Nchi ya Ajabu: Nimewaona Wafanyabiashara wa Tanzania wamekuja Kampala kununua Bidhaa za China

Kwenye Korosho, Mimi nilishakuja na Mada hapa. Kwamba. Waliomshauri Raisi, wanatakiwa kuwa Gerezani na Viboko Juu. Kumbuka Raisi siyo mfanyabiashara, ila Ana washauri wa biashara na mishahara wanalipwa. Hawa hawana tofauti yoyote na Wahujumu uchumi.
Wewe acha kumtetea huyo mtu wako.Tatizo kubwa ni yeye na wasaidizi wake wanafanya anachokitaka.
 
Kwenye Korosho, Mimi nilishakuja na Mada hapa. Kwamba. Waliomshauri Raisi, wanatakiwa kuwa Gerezani na Viboko Juu. Kumbuka Raisi siyo mfanyabiashara, ila Ana washauri wa biashara na mishahara wanalipwa. Hawa hawana tofauti yoyote na Wahujumu uchumi.
Anashaurika? Si ameshasema anawatukanaga...!!
 
Nakubaliana na wewe mkuu, Dawa ni kupanga safu mpya kabisa. Hawa waliokuwepo ni mtandao wa Kishetani. Ni watu wenye Choyo wivu na Roho za kwanini kwa wafanyabiashara wa Nchi Hii. Pls, Mheshimiwa Raisi. Fukuza haraka hawa watu, hawana wanachokusaidia, wameshakujengea uadui mkubwa na Wafanyabiasha.
Siyo suluhisho... ishu hapa ni ONE MAN SHOW..... Fikiria zile amburence "zilizookotwa" bandarini...
 
Usishangae kusikia hao wenye hizo mbinu chafu ni wasomi waliosomeshwa kwa fedha za serikali huko ughaibuni,tusitegemee maendeleo tusijdanganye
 
Yeye ndie anaewapa target ya kukusanya kwa mda flan so huwez kumuexlude kwenye hili, yeye ndie chanzo cha tatizo tuuseme ukweli.
Ni kweli mkuu, yeye ndiye anayetoa target. Lakini kumbuka hata huyu anayepewa target ni lazima awe na akili ya kukusanya kodi na kuiboresha hali ya huyo anayemlipa kodi. Ili mwakani akusanye zaidi. Sasa Kama unakusanya kodi na huyu anayekupa kodi unamwacha hoi masikini, unategemea nini mwakani? Bado kuna tatizo kubwa.
 
Mkuu sio ishu ya thaman ya sh na pesa ya uganda ndio znamata hapo

Na una uhakika kwamba hzo bidhaa znapita bandar ya dsm na sio mombasa au kwingne,..

Mambo ni meng,labda niwe sjaelewa injinia mim na maswal ya kodi wap na wap
 
Siyo suluhisho... ishu hapa ni ONE MAN SHOW..... |Fikiria zile amburence "zilizookotwa" bandarini...
Mambo mengine siyo ya kufukua sana Mkuu, mengine tupotezee. Wakati mwingine tuisaidie Nchi yetu kiushauri tu. Ipo Siku watasikia.hilo la One Man Show, yeye mwenyewe ameshastuka anaingia Chaka. Sasa hivi anabadilika sana.
 
Nchi imeona biashara iendeshwe na wamachinga kwa ushuru wa elfu 20. Machinga atafuata mzigo ulioingilia bandari yet kwa bei nafuu halafu arudishe bongo, avae kitambulisho Cha elfu 20, asambaze mzigo huku wenye maduka wakikodoa macho na EFD machine. Subiri makusanyo ya TRA labda yatapanda kupitia machinga.
 
Naunga mkono hoja, hata mimi, bi mdogo ni mfanyabiashara wa nguo, alianzia kwenda South, nguo za kule ghali, akaenda Uturuki, nguo ni quality lakini overheads kubwa. Akaja kwenda China, ili ilipe lazima ulete mzigo mkubwa, sasa anakwenda Uganda, aki fly Jumatano, Jumamosi yuko hapa, mzigo wote ni wa Mchina, uliopitia bandari yetu!. Anasema Kariakoo is full of the cheapest Chinese stuff, Uganda has a better quality.
P
 
Mkuu sio ishu ya thaman ya sh na pesa ya uganda ndio znamata hapo

Na una uhakika kwamba hzo bidhaa znapita bandar ya dsm na sio mombasa au kwingne,..

Mambo ni meng,labda niwe sjaelewa injinia mim na maswal ya kodi wap na wap
Swali ni Zuri Mkuu. Ni kweli inawezekana bidhaa zikapitia bandari ya Mombasa au Dar. Lakini kumbuka mtoza kodi ni Mamlaka ya Mapato Uganda. URA. Kuhusu thamani ya pesa hakawezi kusababisha bidhaa iuzwe rahisi Nchi nyingine. Kumbuka, hizi bidhaa zote zinatoka China na zote zinanunuliwa kwa Dola
 
Mambo mengine siyo ya kufukua sana Mkuu, mengine tupotezee. Wakati mwingine tuisaidie Nchi yetu kiushauri tu. Ipo Siku watasikia.hilo la One Man Show, yeye mwenyewe ameshastuka anaingia Chaka. Sasa hivi anabadilika sana.
Nini umeona ndo alama ya kubadilika kwake? Unakumbuka maneno ya mbunge wa KILWA Bwana BWEGE..!!??? Mwishooooooooooooooooooooniiiiiiiiiiiiiiiiiiii mtabadilika.... Tunawajua nyie CCM...... Mwisho wakunukuu
 
Usimtoe mheshimiwa wako kwenye hili kwani linamhusisha 100%.
Yeye ndiye muasisi wa wafanyabiashara kuishi kama mashetani. Yametimia sasa
Wakati anahangaika kuwafanya matajiri waishi kama mashetani, ALITEGEMEA AKINA SISI WA LIULI MBINGA, WA KYERWA KAGERA, WA KISHUMUNDU KILIMANJAO, etc... TUISHI KAMA NANI?
 
Juzi nilikuwa TRA. Katika watu 10 tuliokuwa kwenye line, 7 walikuwa wapo pale “kufunga au kusimamisha biashara zao kwa muda”. Wengi sasa hivi wapo radhi wastopishe biashara zao rasmi na waanze kufanya upya kimyakimya bila kutoa taarifa TRA na Manispaa.

Kuna haja TRA kuangalia wapi tunakosea na kurekebisha baadhi ya sheria mbovu za kodi zisizo na tija
 
Back
Top Bottom