mwakweya70
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 414
- 106
Wahoji nini wakati wamepitishwa?
Well said!
Hapa tatizo ni mfumo huu ulioasisiwa na chama 1!.
Lkn watu hawaelewi
Ooh magufuli jembe sijui nn!
Hakuna jipya chini ya huu mfumo!!
Tanzania hakuna waandishi wa habari kuna reporters tu tena sio reporters makini ni reporters wanaoongozwa na matakwa ya matumbo yao
Kwa hali ilivyo ni bora iwe hivyo kwa muda. . . . . . " kuna mambo labda hayahitaji mjadala na labda kuna mambo yakiwekwa wazi kabisa itahitajika nguvu kubwa zaid kutuliza jamii" hizi ni aasumptions ambazo zinaweza sababisha nchi kuelekezwa nini cha kufanya . . . . .
Naamini ni kwa faida ya wengi na ya muda mrefu. . .
Unless kuna mapinduzi, hiyo ni standard practice dunia nzima.
Fuatilia kilichompata Princess Diana yule wa Uingereza aliyetaka kuolewa na mwarabu, alipatiwa ajali na akamalizwa haraka sana.
Sasa hao usalama wa taifa si waingie na kwenye michakato ya vyama vingine ili kuweka usawa katika kupata mtu safi mbele ya wananchi?
Mfumo ni watu mmoja mmoja na taasisi waziundazo. . . . .Ukipata key palyer mzuri anaweza badili mchezo mkaacha kufungwa mkaingia kwenye kutoa droo. . . . .
So far apewe benefit of doubt. . . . . sababu anaweza akiamua sasa asipoamua tutaanzia hapo japo tutakuwa tumeumia. . . .
Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?
Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
========
Some interesting comments:
Well nailed. . . . .Wewe ndo umeongea point kabisa.....watu hapa wanachangia kisiasa zaidi..,
Ikitokea UKAWA walete mgombea maslahi mfukoni, pia CCM watuleteee mwingne kuipeleka nchi shimoni ndo tuwaache tu kisa nini?
Kuna mambo wananchi hawawezi kuyasikia na ikitokea wakafaham juu ya hao wanaowashabikia wanaweza wakastajaabu na kupata stroke
Hii nchi bado changa sana hata huo upinzani inabidi ujengewe uwezo kuongoza nchi.....Mtauzwa hadi mayai yaliyo tumboni kwa ushabiki watanzania ....tulieni tujenge hii nchi yetu sote si ya kuendeleza kusini, Kaskazini, wala kanda yeyote ile..tunahitaji maendeleo na tuache propaganda tusizozijua kwa undani wake...hatuwezi kabidhi nchi kwa mtu kisa mahaba ya siasa
We need people like John Edgar Hoover katika ofisi za Usalama wa Taifa. Mtu akayepigania Usalama wa taifa uwe na nguvu kama walizokuwa nazo enzi za Nyerere au zaidi ya hapo. Wawe na misuli ya kwenda sehemu yoyote ya nchi na nje ya nchi bila ya kuingiliwa na wanasiasa. wakatae kutumika kisiasa kama John Edgar Hoover, wajikite kwenye ufanisi wa kazi zao.Kwenye maelezo yako umesema kwa kumuweka mtu anaweza leta hayo mabadiliko
Sasa Magufuli sidhanikama nimsikivu enough hata kwa hao KITENGO
na power ya urais inampa nguvu hata ya kukisuka KITENGO kwa malengo yake
ni gamble ambayo watu wenye uzalendo wa kutosha wasingeifanya
kitengo ndicho chenye kuamua mpaka hesabu za kura ziendee kwa nani.
ha ha ha...naona sasa vijana wamelipwa kuja mitandaoni kutuletea porojo.
ACHENI POROJO NA KUTUMIKA...
Lowasa mwenyewe ni hatari kwa afya yake binafsi...sembuse familia yake na watanzania.
Ah wapi! Ukibahatika kutembelea sehemu mbalimbali za nchi ndo utagundua kwamba maamuzi 'yao' mengi wala si kwa manufaa ya taifa.
Sina uhakika sana na hili la kiinua mgongo cha wabunge na sijalisikia tena tokea karibu wiki mbili zilizopita lakini kama kweli hicho kitengo dhima yake kuu ni kulinda maslahi ya taifa basi kingeingilia kati ili hayo mabilioni ambayo yanadaiwa wabunge watalipwa yaende sehemu ambazo zina uhitaji mkubwa zaidi.
Thubutu! Watanzania wa kizazi hiki hawana ujasiri wala uthubutu wa kupishana na maamuzi ya 'kitengo'. Majuzi tu hapa tumeona jinsi ambavyo rafu imechezwa hadi Magufuli akawa railroaded kuwa mteule wa chama na yule ambaye iliaminika ndiye aliyekuwa chaguo la wengi kutoselewa mbali tena kwa udhalilishaji wa hali ya juu. Walipojitokeza watu wawili watatu kujaribu kupinga kilichotokea walizimwa haraka sana na wakarudishwa mstarini.
Sisi hatuna tume huru ya uchaguzi. Hiyo ambayo tunayo sasa ni extension ya 'kitengo' tu. Hebu tumia tu hata busara zako za kawaida [common sense]. Ni nani ambaye huiunda hiyo tume? Mwenyekiti wa hiyo tume na hao wenzake huwa wanapatikanaje?
Kwa ujumla mimi sioni faida yoyote ile hususan kwenye urais. Kwa jinsi ambavyo mambo yalivyo hivi sasa CCM kuja kushindwa na wapinzani haiwezekani hata kidogo. Kutegemea mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyeteuliwa na rais/ mwenyekiti wa CCM kumtangaza mshindi wa kiti cha urais mgombea wa upinzani ni sawa na kutegemea ngamia apite kwenye tundu la sindano.
Kama kuna anayedhani hiyo tume ya uchaguzi siyo extension ya kitengo namsihi arudi kumwangalia mmoja wa watangaza nia wa CCM - Jaji Agustino Ramadhani. Huyu bwana nadhani alikuwa ni makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuanzia mwaka 1993 hadi 2002 na kuanzia 2002 hadi 2007 alikuwa makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar [eti hawa watu nao wana tume yao ya uchaguzi!!].
Hiyo inatueleza nini kuhusu hiyo inayoitwa tume ya uchaguzi? Je, ina maana tume nzima imejaa makada wa CCM? Mimi nadhani ni hivyo.
Ni maigizo tu. Demokrasia gani hiyo isiyotoa fursa sawa kwa washindani wote? Hata katiba ya nchi inayoendana na misingi mikuu ya kidemokrasia hatuna. Eti juzi juzi tu hapa ndo tumestuka na kuona umuhimu wa kuandika katiba mpya.
Kwa nini hilo halikufanyika hapo awali kabisa mwaka 1992 tulipoingia kwenye siasa za vyama vingi?
Na kusema ukweli Tanzania wala hatuna siasa za vyama vingi. Siasa zetu ni za chama kimoja ila kuna mazingaombwe yanayofanya watu wadhani kwamba tuna siasa za vyama vingi. Hatuna.
Wiki ilopita tumeshuhudia jinsi ambavyo nadhari karibu ya Watanzania wote ilivyoelekezwa huko Dodoma katika shauku ya kutaka kujua rais ajaye atakuwa nani.
Hakuna ubishi wowote ule kuwa rais wa 5 wa Tanzania ni John Magufuli.
Hata kupatikana kwake hakukuwa kwa demokrasia. Kinachosubiriwa sasa ni kukamilishwa tu kwa taratibu [igizo la uchaguzi mkuu hapo Oktoba] na yeye kuapishwa, basi.