Nchi inabidi kuongozwa na mifumo thabiti na imara na si matamko ya wanasiasa. Wasomi tulisaidie Taifa

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,132
45,932
Tumefika hapa tulipo kwa sababu hatuna mifumo ya kuongoza nchi.

Inashangaza kuona anatokea mtu mmoja mjinga anavunja katiba ya nchi na bado anaendelea kuwa kiongozi.

Hatuwezi kupiga hatua kama Taifa liashindwa kuwa na mfumo sahihi.

Wasomi hakikisheni mnalikomboa Taifa kila kitu kinabi kuwa written na sio Mtu anaongea ongea tu kama mlevi.

Kama kila mwezi katika kata ya Temeke wanazaliwa watoto 1000 je Serikali inabidi kuajiri walimu wangapi na kujenga shule ngapi?

Ebu hakikisheni mnakuwa na mifumo ya kuongoza nchi na mtu akitoka nje ya mfumo anabidi kukaa benchi and nothing else.
 
Fyetueni Watoto nitawasomesha bure.Ilisikika sauti ya kichaa mmoja ikihamasisha kuzaana kama Nzige
Population inaongezeka kwa kasi Sana maana masikini huwezi kuwatenganisha na kuwa na watoto wengi Sasa swali langu je.

Kama Temeke hosptali wanazaliwa watoto elfu 1000 kila Mwezi je hapo Serikali inabidi kujenga shule ngapi na kuajiri waliimu wangapi maana itafika Muda watu watakosa shule na watakosa pesa za kuajiri walimu ili kuweka man power.

Sasa wanasiasa wamelala usingizi wa pono huku wakijificha katika kichaka cha Uzalendo uchwara.
 
Wachache mno, yaani ongezeko la watu 12,000 kwa mwaka ndo waona wengi
 
Wafahidhina wa kuzaa hawawezi kuelewa matokeo ya hii kasi kubwa ya kuzaliana isiyoendana na ukuaji wa chumi. Hali itazidi kuwa mbaya zaidi katika huduma za kijamii, miondombinu na ajira.
 
Kila mwezi kwenye kata moja kufyatuliwa watoto 1000 ni kidogo?! Kwa hali hiyo serikali itafanya kazi nyingine zaidi kujenga madarasa na kutengeneza madawati??
Wachache mno, yaani ongezeko la watu 12,000 kwa mwaka ndo waona wengi
 
Mifumo imara inajengwa na watu imara, katiba imara inajengwa na watu imara.

Maendeleo ya kasi/ Rapid economic development yana letwa na watu imara + katiba imara + mifumo imara.
 
Mifumo imara inajengwa na watu imara, katiba imara inajengwa na watu imara.

Maendeleo ya kasi/ Rapid economic development yana letwa na watu imara + mifumo imara.
Umeongea vizuri sana,je hii nchi yetu ina watu imara kweli?
 
Umeongea vizuri sana,je hii nchi yetu ina watu imara kweli?
Haina watu imara kwa sababu haina mfumo wa kutengeneza watu imara.

Mimi ni mtu naye fuatilia sana siasa za kimataifa, nitakupa mfano wa nchi inayo tengeneza watu imara.

China ina fanya vizuri sana katika kutengeneza watu imara kupitia mfumo wake wa kisiasa, licha ya kuwa chama cha mapinduzi kina jaribu kunakili baadhi ya mambo kutoka China hasa hasa katika chama cha kikomunisti lakini waneshindwa kuendana na namna China inavyo tengeneza watu imara katika taifa lao.

Nakupa case study: jifunze kuhusu siasa za China, chama chao cha kikomunisti, michakato ya kupatikana viongozi, michakato ya kujiunga na chama na mfumo mzima wao wa uongozi kuna vitu bora utapata.

Uki fuatilia hivyo utanielewa nacho zungumza.
 
Kila mwezi kwenye kata moja kufyatuliwa watoto 1000 ni kidogo?! Kwa hali hiyo serikali itafanya kazi nyingine zaidi kujenga madarasa na kutengeneza madawati?
Kwa mtizamo wangu,namuunga mkono mtoa mada. Kama wasomi wangekuwa na akili basi hata hiyo population isingetuathiri
 
Watu Kama nyie ndo hamna kitu upstairs so hamuwezi kuona Kesho mnaishi kama mmekufa wakati mpo hai
Kuna nchi zina population na maisha yanaenda chanya,kwa hiyo jamaa yupo sahihi.
Point tayari umeshaiweka wazi kwamba wasomi hawalisaidii taifa.
Wamejikita kusaka teuzi tu.
 
Haina watu imara kwa sababu haina mfumo wa kutengeneza watu imara.

Mimi ni mtu naye fuatilia sana siasa za kimataifa, nitakupa mfano wa nchi inayo tengeneza watu imara.

China ina fanya vizuri sana katika kutengeneza watu imara kupitia mfumo wake wa kisiasa, licha ya kuwa chama cha mapinduzi kina jaribu kunakili baadhi ya mambo kutoka China hasa hasa katika chama cha kikomunisti lakini waneshindwa kuendana na namna China inavyo tengeneza watu imara katika taifa lao.

Nakupa case study: jifunze kuhusu siasa za China, chama chao cha kikomunisti, michakato ya kupatikana viongozi, michakato ya kujiunga na chama na mfumo mzima wao wa uongozi kuna vitu bora utapata.

Uki fuatilia hivyo utanielewa nacho zungumza.
Mkuu upo sahihi 100% shida ya nchi yetu ipo hapo.
Tupo katika jamii dhaifu sana.
 
Hivi kuna mifumo thabiti?

Katika mifumo thabiti, naamini uwepo wa mfumo mmoja tuu, nao ni Binadamu. Na vilevile, haujitoshelezi kama mfumo thabiti....

Umegusia huko hivyo imenibidi kutumia mfano wa mifumo ninayojua.

Hatahivyo
Kama kila mwezi katika kata ya Temeke wanazaliwa watoto 1000 je Serikali inabidi kuajiri walimu wangapi na kujenga shule ngapi?
Je,kata ya Temeke kila mwezi ina watu wangapi wanaopoteza maisha.? Wanaokufa? Manake kinyume cha kuzaliwa ni kufa...it is a given fact.

Kumetokea nini huko Temeke? Ni Mwanasiasa gani aliyetoka nje ya mfumo thabiti?
 
Hivi kuna mifumo thabiti?

Katika mifumo thabiti, naamini uwepo wa mfumo mmoja tuu, nao ni Binadamu. Na vilevile, haujitoshelezi kama mfumo thabiti....

Umegusia huko hivyo imenibidi kutumia mfano wa mifumo ninayojua.

Hatahivyo

Je,kata ya Temeke kila mwezi ina watu wangapi wanaopoteza maisha.? Wanaokufa? Manake kinyume cha kuzaliwa ni kufa...it is a given fact.

Kumetokea nini huko Temeke? Ni Mwanasiasa gani aliyetoka nje ya mfumo thabiti?
Serikali imeanza kuzidiwa , population inaongezeka kwa kasi na life span inaongezeka hapa Mimi natajaribu kutaka nchi iwe na mifumo sahihi na sio nchi kuongozwa kwa matamko mfano hawa watoto elfu moja wanapozaliwa kila Mwezi katika kata ya moja maana yake huko Mbele kitatokea Matatizo ya ukosefu wa shule, zahanati n.k mfano shule nyingi za mjini darasa moja wanakaa watoto 100+ badala ya 45 so wanasiasa wamepiga usingizi wa pono.
 
Sawa, na wanakufa vilevile. Kwa manitiki hiyo Tutakosa ardhi ya kuwazika?
Aiseee wanasiasa wana kazi....nimeona suala hili Uchina, Marekani, Uingereza na kwingineko, cah kustahabisha hakuna aliye na 'mfumo thabiti'.

Mtafute Bill gates
 
Back
Top Bottom