Safari yangu ya Kongo na kula nyama ya Nyau

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,128
5,236
Kama kawaida...

Katika pita pita za kutafuta mkono upande juu ya mdomo...nimewahi zunguka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Siku moja tumeondoka bongo tukaelekea Kongo maeneo ya kalemii na jamaa YANGU kusaka life...ebwana ilikuwa ni hatari sana!!!aisee tuliteseka sana.

Tuliingia Kongo lengo kwenda kutafuta dhahabu kwenye machimbo ya misisi. Kwa watembezi watakuwa wanapajua,tulitumia usafiri wa boti kupitia kibirizi, kigoma....mpaka kalemii tukifika Kule ndiyo tuangalie mchakato wa kuelekea misisi.

Ilikuwa mwaka 1996..vita imetawala Kongo nzima hakuna pa kupita...lakini tulikaza moyo Mimi na jamaa YANGU "J" .MZEE J alikuwa MTU wa kupenda kula ganja na kupiga chabo mademu/wanawake...sasa mule ndani ya boti tulilopanda kulikuwepo mama wa kikongo akawa amekaa vibaya...J akawa anapiga chabo alafu anacheka sana...dah! Boti zima hadi shofere.. wote tukawa tunamshangaa J,kwa nini anacheka ....yeye akawa anaendelea.....nikagundua huu itakuwa ndiyo ule mchezo wake..nilipomsogelea

akanionesha vile yule 'mamaa kiloo' kiswahili cha kongo..alivyoacha mambo hadharani...niligeuza shingo fasta..baada ya kuona kidogo sana!! ..Mali ya bakubwa,fasta...nikamlaani shetani nikabadilisha makazi Ila sikumwambia MTU ,safari ikaendelea japo mawimbi yalikuwa makubwa hadi maji yanaingia ndani ya boti, pia ilikuwa imejaza sana magunia ya chumvi.

Sasa safari yetu ikaendelea japo roho zilikuwa mkononi na Yale mawimbi na dhoruba 'J' yeye aliendelea kupiga chabo mpaka lilpopiga wimbi Kubwa sana ,maji yakaingia kwanye boti ikapiga na radi
💥💨 Kali sana kama Bomu💣...aisee boti zima tulikumbatiana kwa mshituko "J" akaacha kabisa kupiga chabo...kidogo mambo yakawa safi kabisa namimi nikashukuru.

Sàfari yetu ilikuwa na misukosuko mingi sana tulipofika mbele ...kidogo tukaona minyororo inashuka ndani ya maji ikiwa na moto kama wa chuma kilichowekwa kwenye moto mkali kikawa chekundu,Mara tukaona joka kuu linapandishwa kama umeme kwenda mawinguni tukapoteza fahamu kuzinduka tunaiona kalemii hiyo hapo mbele ya mboni zetu,kisha.. J akawa anamuliiza yule mama kuhusu njia za kupita kwa wasiyo na passpoti na hela ya visa, iilikuwa visa ni dola 50..na sisi tulikuwa na 30 tuliyoichange pale kibirizi kabla ya kuondoka kwa ajili ya matumizi,yule mama aliyepigwa shoo ya chabo akasema ningumu kutoboa bila hela,askari wa Congo wanapenda hela..tulipofika bandarini pale tukaamua kujitosa ndani ya maji tukaogelea mpaka nchi kavu....tukaibukia kijiji kimoja cha jirani na pale forodha ya kalemii,tukajifanya tumetoka kivu tumeenda kutafuta maisha.

Asubuhi tunaamka kwenye nyumba ya MZEE jampiere aliyetupokea....tunasikia habari kuna mama kajifungua watoto wawili mapacha wakike na wakiume aisee Kongo ni shida sana MTU asikwambie wale watoto..walikuwa wa ajabu sana!!!!..wakiume alizaliwa na ndevu nyingi tu, yaani kama mzuzu na nywele za makwapani !!! Wakike naye ndiyo Yale Yale kazaliwa na matiti makubwa, yaani ni shida kama anatenda ya kunyonyesha walevi!!!! ikabidi tukaangalie maajabu Mimi na jamaa YANGU J ,kufika njiani kuna mama tulikutana nae anaenda kuoga kabeba ndoo ya maji, bafu lilikuwa kichochoroni,dah si jamaa YANGU J akamuona ikabidi aahirishe kwenda kwenye maajabu, abaki anapiga chabo kama kawaida yake..MZEE,Mimi nikaenda kucheki maajabu ile watu wamekusnyika kuwaona hao watoto...Mara paap waasi wa maimai hawa hapa kijijini,wanapiga bunduki kama wendawazimu....Rambo akasome.!!!... aisee tulisambaana pale kila mmoja akakimbia kivyake tukapoteana na mshikaji wangu J.

Hatukuonana tena na J ...mpaka leo,sasa baada ya ule mtafaruku wa maimai...nikakimbia nisipopajua nikajikuta nimekutana na familia moja wanakimbia vita nikaunga nao mambo ya kwenda misisi yakawa yameishia hapo,akili inawaza kurudi Tanzania sina hamu tena na dhahabu...tukapanda mtumbwi kuelekea eneo LA karamba ili tufike Tanzania...sasa ile familia walikuwa wanaongea lingala na kiswahili kibovu....wakanipa ugali na kipande cha samaki mkavu nikala kupoza njaa ya YANGU ya tangu jana Ila sikushiba,tukafika eneo LA rasi ya karamba....tukaegesha mtumbwi wetu nchi kavu kwenye ufukwe uliyotulia.

Nikawaomba nikaoge pale ufukweni nikavua mavazi YANGU, nikajitupa ndani ya maji...nikatoka nikapaka sabuni nikajitupa tena ile nageuka nyuma Mara naona joka kubwa sana jeusi kama mkaa linanifuata...nilipiga kelele za kufa MTU....nikakimbia kule walipokuwa wale wakongo...zile kelele zilifika mpaka nyumba za jirani ya ile fukwe.

Watu wakatoka nje kuniona natoka ndani ya maji wakaanza kupiga kelele na kulaani....weye utatuua bure hapo ni marufuku kuoga....MZEE mmoja alisikika akiniambia kwa ukali...kumbe pale kuna mashetani,miiko yao hutakiwi kuoga au kufua,na shughuli zozote za usafi,Bali uchote maji ukafanyie pembeni siyo ndani ya maji,na joka ndiyo shetani lenyewe....ebwana sikuamini..kama nimepona.
Wale wenzangu wakawaambia sisi ni wageni hatujui chochote tunakimbia vita..tunaenda Tanzania kujinusuru....MZEE akaelewa akawaamrisha watu wake wawe wapole warudishe silaha zao walizokuja Nazo,wakitaka kunishambulia kwa kutaka kuwaletea maafa maana ningeliwa kama mboga,na mvua za maafa ya kuangamiza zingenyesha pale..kumbe sijui chochote.

Mambo yakawa yamepoa hivyo.....yule MZEE aliyenipa onyo kwa kuoga akatupokea akatupeleka kwake....akatuandalia chakula,ilikuwa ugali na nyama....mkewe na wanae wakike wawili walitukuta pale nyumbani walikuwa wameenda shamba....Mimi na wenzangu wale wakongo tukaanza kula ugali wetu mkubwa nyau haruki....nyama ilikuwa tamu sana,sijui niseme nini...tukamaliza kula nikajipumzisha kidogo kwenye mkeka pale pale tulipolia nikapitiwa na usingizi....nikaota na kula nyama ya nyau aliyenona na ugali....dah nilijuta sana katika ile ndoto...ile kushtuka baada ya kupiga makelele ndotoni...nikaamka nizunguke zunguke kupunguza uchovu aisee nilikutana na ngozi ya nyau mweusi sana, na kichwa chake kikubwa kama JIWE ....zile zinazokulaga kuku,nilisikitika ,kutapika nikashindwa nikajiuliza nilipize kisasi...gani kwa huyu MZEE japo katusaidia sikupata ufahamu kama nyau ni mboga huko kwa wazairwaa!!!....nikapata jibu bora kupiga chabo mkewe akienda kuoga!!!...
Basi nitakuwa nimelipiza kisasi bila chenchi ,na kumuenzi mshikaji wangu J.

Ila sikufanya nilivyokusudia nikaona nibora kumtorosha binti YAKE wa PILI aliyeitwa mimii...ili nije naye Tz iwe kama fidia....Tulikaa pale kijijini kwa siku mbili kisha tukaondoka na mtumbwi wetu na wale wakongo waliokuwa wanakimbia vita,yule binti wa yule MZEE nilimpiga saundi kali....akanielewa siunajua tena!!!!! mtanzania....anavyoshobokewa,kwa kifupi nilifanikiwa kumtorosha na kumleta Tanzania na kuachana na wazo potofu la kumpiga chabo mama yake....tulifunga ndoa na Mimii,mke wangu mkongo.... tukafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume....Ila tuliachana baada ya yeye kutaka twende kambini nyarugusu ili tutafute nafasi za kwenda ulaya/America....Mimi nilikataa,nikiamini ukikomaa hapa hapa bongo kwa nyerere, utatoka tu japo utachelewa!!!!....mwenzangu aliondoka 2006,na mwangu wakaelekea Canada kama wakimbizi....mpaka sasa sijawaona zaidi ya mawasiliano....
WhatsApp basi,huwa anitupi hunitumia dola 100 kila mwezi,japo aliolewa na zee lilochoka LA kizungu na....kushindwa kunitumia nauli niende tukale DuNIA.
 
Kama kawaida...

Katika pita pita za kutafuta mkono upande juu ya mdomo...nimewahi zunguka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Siku moja tumeondoka bongo tukaelekea Kongo maeneo ya kalemii na jamaa YANGU kusaka life...ebwana ilikuwa ni hatari sana!!!aisee tuliteseka sana.

Tuliingia Kongo lengo kwenda kutafuta dhahabu kwenye machimbo ya misisi. Kwa watembezi watakuwa wanapajua,tulitumia usafiri wa boti kupitia kibirizi, kigoma....mpaka kalemii tukifika Kule ndiyo tuangalie mchakato wa kuelekea misisi.

Ilikuwa mwaka 1996..vita imetawala Kongo nzima hakuna pa kupita...lakini tulikaza moyo Mimi na jamaa YANGU "J" .MZEE J alikuwa MTU wa kupenda kula ganja na kupiga chabo mademu/wanawake...sasa mule ndani ya boti tulilopanda kulikuwepo mama wa kikongo akawa amekaa vibaya...J akawa anapiga chabo alafu anacheka sana...dah! Boti zima hadi shofere.. wote tukawa tunamshangaa J,kwa nini anacheka ....yeye akawa anaendelea.....nikagundua huu itakuwa ndiyo ule mchezo wake..nilipomsogelea

akanionesha vile yule 'mamaa kiloo' kiswahili cha kongo..alivyoacha mambo hadharani...niligeuza shingo fasta..baada ya kuona kidogo sana!! ..Mali ya bakubwa,fasta...nikamlaani shetani nikabadilisha makazi Ila sikumwambia MTU ,safari ikaendelea japo mawimbi yalikuwa makubwa hadi maji yanaingia ndani ya boti, pia ilikuwa imejaza sana magunia ya chumvi.

Sasa safari yetu ikaendelea japo roho zilikuwa mkononi na Yale mawimbi na dhoruba 'J' yeye aliendelea kupiga chabo mpaka lilpopiga wimbi Kubwa sana ,maji yakaingia kwanye boti ikapiga na radi
Kali sana kama Bomu...aisee boti zima tulikumbatiana kwa mshituko "J" akaacha kabisa kupiga chabo...kidogo mambo yakawa safi kabisa namimi nikashukuru.

Sàfari yetu ilikuwa na misukosuko mingi sana tulipofika mbele ...kidogo tukaona minyororo inashuka ndani ya maji ikiwa na moto kama wa chuma kilichowekwa kwenye moto mkali kikawa chekundu,Mara tukaona joka kuu linapandishwa kama umeme kwenda mawinguni tukapoteza fahamu kuzinduka tunaiona kalemii hiyo hapo mbele ya mboni zetu,kisha.. J akawa anamuliiza yule mama kuhusu njia za kupita kwa wasiyo na passpoti na hela ya visa, iilikuwa visa ni dola 50..na sisi tulikuwa na 30 tuliyoichange pale kibirizi kabla ya kuondoka kwa ajili ya matumizi,yule mama aliyepigwa shoo ya chabo akasema ningumu kutoboa bila hela,askari wa Congo wanapenda hela..tulipofika bandarini pale tukaamua kujitosa ndani ya maji tukaogelea mpaka nchi kavu....tukaibukia kijiji kimoja cha jirani na pale forodha ya kalemii,tukajifanya tumetoka kivu tumeenda kutafuta maisha.

Asubuhi tunaamka kwenye nyumba ya MZEE jampiere aliyetupokea....tunasikia habari kuna mama kajifungua watoto wawili mapacha wakike na wakiume aisee Kongo ni shida sana MTU asikwambie wale watoto..walikuwa wa ajabu sana!!!!..wakiume alizaliwa na ndevu nyingi tu, yaani kama mzuzu na nywele za makwapani !!! Wakike naye ndiyo Yale Yale kazaliwa na matiti makubwa, yaani ni shida kama anatenda ya kunyonyesha walevi!!!! ikabidi tukaangalie maajabu Mimi na jamaa YANGU J ,kufika njiani kuna mama tulikutana nae anaenda kuoga kabeba ndoo ya maji, bafu lilikuwa kichochoroni,dah si jamaa YANGU J akamuona ikabidi aahirishe kwenda kwenye maajabu, abaki anapiga chabo kama kawaida yake..MZEE,Mimi nikaenda kucheki maajabu ile watu wamekusnyika kuwaona hao watoto...Mara paap waasi wa maimai hawa hapa kijijini,wanapiga bunduki kama wendawazimu....Rambo akasome.!!!... aisee tulisambaana pale kila mmoja akakimbia kivyake tukapoteana na mshikaji wangu J.

Hatukuonana tena na J ...mpaka leo,sasa baada ya ule mtafaruku wa maimai...nikakimbia nisipopajua nikajikuta nimekutana na familia moja wanakimbia vita nikaunga nao mambo ya kwenda misisi yakawa yameishia hapo,akili inawaza kurudi Tanzania sina hamu tena na dhahabu...tukapanda mtumbwi kuelekea eneo LA karamba ili tufike Tanzania...sasa ile familia walikuwa wanaongea lingala na kiswahili kibovu....wakanipa ugali na kipande cha samaki mkavu nikala kupoza njaa ya YANGU ya tangu jana Ila sikushiba,tukafika eneo LA rasi ya karamba....tukaegesha mtumbwi wetu nchi kavu kwenye ufukwe uliyotulia.

Nikawaomba nikaoge pale ufukweni nikavua mavazi YANGU, nikajitupa ndani ya maji...nikatoka nikapaka sabuni nikajitupa tena ile nageuka nyuma Mara naona joka kubwa sana jeusi kama mkaa linanifuata...nilipiga kelele za kufa MTU....nikakimbia kule walipokuwa wale wakongo...zile kelele zilifika mpaka nyumba za jirani ya ile fukwe.

Watu wakatoka nje kuniona natoka ndani ya maji wakaanza kupiga kelele na kulaani....weye utatuua bure hapo ni marufuku kuoga....MZEE mmoja alisikika akiniambia kwa ukali...kumbe pale kuna mashetani,miiko yao hutakiwi kuoga au kufua,na shughuli zozote za usafi,Bali uchote maji ukafanyie pembeni siyo ndani ya maji,na joka ndiyo shetani lenyewe....ebwana sikuamini..kama nimepona.
Wale wenzangu wakawaambia sisi ni wageni hatujui chochote tunakimbia vita..tunaenda Tanzania kujinusuru....MZEE akaelewa akawaamrisha watu wake wawe wapole warudishe silaha zao walizokuja Nazo,wakitaka kunishambulia kwa kutaka kuwaletea maafa maana ningeliwa kama mboga,na mvua za maafa ya kuangamiza zingenyesha pale..kumbe sijui chochote.

Mambo yakawa yamepoa hivyo.....yule MZEE aliyenipa onyo kwa kuoga akatupokea akatupeleka kwake....akatuandalia chakula,ilikuwa ugali na nyama....mkewe na wanae wakike wawili walitukuta pale nyumbani walikuwa wameenda shamba....Mimi na wenzangu wale wakongo tukaanza kula ugali wetu mkubwa nyau haruki....nyama ilikuwa tamu sana,sijui niseme nini...tukamaliza kula nikajipumzisha kidogo kwenye mkeka pale pale tulipolia nikapitiwa na usingizi....nikaota na kula nyama ya nyau aliyenona na ugali....dah nilijuta sana katika ile ndoto...ile kushtuka baada ya kupiga makelele ndotoni...nikaamka nizunguke zunguke kupunguza uchovu aisee nilikutana na ngozi ya nyau mweusi sana, na kichwa chake kikubwa kama JIWE ....zile zinazokulaga kuku,nilisikitika ,kutapika nikashindwa nikajiuliza nilipize kisasi...gani kwa huyu MZEE japo katusaidia sikupata ufahamu kama nyau ni mboga huko kwa wazairwaa!!!....nikapata jibu bora kupiga chabo mkewe akienda kuoga!!!...
Basi nitakuwa nimelipiza kisasi bila chenchi ,na kumuenzi mshikaji wangu J.

Ila sikufanya nilivyokusudia nikaona nibora kumtorosha binti YAKE wa PILI aliyeitwa mimii...ili nije naye Tz iwe kama fidia....Tulikaa pale kijijini kwa siku mbili kisha tukaondoka na mtumbwi wetu na wale wakongo waliokuwa wanakimbia vita,yule binti wa yule MZEE nilimpiga saundi kali....akanielewa siunajua tena!!!!! mtanzania....anavyoshobokewa,kwa kifupi nilifanikiwa kumtorosha na kumleta Tanzania na kuachana na wazo potofu la kumpiga chabo mama yake....tulifunga ndoa na Mimii,mke wangu mkongo.... tukafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume....Ila tuliachana baada ya yeye kutaka twende kambini nyarugusu ili tutafute nafasi za kwenda ulaya/America....Mimi nilikataa,nikiamini ukikomaa hapa hapa bongo kwa nyerere, utatoka tu japo utachelewa!!!!....mwenzangu aliondoka 2006,na mwangu wakaelekea Canada kama wakimbizi....mpaka sasa sijawaona zaidi ya mawasiliano....
WhatsApp basi,huwa anitupi hunitumia dola 100 kila mwezi,japo aliolewa na zee lilochoka LA kizungu na....kushindwa kunitumia nauli niende tukale DuNIA.

mixture ya chai ,mchuzi wa pweza na alkasus

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Oyo jf sio km fcbku..huu ujinga uliofanya hapa umenikera sana.
Kwani ukicoment tuu kwa wenzio si unaendelea kuwa mwanachama hai? Kuliko kuanzisha sread ya ki za mwamwa kama hii.
 
Fcbku ni nini?
Mbona sijakuelewa mheshimiwa...Ila samaani kwa kukukera.
 
Back
Top Bottom