- Thread starter
- #41
TRA lazima wajipange sana Mkuu. Hawa watu bado wanatumia ule mfumo wa tangu tumepata Uhuru. Hawataki kabisa kubadilika kwenda na mfumo wa uchumi wa ushindani wa Dunia ya sasa. Wenzetu Kenya na Uganda wamebadilika sana. Pamoja na sheria za kodi za East Africa lakini nakuhakikishia hii sheria ni kiini macho tu. Kenya na Uganda hawafuati kabisa hizi sheria. Wao wanafata matakwa ya wafanyabiashara wao.Naunga mkono hoja, hata mimi, bi mdogo ni mfanyabiashara wa nguo, alianzia kwenda South, nguo za kule ghali, akaenda Uturuki, nguo ni quality lakini overheads kubwa. Akaja kwenda China, ili ilipe lazima ulete mzigo mkubwa, sasa anakwenda Uganda, aki fly Jumatano, Jumamosi yuko hapa, mzigo wote ni wa Mchina, uliopitia bandari yetu!. Anasema Kariakoo is full of the cheapest Chinese stuff, Uganda has a better quality.
P
Ndiyo maana unaona k,koo imekufa. Wateja wote wa Zambia Malawi Zaire wamehamia Nairobi. Kampala Nenda utawakuta wamejaa Mahotellini usiku. Mchana wanafungasha tu mizigo. Shida waliyonayo hawa TRA wa Tanzania ni kubwa kuliko Raisi anavyofikiria.