseve ni kutafuta umaarufu na sifa zisizo na faida kwake wala wananchi wa Uganda! Kwani angefunika kombe yapite kungekuwa faida zaidi!
lakini mkuu si unajua kua mawasiliano yalikatika wakati bado hajatoa hoja zote?kwanini unapata conclusion amekubali ushoga?mimi na conclude hajakubali ushoga kwakua alikua bado anazungumzia kitendo cha m7 kusaini kibabe kama hahitaji misaada yao.mimi namlaumu sana m7 maana ameshindwa kusoma alama za nyakati,hizi ni nyakati za mwisho mkuu,uliona kikwete alivyojibu CNN juu ya ushoga?kikwete mjanja anajua alama za nyakati,sheria za kukataza ushoga tunazo hata sisi TZ mkuu lakini lazma uende na gemu ili uokoe wengi na bado usikubali ushoga.SIO UNALETA UBABE WAKATI HUNA LOLOTE,UNATEGEMEA HELA HIZOHIZO ZA HAO WAZUNGU.m7 anaangamia kwa kukosa maarifa.
Kiukweli pamoja na binafsi kuchukia ushoga lakini kiukweli kwa umasikini huu wa nchi zetu hatuwezi kupambana sasa hivi otherwise umejipanga kwelikweli.
Museveni angepambana na ushoga kimya kimya kupitia vyombo vya usalama bila kuhitaji sheria rasmi.
Ubabe katika lindi la umasikini ni kujidanganya tusikatae ukweli.Ushoga ufyekwe kwa mbinu nyingine ili isipeleke nchi ilipo Zimbabwe.
Tatizo la wabongo hatujui kusoma between the lines. Kitila hakutetea ushoga lakini ameonesha wasiwasi wa ubavu wa sisi waafrika kutetea misimamo yetu ilhali tunategemea misaada. Mizungu inakuja inapoara mali zetu, viongozi wanakwapua mali za umma leo tuna nusu karne na zaidi bado tunapanda ndege kutembeza bakuli. Tunawezaje kukataa masharti yao ilhali bado tuko tegemezi kiuchumi na kiteknologia? THINK OUTSIDE THE BOX

wote tumethink outside the box...
ila kufikiri na kuchambua mawazo ya mtu kuna tofautiana .. na uchambuzi wangu si lazima uwe sawa na wakwako..
kaongea utata ..ambapo kunampa mtu fikra ya kufikiri vitu vingi ..
Dr.. alikosea kuwa neutral .. na kutoonyesha msimamo wake .. hivi mtu akisema aliutetea ushoga hata kua amekosea .. pia ni uchambuzi wake ... kwan Dr..hakuonyesha wp yupi ..
na jambo kama hilo nadhni ilimpasa kua open bila kuleta utata
Tena Swali la Charles lilikuwa wazi kabisa.....
".... unaonaje issue juu ya Uganda na misaada iliyozuiwa na world bank baada yakupitishia sheria kali ya kuzuia ushoga ..?"
Mkumbo anajibu, pamoja na mambo mengine kuwa
..."Viongozi wa kiafrika wanapenda kujivika ujasiri bandia katika mambo yasiyo na tija. Katika bara la Afrika kuna matatizo mengi na makubwa zaidi kuliko ushoga. Lakini wanatumia kadi ya ushoga kwa sababu ni swala gumu katika bara la Afrika ili kujipatia umaarufu hewa. Ushoga (UOVU) haliwezi kuwa tatizo kubwa kuliko rushwa na wizi wa raslimali unaoendelea bara la Afrika."
'Uovu', wizi wa rasilimali, rushwa, utumiaji na ufanyaji wa biashara ya madawa ya kulevya...ni matatizo makubwa sana kwa Afrika. Ni lazima tuyashughulikie kwa pamoja bila kupuuza hata moja ....na ukiona mtu anapuuza tatizo la UOVU kuwa si tatizo sana Ujue huyo anaungana na watoa misaada yenye masharti "ovu". Kwa maneno mengine naye hakitakii mema kizazi cha sasa na kvijavyo vya Waafrika. Huyu naye tumuepuke. Hatufai asilani...!
Tanzania tunahitaji mfumo mpya wa elimu utakaozalisha watu ambao wanaweza kufanya tafakuri makini na si watu wa kujibu hoja kwa jazba kama inavyotokea katika maoni yanayoibuliwa ndani ya mitandao ya jamii.
[[ By Kitila Mkumbo Tusipotoshe. Katika mazungumzo yangu sikutetea wala kupinga ushoga kwa sababu hiyo haikuwa mada. Nilichosema:
i) Misaada kutoka nchi za magharibi huambatana na masharti. Masharti mengi yanalenga katika kuchochea utawala bora hasa ukilenga kukuza demokrasia ya kimagharibi na kulinda haki za binadamu. Moja ya haki ambazo zinalindwa sana na nchi za kimagharibi ni haki za wapenzi wa jinsi moja.
Kwa hiyo ilitarajiwa kwamba nchi hizo zingeikatia misaada nchi ya Uganda pale ambapo Rais Museveni angesaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsi moja. Nikasisitiza hakuna njia ya kukwepa masharti haya kama nchi za kiafrika zitaendelea kutegemea misaada kutoka magharibi. Hatuwezi tukala keki na tukawa nayo at the same time.
ii) Viongozi wa kiafrika wanapenda kujivika ujasiri bandia katika mambo yasiyo na tija. Katika bara la Afrika kuna matatizo mengi na makubwa zaidi kuliko ushoga. Lakini wanatumia kadi ya ushoga kwa sababu ni swala gumu katika bara la Afrika ili kujipatia umaarufu hewa. Ushoga haliwezi kuwa tatizo kubwa kuliko rushwa na wizi wa raslimali unaoendelea bara la Afrika.
Rais Museveni ana matatizo makubwa ya kiutawala na hali yake kisiasa si njema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2016 na anatumia hili la ushoga ili kujikweza na kujiweka sawa katika kuwasaulisha waganda matatizo ya kisiasa na kiuchumi yaliyosababishwa na utawala wake. Anatumia pia kadi ya ushoga ili aendelee kugombea kiti cha urais wakati alipaswa kuondoka juzi.
Bahati mbaya mawasiliano yalikatika na nikaishia hapo. ]]
Ni wazi kuwa Dr Kitila umetetea ushoga tena bila kupindisha maneno.
Sijajua unachokanusha ni nini?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.