Nchi ya Kongo kuna vita, wanawezaje kutumia umeme bure bila kulipia?

Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,298
2,000
Mwaka jana nilibahatika kwenda nchini Kongo na nikaweza kujionea mengi sana ambayo hapa nchini kwetu Tanzania hakuna na mojawapo la jambo hilo ni suala la umeme.

Kule Kongo karibia nyumba zote nilizofikia hakuna mita za umeme kama nchini kwetu. Nikapata shauku ya kutaka kujua kwanini nyumba zina umeme lakini hazina mita ikabidi nimuulize mkongo man mmoja ndipo aliponambia huduma ya umeme kule Kongo ni bure ndio maana wanatumia majiko ya umeme, heater nk.

Sasa nikaanza kujiuliza serikali yao wanawezaje kufanya haya yote wakati nchi yao ina vita muda wote na kwanini kwetu kuna amani lakini umeme tunatumia wa kulipia. Je, hatuwezi fanya kama Kongo ?
 
leiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
621
1,000
Waliweka sawa mfumo wao wa kujali raia. Raisi wao si dikteta wakujali maslahi ya watu wa kanda fulani tu. Wanalinda mazingira kwa vitendo sio kampeni hewa kama kila mwanafunzi na mti wake..........
 
bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,176
2,000
Sisi tunaaminishwa kwamba tuna umoja wa kitaifa wakati siyo kabisa

Sisi tunaaminishwa kwamba tuna amani wakati siyo kabisa

Sisi tunaaminishwa ndo tuna maisha ya mfano wakati siyo kabisa

KINACHOTUGHARIMU NI KUTOJUA WENZETU WANAISHI VIPI=Exposure to foreign countries na utumwa fulani wa kiaina unaoendelezwa na mataifa ya magharibi kwa vile elimu yetu ni ndogo, mbaya na haitusaidii kufaidika na rasilimalli zetu zilizo nyingi.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,870
2,000
Mwaka jana nilibahatika kwenda nchini Kongo na nikaweza kujionea mengi sana ambayo hapa nchini kwetu Tanzania hakuna na mojawapo la jambo hilo ni suala la umeme.

Kule Kongo karibia nyumba zote nilizofikia hakuna mita za umeme kama nchini kwetu. Nikapata shauku ya kutaka kujua kwanini nyumba zina umeme lakini hazina mita ikabidi nimuulize mkongo man mmoja ndipo aliponambia huduma ya umeme kule Kongo ni bure ndio maana wanatumia majiko ya umeme, heater nk.

Sasa nikaanza kujiuliza serikali yao wanawezaje kufanya haya yote wakati nchi yao ina vita muda wote na kwanini kwetu kuna amani lakini umeme tunatumia wa kulipia. Je, hatuwezi fanya kama Kongo ?
Jibu ni ufisadi ndiyo kiama chetu
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,177
2,000
Mkuu kama ni kweli nimeipenda hii.Huku service line,ile luku,nguzo,wire ule na makorokoro yote unanunua mwananchi
 
Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,585
2,000
Mikataba mibovu ndiyo yaliyo sababisha yote haya...

Nchi ya kongo utajiri wake wa asili unaweza kuilisha bara lote la Africa.. Sema ndiyo hivyo akili zimeshikiwa na wazungu.. Vita haviishi waafrica wanapigana wao kwa wao yaani ni shida tupu.... Kama siyo vita lile taifa lingekuwa lipo mbali sana.....
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,287
2,000
Kwhayo Hapa Kwetu Umeme Bure Haiwezekani?
FB_IMG_1497948497085.jpg

FB_IMG_1497947069869.jpg
 
Gauss93

Member
Mar 28, 2017
9
45
Je, hatuwezi fanya kama Kongo ?

The Inga Dam, alone on the Congo River, has the potential capacity to generate 40,000 to 45,000 MW of electric power, sufficient to supply the electricity needs of the whole Southern Africa region. Ongoing uncertainties in the political arena, and a resulting lack of interest from investors has meant that the Inga dam's potential has been limited.

In 2001, the dam was estimated to have an installed generating capacity of 2,473 MW. It is estimated that the dam is capable of producing no more than 650–750 MW, because two-thirds of the facility's turbines do not work. There are plans to raise the Inga power station to 44,000 MW capacity by 2010. The African Development bank has agreed to supply $8 million towards it. The government has also agreed to strength the Inga-kolwezi and Inga-South Africa interconnections and to construct a 2nd power line to supply power to Kinshasa.

If harvested to its full potential, the hydroelectricity could provide power for the whole of Africa.
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,966

What about minerals.... !??
 
germanium

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
688
1,000
DRC usiilinganishe na sisi hiyo nchi kwenye natural resources hakunaga zaidi yao duniani na kwa dondoo chache tu ni kwamba drc wanabwawa lao moja kwenye mto congo linaitwa inga dam linauwezo kwa kuhudumia southern africa region yote bila shida na kwa nyanzo vyake vyote vya umeme wa maji(hydropower plants) wakiamua vifanye kazi vinatosha kuhudumia umeme africa nzima

sasa hapo maana yake ni kwamba gharama ya umeme wa maji ni za chini kabisa ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme na sisi vyanzo vyetu tungeamua vyote viwe ni vya umeme wa maji kwa ruzuku wanayopewa tanesco ingetosha raia kupata umeme bure au kwa gharama ya chini kabisa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom