Kilbark
JF-Expert Member
- Feb 25, 2008
- 572
- 161
Hawa jamaa wasituzingue wameviua viwanda kibao ngoja nitaje vichache tu ninavyovijua tuanzie pale ubungo kulikuwa na kiwanda cha UFI, Fishnet,Maziwa,Urafiki. Mbeya kulikuwa na kiwanda cha ZZK-MBEYA. Haya twende kwenye usafirishaji kulikuwa na ma kampuni kila mkoa yaliyokwenda kwa jina la RETCO hapo ikitanguliwa na prefix zenye jina linalotambulisha mkoa fulani. Twende Ugawaji,SUKITA,RTC hawa jamaa wasitake kutuchanganya AISCO imefia wapi na kulikuwa na kiwanda kizuri tu hapa Tanzania cha ku assemble matekta ya VALMET. Twende STAMICO jamaa waeua kila kitu tulikuwa na TANCUT Almasi pale Iringa. Wa kulaumiwa nani? Nyerere hakuwa na hiyana kila sekta aliipatia japo chuo mfano chuo cha kilimo Sokoine. Mimi siongei zaidi.