Nchi ya Ajabu: Nimewaona Wafanyabiashara wa Tanzania wamekuja Kampala kununua Bidhaa za China

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Juzi Alhamisi nimeshuhudia mwenyewe. Mwanzoni nilikuwa siamini nikijua ni siasa tu, nikiwa katikati ya Jiji la Kampala wakati wa lunch time ktk mgahawa mmoja nilikutana na Wafanyabiashara watatu Watanzania. Nilikuwa nimekaa meza ya jirani na wao, niliposikia Kiswahili chao fasaha nikagundua hawa ni ndugu zangu wa Home, nikasogea tukakaa pamoja, hapo ndipo Mazungumzo yakaanza.

Ktk maongezi kila mmoja wetu alijitambulisha ni nani na amefata nini Kampala, wao walisema kuna bidhaa huwa wanazichukua Kampala na kuzipeleka Tanzania. Aina ya bidhaa sitazitaja. Lakini ni bidhaa hizi hizi za kawaida zinazotoka China na Zimepitia bandari ya Dar kuja Kampala. Nilijaribu kuwadadisi ya kwamba kwanini wasinunue Dar wakati pia zipo, walijibu bei ni kubwa sana na haiwezi kuwalipa.

Tuliongea mengi sana. Lakini nilichogundua ni kwamba, aidha kuna mkakati wa Makusudi wa baadhi ya watendaji wa TRA wa kuhakikisha kwamba hakuna mfanyabiashara wa Tanzania atakayefanikiwa kibiashara. Kwa sababu haiwezekani Bidhaa inayotoka China kupitia bandari yetu halafu iuzwe kwa bei ya chini Kampala kuliko Dar.halafu wafanyabiashara wetu waifate Kampala na kuirudisha Dar na waiuze Dar na kupata faida kuliko Yule Mtanzania aliyenunua bidhaa hiyo hiyo China na akaipitisha bandarini dar na akaiuza Dar.

Madhara yanayosababishwa na Hawa Majini TRA ni makubwa sana tofauti na wenye akili ndogo wanavyofikiria. Nitayataja baadhi.

1 Wafanyabiashara majirani zetu ambao hawana bandari wamekoma kuja Tanzania

1 Wafanyabiasha wetu haswa wa Soko letu kubwa la Kimataifa k,koo wako hoi kiuchumi

3 Wenye Mahotel ambao target Yao ilikuwa ni kuwapokea wageni kutoka Zaire, Malawi, Zambia,
Burundi, Rwanda, lazima watafilisika kwa kukosa wateja.

4 Wenye Restaurant wengi watafunga kwa kukosa wateja. Na hivyo wafanyakazi wengi
Watapoteza ajira.

5 Wabeba mizigo Ajira zao zitakufa rasmi hawa ni kuanzia wale Vibega, matoroli, bajaji, kirikuu, Canter
Fuso malori nk, hii cheni ni kubwa

6 Mama lishe biashara sitadoda.

7 TRA wenyewe hawatoweza kukusanya tena kodi kwa sababu biashara wameua wenyewe.

Maoni yangu,

Pamoja na Raisi kukaa na wafanyabiashara wachache, pia ni lazima TRA wenyewe wakae na Wafanyabiashara haswa wale wanao import bidhaa toka Nchi mbali mbali Duniani. Ili kupanga namna na viwango bora vya kulipa kodi.

TRA ni lazima iwe inawapeleka baadhi ya wafanyakazi wake nje kujifunza ktk Nchi Kama Dubai , Hong Kong, China Uganda South Africa, kuona wao wamewezaje kufanikiwa ktk Suala la kodi kwa kiasi hicho na Kufanya hizo Nchi Wafanyabiashara wakawa na furaha.
 
Wi ar in the raiti traki......labda traksuti

Halafu ndo unapendekeza wapelekwe Dubai,Hong kong kujifunza mapumbavu hayo yaache yakae humu humu yanaendaga shoping tu huko badala ya kujifunza. Nna hasira nao hao nishafunga biashara zangu mbili
 
Jiulize hii TRA haikuwepo katika tawala zilizopita?

Elewe tatizo ni bwana yule anaetaka sifa ya kuonekane kuwa katika awamu yake ameongeza makusanyo kuliko watangulizi wake.
Mimi hapo napishana na wewe Mkuu, kwa sababu Kama ni juhudi za kuwatumbua Mbona anafanya kila Siku? Angekuwa anafurahia wala asingepata Muda wa kukaa na wafanyabiashara . Tatizo lipo hapo hapo TRA tu.
 
Miaka 4 ilopita hali ilikuwa kinyume na hicho ulicho kisema. Bidhaa zilininuliwa dar kwenda huko. TRA msiwalaumu sana tatizo ni la Magu, tra walikuwepo na walikuwa hawafanyi kama wafanyayo sasa, wamebadilika baada ya ujio wa Magufuli. Pesa inatafutwa kwa namna zote.
 
Mimi hapo napishana na wewe Mkuu, kwa sababu Kama ni juhudi za kuwatumbua Mbona anafanya kila Siku? Angekuwa anafurahia wala asingepata Muda wa kukaa na wafanyabiashara . Tatizo lipo hapo hapo TRA tu.
Hata kwenye kikokotoo hadaa hii tuliiona.

Usisahau na ya koroshow.

Jiulize pia ni nani yuko nyuma ya vitambulisho vya wamachinga.
 
Kutumbua na kuacha viini vya jipu ni kazi bure
Nakubaliana na wewe mkuu, Dawa ni kupanga safu mpya kabisa. Hawa waliokuwepo ni mtandao wa Kishetani. Ni watu wenye Choyo wivu na Roho za kwanini kwa wafanyabiashara wa Nchi Hii. Pls, Mheshimiwa Raisi. Fukuza haraka hawa watu, hawana wanachokusaidia, wameshakujengea uadui mkubwa na Wafanyabiasha.
 
74 Reactions
Reply
Back
Top Bottom