Nchi imeuzwa!

Naona This Day is picking up our cue!

Unaweza ukaandika kwa lugha yetu ya kiswahili ili wasomaji tuweze kuelewa vizuri unachokiongelea.

Janejo,

Sitaki kuondoka kwenye mada, nataka kuelezea hali halisi mara moja halafu turudi kwenye mada.

Naelewa umuhimu wa Kiswahili na hadhira yake.Lakini katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi, ambao kama alivyosema Al-Ustaadh Al-Hadj Ali Hassan Mwinyi kwamba "Kiingereza ni Kiswahili cha dunia" tukitaka kuenda popote kwa mafanikio inabidi tujifunze kiingereza.

Sasa kama tunataka kuwaandikia hawa Wamarekani na WaCanada wasiojua Kiswahili kwenye "The New York Times" na "Wall Street Journal" wanakoweza kumsuta huyo mwenzao Sinclair tutaandika Kiswahili kweli?

Mimi ni Mtanzania ninayekipenda Kiswahili, lakini nakubaliana ma Mzee Mwinyi kwamba kuna haja ya kujifunza kiingereza zaidi ili tusiachwe.

He is not talking too fast, some of us are listening too slow.
 
Mkuu Kitila,

Je hao best sons and daughters wa TZ tunao?

Naanza kupata wasiwasi kwamba huenda TZ tuna watu wachache sana ambao wanaweza kutusaidia na bahati walio wengi sio wanasiasa au hawawezi kuchaguliwa kwenye siasa.

Hali inasikitisha sana na kutisha pia. Tuombee 2010 labda tupate watu wazuri wengi kwenye nafasi mbalimbali.

Tunao sana watu Mtanzania. Mama wa matatizo ya uongozi wa nchi yetu ni kuendelea kuamini kwamba ni CCM pekee yenye watu wanaofaa kuwa viongozi. Hili la kuendelea kuamini kwamba ni CCM tu ndiyo yenye uwezo wa kutawala sasa limezalisha matatizo mengine matatu ya hatari kabisa.

i) mfumo wa wa uongozi katika CCM ni wa ki-mediocre kiasi kwamba watu wenye sifa zao wanakuwa scared kushiriki katika mchakato wa kawaida wa kisiasa. Ndio maana CCM ina watu wengi sana wazuri lakini wote hawa wanakubali kusemewa na akina Tambwe na Makamba. Sasa kama chama kikubwa kama CCM kinakuwa na spin doctor anayeitwa Tambwe na General Secretary anayeitwa Makamba, unategemea hapo kuna swala la merit tena? Ajabu bado watanzania, tena wengi kabisa wapo hapa JF, wanaendelea kuamini kwamba hawa jamaa wanaweza wakaibadilisha nchi! Surely, we must be delusional and day dreaming!

ii) wale wenye moyo wa kujaribu mara nyingi hukwama kwa sababu wanapoenda wanauza sifa badala ya ujanjaujanja na hivyo hujikuta hawafui dafu.

iii) Wale wenye uwezo wao na wakafanikiwa kupenya kuingia kwenye mfumo wa uongozi wa CCM hujikuta wanaambukizwa uchafu kwa kasi ya kutisha. tafiti zote zinaonyesha kwamba ni vigumu kuepuka ushetani unapokuwa unaishi kwenye ushetani. Ni kwa sababu ya mazingira haya wale askari wa marekani wakajikuta wanatesa watu kule kwenye lupango ya Guantamalo. Ni mazingira ya ushetani yaliyosababisha askari wa Ujerumani wakubaliane na Hitler kufanya unazi. Sasa basi ni ujuha mkubwa kuendelea kuamini kwamba unaweza kwenda CCM na ukaibadilisha na hivyo kuleta tija katika nchi yetu.

Lengo kubwa la CCM, ambalo hata baadhi ya wanachama wake hapa wamethibitisha, ni kukamata madaraka, lakini wala hawajui wayafanyie nini hayo madaraka zaidi ya kuwasaidia kuhama kutoka Kimara kwenda Mbezi Beach na kuwahamisha watoto wao kutoka shule ya msingi Tandika Reli kwenda St Marys au ka-International school fulani huko Uganda au Kenya. Kwa hiyo kwao madaraka ni lengo sio njia. Tunahitaji chama ambacho lengo lake ni kutumia madaraka kama njia ya kuwapa watanzaia serikali safi yenye kutekeleza wajibu wake wa kiserikali na kuwapa kila nafasi na furasa kila mwananchi ya kutimiza kipaji na uwezo aliopewa na mwenye Mungu.

Madamu tunaamini kwamba CCM haijatutesa vya kutosha na kwamba ni CCM pekee yenye uwezo wa kutawala kwa sasa na kwamba huwezi kuwa kiongozi mzuri hadi upitie CCM, then tutaendelea kufungua thread za ufisadi katika JF na magazeti yetu yataendelea kujaa habari za wana CCM walivyopora hazina badala ya habari za maendeleo.

Wanasaikolojia wanaamini kwamba binadamu hupata wanachotaka na kutafuta. What goes around it is what comes around. Ufisadi na matatizo ya nchi yetu sio ya bahati mbaya. Nido nikasema kuwa Kwa kuchagua kuendelea kukaa chini ya CCM tumechagua kuendelea kuishi na ufisadi.

Bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo tukiamua. Hatua ya kwanza ni kuachana na fikra kwamba hakuna chama kingine chenye uwezo wa kutawala isipokuwa CCM. Tuachane na maneno ya rejareja kwamba wapinzani wasubiri kwanza wakomae, waingie bungeni, etc. Kama Mwalimu Nyerere angekuwa mwoga kama baadhi ya watanzania hapa asingekubali kupokea uhuru mwaka 1961 maana alikuwa na madaktari watatu nchi nzima.
 
Tunao sana watu Mtanzania. Mama wa matatizo ya uongozi wa nchi yetu ni kuendelea kuamini kwamba ni CCM pekee yenye watu wanaofaa kuwa viongozi. Hili la kuendelea kuamini kwamba ni CCM tu ndiyo yenye uwezo wa kutawala sasa limezalisha matatizo mengine matatu ya hatari kabisa.

i) mfumo wa wa uongozi katika CCM ni wa ki-mediocre kiasi kwamba watu wenye sifa zao wanakuwa scared kushiriki katika mchakato wa kawaida wa kisiasa. Ndio maana CCM ina watu wengi sana wazuri lakini wote hawa wanakubali kusemewa na akina Tambwe na Makamba. Sasa kama chama kikubwa kama CCM kinakuwa na spin doctor anayeitwa Tambwe na General Secretary anayeitwa Makamba, unategemea hapo kuna swala la merit tena? Ajabu bado watanzania, tena wengi kabisa wapo hapa JF, wanaendelea kuamini kwamba hawa jamaa wanaweza wakaibadilisha nchi! Surely, we must be delusional and day dreaming!

ii) wale wenye moyo wa kujaribu mara nyingi hukwama kwa sababu wanapoenda wanauza sifa badala ya ujanjaujanja na hivyo hujikuta hawafui dafu.

iii) Wale wenye uwezo wao na wakafanikiwa kupenya kuingia kwenye mfumo wa uongozi wa CCM hujikuta wanaambukizwa uchafu kwa kasi ya kutisha. tafiti zote zinaonyesha kwamba ni vigumu kuepuka ushetani unapokuwa unaishi kwenye ushetani. Ni kwa sababu ya mazingira haya wale askari wa marekani wakajikuta wanatesa watu kule kwenye lupango ya Guantamalo. Ni mazingira ya ushetani yaliyosababisha askari wa Ujerumani wakubaliane na Hitler kufanya unazi. Sasa basi ni ujuha mkubwa kuendelea kuamini kwamba unaweza kwenda CCM na ukaibadilisha na hivyo kuleta tija katika nchi yetu.

Lengo kubwa la CCM, ambalo hata baadhi ya wanachama wake hapa wamethibitisha, ni kukamata madaraka, lakini wala hawajui wayafanyie nini hayo madaraka zaidi ya kuwasaidia kuhama kutoka Kimara kwenda Mbezi Beach na kuwahamisha watoto wao kutoka shule ya msingi Tandika Reli kwenda St Marys au ka-International school fulani huko Uganda au Kenya. Kwa hiyo kwao madaraka ni lengo sio njia. Tunahitaji chama ambacho lengo lake ni kutumia madaraka kama njia ya kuwapa watanzaia serikali safi yenye kutekeleza wajibu wake wa kiserikali na kuwapa kila nafasi na furasa kila mwananchi ya kutimiza kipaji na uwezo aliopewa na mwenye Mungu.

Madamu tunaamini kwamba CCM haijatutesa vya kutosha na kwamba ni CCM pekee yenye uwezo wa kutawala kwa sasa na kwamba huwezi kuwa kiongozi mzuri hadi upitie CCM, then tutaendelea kufungua thread za ufisadi katika JF na magazeti yetu yataendelea kujaa habari za wana CCM walivyopora hazina badala ya habari za maendeleo.

Wanasaikolojia wanaamini kwamba binadamu hupata wanachotaka na kutafuta. What goes around it is what comes around. Ufisadi na matatizo ya nchi yetu sio ya bahati mbaya. Nido nikasema kuwa Kwa kuchagua kuendelea kukaa chini ya CCM tumechagua kuendelea kuishi na ufisadi.

Bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo tukiamua. Hatua ya kwanza ni kuachana na fikra kwamba hakuna chama kingine chenye uwezo wa kutawala isipokuwa CCM. Tuachane na maneno ya rejareja kwamba wapinzani wasubiri kwanza wakomae, waingie bungeni, etc. Kama Mwalimu Nyerere angekuwa mwoga kama baadhi ya watanzania hapa asingekubali kupokea uhuru mwaka 1961 maana alikuwa na madaktari watatu nchi nzima.

Kitila,

Kinachonipa wasiwasi mimi sio hao walioko serikalini, ni hawa Watanzania ambao nakutana nao mitaani au nimekuwa nakutana nao kwa miaka mingi.

Ukiangalia na kufuatilia matendo yao kwenye uwajibikaji kwa haki na mapendo kwa nchi yao, unapata kigugumizi.

Tatizo kama lingelikuwa kwa wanasiasa tu, ingekuwa nafuu maana ingefika siku tungeweza kuwang'oa tu. Huenda tatizo letu ni kubwa zaidi ya hapo.

Angalia mabadiliko ya siasa Eastern Europe, kule kweli unajua tatizo lilikuwa mfumo mbaya pamoja na wanasiasa waliokuwa madarakani.

Angalia mabadiliko ya siasa Kenya, Malawi au Zambia. Tatizo ni wananchi karibu wote.

Lets hope kwamba kwa TZ tatizo letu ni kama la Eastern Europe na hao watakaokuja watakuwa tofauti sana na mafisadi wa CCM.
 
tuliwahi kuandika hapa kuwa watanzania wana tabia tofauti sana duniani, yaani ubinafsi, hakuna mfia nchi hapa. wengine mlishangaa kusikia wapemba wanataka kuanza kujilipua katika kutetea pemba kujitenga. anayeonekana mwanamapinduzi akitia mguu huko serikalini anabadilika ghafla, anawaza kuwa na ngawira ili asipate shida ya kuja kuomba kura. manake ukiwa na ngawira mabo yako mtelezo, utashinda kura za maoni na ukishazishinda wewe ni mtelezo tu, kugawa pilau na kanga unapata ubunge then murwaa unaibu waziri halafu nyumba marekani.

wako wapi wale watanzania kama akina jenerali ulimwengu/ yule aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya akasema hapana? akina mabere marando yule aliyeteuliwa kwenda kuuliza wanachi kama wanataka vyama vingi aksema hapana? mko wapi wana wa nchi? ambaop mtakuwa tayri kupigwa mabomu kupinga uzandiki huu wa watawala? mko wapi wana wa nchi ambao mtaweza kumwambia jk wewe ni kbaraka wa sinclair bila kumumunya maneneo? mko wapi?
ndiyo tupa hapa yunapinga kwa kuandika! ndiyo tuko hapa tunapinga kwa kusikitika! tuko hapa tunapinga kwa kukata tamaa! tuko hapa tunapinga eti kwa kushauri kukarabati ccmkama vile ccm ni msahafu fulani. tuko hapa tuanendela kulipa kodi ili akina richmond na akina downas waneemeke!

tutafakari tena, je taifa langu nimekufanyia nini?
 
Usiombe kujipenyeza nakuingia ccm maana punde utashangaa kuwa na wewe umeshakuwa fisadi. Nakwambia ufisadi wa ccm ni kama ugonjwa hatari maana hauchelewi kuambukiza.
Salama yetu ni vyama imara vya upinzani. Vyama vinavyosimamia kile vianaamini kama Chadema.
 
Kitila,

Kinachonipa wasiwasi mimi sio hao walioko serikalini, ni hawa Watanzania ambao nakutana nao mitaani au nimekuwa nakutana nao kwa miaka mingi.

Ukiangalia na kufuatilia matendo yao kwenye uwajibikaji kwa haki na mapendo kwa nchi yao, unapata kigugumizi.

Tatizo kama lingelikuwa kwa wanasiasa tu, ingekuwa nafuu maana ingefika siku tungeweza kuwang'oa tu. Huenda tatizo letu ni kubwa zaidi ya hapo.

Angalia mabadiliko ya siasa Eastern Europe, kule kweli unajua tatizo lilikuwa mfumo mbaya pamoja na wanasiasa waliokuwa madarakani.

Angalia mabadiliko ya siasa Kenya, Malawi au Zambia. Tatizo ni wananchi karibu wote.

Lets hope kwamba kwa TZ tatizo letu ni kama la Eastern Europe na hao watakaokuja watakuwa tofauti sana na mafisadi wa CCM.

Mkuu umesomeka.

Bahati nzuri wengine tumeishi katika nchi yetu kwa muda wa kutosha. Tumeishi katika mazingira ya kila aina. Na tumeishi nchi za wengine kwa muda wa kutosha pia. Unachokisema na anachokisema kitila vinafanana.

Unajua mfumo ulioko Tanzania umejengwa vizuri sana ndio maana utasikia Ufisadi TRC, TPB, BoT nk, lakini utasikia hakuna anayechukuliwa hatua. Matatizo yote, mashetani yote yametengenezwa vizuri sana. Ni mfumo wa kuwatajirisha wengine na wengine wabaki masikini.

Ndio maana utasikia leo hii kakindomaster nikiwa Mkuu wa kitengo nachukua jamaa, marafiki na kila uchafu kuanzia siku hiyo wanakuwa watawala. Nikiwa na maana tunapeana ulaji. kwa hiyo huu uchafu unatoka juu kuelekea chini. tutapiga kelele tutapiga kelele lakini kikubwa kinachotuletea matatizo ni viongozi wetu wa juu au mfumo uliojengeka ktk chama tawala. Kujua nani ni mtanzania na nani siyo mtanzania pia ni tatizo la makusudi. kuwaleta wahindi kila kukicha na kuwa watanzania zaidi za mzawa na pia ni tatizo.

katika mfumo tulionao nakumbuka zamani kuna watu walisha jitoa serikalini kama vile walivyo Jenerali, lakini baadhi ya waliojitoa walirudi wenyewe baada ya kuona hakuna msimamo wa kutosha Tanzania. Nakumbuka hili pia lilimkuta Mwandosa miaka hiyo. kwa wale wanaokumbuka kipindi cha Hassan watajua hili vizuri au kwamba kuchezewa sekta ya umeme Tanzania haijaanza leo.

Tatizo liliko Tanzania la kupindisha sheria ambalo linaonekana mpaka katika ngazi za chini limetengenezwa na watawala kwa manufaa yao binafsi. Na ndio maana hata sheria pale zinapopinda wanaishia kusema ni ajari ya kisiasa. ikiwa na maana walikuwa wanatufeki hila sasa wamegundulika.

katika nchi kama Tanzania tuzungumze tufanye nini hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote kama tutaamini katika ujanja ujanja. Maendeleo tutayasikia ktk nchi nyingine wakati tukiendelea kujisifu kuwa na amani na utulivu wakati wananchi wa kawaida wakilala njaa.

Suluhisho la haya matatizo ni kuwaonyesha watawala kwamba kama hawatakuwa tayari kujua watanzania wanajua madhambi yao wajue wamekwisha. Si vizuri kusema hila lakini lazima niseme bila kutoa CCM madarakani tumekwisha. Baadhi watafikiria kakindomaster ni mpinzani anachuki na chama tawala lakini mimi nilipewa kadi ya CCM mwaka 1990 wakati namaliza kidato cha nne sijawahi kujiunga na chama kingine chochote cha siasa mpaka sasa.

Bila kuondoa CCM na mfumo wake hili mabaya yake yafe na chama tawala tutakufa sisi. inatakiwa tuige vizuri wakenya waliohakikisha kanu inakufa na haitakaa ifufuke tena.
 
Usiombe kujipenyeza nakuingia ccm maana punde utashangaa kuwa na wewe umeshakuwa fisadi. Nakwambia ufisadi wa ccm ni kama ugonjwa hatari maana hauchelewi kuambukiza.
Salama yetu ni vyama imara vya upinzani. Vyama vinavyosimamia kile vianaamini kama Chadema.

Huko sisiemu kuna mamr and ms misifa! ukifanya ufisadi mkubwa ndio unaonekana, mjanja, jasiri, mtoto wa mjini, msomi, n.k. Ukiwa msafi hata rafiki utakosa. Na misifa ndio inawafanya watu wanafanya ufisadi wa kupindukia, utasikia jamaa bwana anaendesha gari ya millioni 500, nyumba yake millioni 600 anaonekana wa maana na watu kuanza kujikomba bila kuuliza hizo pesa kazipataje. This has to end jamani, but the main question remains, how to end it kama bado vijijini wanawapigia makofi mafisadi?
 
Nchi haijauzwa, kilichotokea hapa ni utendaji kazi wa kawaida na muafaka kabisa. Kosa lililojitokeza ni la bw. Sinclair kuropoka hadharani kuwa ameona nyaraka, lakini msidhani kuwa nyaraka za siri maana yake haziruhusiwi kuonwa na mtu yeyote.Nyaraka za siri zinaonwa na wadau husika.

Bw. Sinclair ni mdau katika sekta ya madini. Kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho ya mapendekezo ya kamati na kabla ya kukihusisha chombo kikubwa kama Bunge basi ilikuwa ni jambo muafaka na la busara sana kwa Rais kuwahisisha pia hao wawekezaji wanaojadiliwa, ili aweze kupata picha ya matokeo ya maamuzi yoyote atakayofanya.
 
Wa kujilaumu ni sisi wenyewe, si akina Sinclair kama alivyosema mjumbe hapo juu. Wakati kila kona ya dunia wananchi wanahakikisha wanachagua the best sons and daughters to run their countries, sisi tumeamua kuchagua watu wenye ujuzi wa ujanjaujanja na uswahili ambao sasa akina Sinclair ndio wamewaweka mfukoni. Tusikate tamaa, tuendelee kupiganisha fikra, ipo siku kitaeleweka.

Who are they?
Is there any method of identifying them?
 
Swali mihimu la kujiuliza ni kuwa huyu Sinclair ameipata wapi hii ripoti ? Kwani kwa jinsi ninavyojua mimi Ripoti hii kwa sasa hiko mikononi kwa Rais , jee ni Rais aliyempatia huyu bwana kopi kabla ya kuwa released to the public ? Na kama ni hivyo jee Sinclair ana cheo gani katika serikali ya Kikwete?
 
Tunao sana watu Mtanzania. Mama wa matatizo ya uongozi wa nchi yetu ni kuendelea kuamini kwamba ni CCM pekee yenye watu wanaofaa kuwa viongozi. Hili la kuendelea kuamini kwamba ni CCM tu ndiyo yenye uwezo wa kutawala sasa limezalisha matatizo mengine matatu ya hatari kabisa.

Sawa sawa, lakini wakulaumiwa sio CCM kwa haya, ila ni sisi wananchi wenyewe na pia viongozi vyama vya upinzani kwa kutotupa sababu nzito za sisi wananchi kutowapigia CCM.
 
Wanasaikolojia wanaamini kwamba binadamu hupata wanachotaka na kutafuta. What goes around it is what comes around. Ufisadi na matatizo ya nchi yetu sio ya bahati mbaya. Nido nikasema kuwa Kwa kuchagua kuendelea kukaa chini ya CCM tumechagua kuendelea kuishi na ufisadi.

Bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo tukiamua. Hatua ya kwanza ni kuachana na fikra kwamba hakuna chama kingine chenye uwezo wa kutawala isipokuwa CCM. Tuachane na maneno ya rejareja kwamba wapinzani wasubiri kwanza wakomae, waingie bungeni, etc. Kama Mwalimu Nyerere angekuwa mwoga kama baadhi ya watanzania hapa asingekubali kupokea uhuru mwaka 1961 maana alikuwa na madaktari watatu nchi nzima.

Na kama vijana wakiwa waoga kuinyoosha CCM basi wanaoipindisha wataendelea kufurahika.
 
.

Bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo tukiamua. Hatua ya kwanza ni kuachana na fikra kwamba hakuna chama kingine chenye uwezo wa kutawala isipokuwa CCM. Tuachane na maneno ya rejareja kwamba wapinzani wasubiri kwanza wakomae, waingie bungeni, etc. Kama Mwalimu Nyerere angekuwa mwoga kama baadhi ya watanzania hapa asingekubali kupokea uhuru mwaka 1961 maana alikuwa na madaktari watatu nchi nzima.

Huu ndio uhalisia wa mambo hivi sasa, with exception of Zanzibar, Chama hicho HAKIPO.Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka mabadiliko ya kweli ana choice tatu: moja ni kuanzisha hicho chama madhubuti, pili ni kuingia kwenye harakati za kuimarisha vyama vya upinzani vilivyopo na tatu ni kuingia kwenye harakati za kuboresha maadili ndani ya CCM.
 
Kitila,

Kinachonipa wasiwasi mimi sio hao walioko serikalini, ni hawa Watanzania ambao nakutana nao mitaani au nimekuwa nakutana nao kwa miaka mingi.

Ukiangalia na kufuatilia matendo yao kwenye uwajibikaji kwa haki na mapendo kwa nchi yao, unapata kigugumizi.

Tatizo kama lingelikuwa kwa wanasiasa tu, ingekuwa nafuu maana ingefika siku tungeweza kuwang'oa tu. Huenda tatizo letu ni kubwa zaidi ya hapo.

Angalia mabadiliko ya siasa Eastern Europe, kule kweli unajua tatizo lilikuwa mfumo mbaya pamoja na wanasiasa waliokuwa madarakani.

Angalia mabadiliko ya siasa Kenya, Malawi au Zambia. Tatizo ni wananchi karibu wote.

Lets hope kwamba kwa TZ tatizo letu ni kama la Eastern Europe na hao watakaokuja watakuwa tofauti sana na mafisadi wa CCM.


I don't like those statements one bit (statements in RED).
Natamani uchapwe viboko!


.
 
Huu ndio uhalisia wa mambo hivi sasa, with exception of Zanzibar, Chama hicho HAKIPO.Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka mabadiliko ya kweli ana choice tatu: moja ni kuanzisha hicho chama madhubuti, pili ni kuingia kwenye harakati za kuimarisha vyama vya upinzani vilivyopo na tatu ni kuingia kwenye harakati za kuboresha maadili ndani ya CCM.


Hiyo option ya tatu ina mshikeli; ni kukubali yaishe au kuamua kuungana nao! Chama mbadala kipo labda kama hutaki kuangalia. Atazamaye huona na anayebisha hodi hufunguliwa, amen.
 
Tanzania tuna kazi!!
Kama watu wazima wenyewe ndio siye????
Na uwezo wetu ndio huu!!
Basi inabidi tukaze buti kweli kweli,
 
Hiyo option ya tatu ina mshikeli; ni kukubali yaishe au kuamua kuungana nao! Chama mbadala kipo labda kama hutaki kuangalia. Atazamaye huona na anayebisha hodi hufunguliwa, amen.

Unajua Kitila mimi siku zote huwa nashindwa kuwaelewa watu wanaokubali kushindwa kudeal na wabinafsi wachache walio ndani ya CCM halafu at the same time wanaomba jukumu la kudeal na wabinafsi wa nchi nzima. Vyama mbadala wabinafsi wake watadhihirika wakishapewa rungu, sasa hivi true colour yao haiwezi kuonekana.
Chama mbadala unachokizungumzia hapo juu I hope is not CHADEMA.
 
Wadau kama nchi imeuzwa, tumashaonyeshwa risiti? maana mie sijaiona bado. kama wameiuza basi ole wao wawe wameiuza bila ya faida, tutashikana mashati. Ni wazalendo ndio walioitolea jasho kuipalilia, kuiwekea vikorombwezo vyote vilivyowavutia wanunuaji, sasa na hiyo faida igawanywe kwa haki basi, mtaji ubaki ili tujue tunaenda kununua ardhi sehemu gani nyingine, tuiite jina gani sijui...Maana nina imani hata hati miliki za jina Tanzania pia zilikuwemo kwenye mkataba wa mauzo.....
 
Mbunge: Nchi imeuzwa

na Martin Malera - T/Taida

MJADALA wa hotuba ya bajeti ya 2008/09 unazidi kuchukua sura mpya kila siku, huku wabunge wakiendelea kutoa kauli kali dhidi ya serikali.

Katika hatua ambayo inaweza kushtua, Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu, naye ameungana na watu wanaoikosoa wazi wazi serikali kwa kusema kuwa viongozi wameiuza nchi bila sababu na hivi sasa wananchi wana hasira dhidi ya viongozi hao.

Nyarandu alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa hotuba hiyo ya bajeti.

“Naomba nimalizie kwa kuangalia kwa nini watu wana hasira. Tumeuza hii nchi bila sababu, tuliiuza Air Tanzania, baadaye tukairudisha, wale Waafrika Kusini wakaja wakaua mpaka karakana ile ya Dar es Salaam, tukauza nyumba za pilots (marubani) na kila kitu.

‘‘Lazima tukubali kuwa, hilo lilikuwa kosa na sasa tujielekeze kuifanya Air Tanzania iifanye Tanzania proudly (kwa sifa).

‘‘Tulikwenda tukauza hoteli zile za THIA na yule mwekezaji alipewa sh milioni 3.5, zile hoteli za THIA kwenye mbuga za wanyama ni prime areas (maeneo mazuri), baadaye akarudi aka-negotiate (akajadiliana) akalipa dola za Kimarekani 1.5, hajawekeza hata mfuko mmoja wa simenti mpaka kesho,” alisema Nyarandu.

Huku akisikilizwa kwa makini na utulivu mkubwa na wabunge wengi, Nyarandu alisema anatarajia kuja na muswada binafsi kuitaka serikali izirejeshe hoteli hizo na zipelekwe upya sokoni.

‘‘Nafikiri nitakuja na muswada binafsi kuitaka serikali ibinafsishe hizo hoteli na zipelekwe upya kwenye soko, ni lazima tufanye U-turn (tugeuke) katika mambo ambayo yanawezekana. Mradi wa IPTL ulikuwa ni mradi mbaya, hautusaidii, ni lazima serikali ifikirie kuununua. Tutaendelea kuwa na mambo mengi ambayo hayatusaidii,” alisisitiza.

Mbunge huyo aliwataka viongozi wanaoingia mikataba na wawekezaji wa nje kwa niaba ya Watanzania, siku zijazo wafahamu kwamba wanafanya kazi ambayo vizazi vyote vitawatazama walifanya nini kwa ajili ya Tanzania, ili nchi isipate hasara tena katika makubaliano yajayo.

Alisema nchi isiyowajali watu wake, haiwezi kufika mbali na ni wajibu wa kila kiongozi kuhakikisha kwamba malalamiko ya dhati yanayotokea anayaona.

Alisema ana mifano mingi ya Wazungu waliokuja Tanzania na kubeba briefcase (mikoba) zenye makaratasi tu ndani, lakini walipoingia nchini walikopeshwa fedha na benki zetu na kuingia katika biashara ya utalii kwa kununua gari moja la kupeleka wageni Ngorongoro na Serengeti, lakini sasa hivi ni mamilionea.

‘‘Mheshimiwa mwenyekiti, hao hao waliokuja na briefcase wamekwenda wakapewa maeneo mbalimbali ya uwekezaji wakati mwananchi wa kawaida hakupewa, mwekezaji wa ndani hakupewa,” alisema.

Kwa mujibu wa Nyarandu, Tanzania si maskini, lakini baadhi ya viongozi wakisikia bajeti imepitishwa, wanajiandaa na kufanya semina na makongamano ya kupunguza umaskini yasiyo na tija, badala ya kujikita katika utendaji kazi wa bidii kuongeza utajiri.

‘‘Mbele ya safari na huko tunakokwenda tuna mambo mawili ambayo lazima tuyaweke sawa, ni lazima tuwaambie Watanzania ukweli na ukweli ndiyo huu kwamba siku zijazo, mwaka huu na mwaka ujao na kadhalika, nchi lazima ijiandae kupambana na uwezekano wa ugumu wa maisha unaotokana na mambo ambayo yako nje ya uwezo wa sisi kama Serikali ya Tanzania.

‘‘Kupanda kwa bei ya mafuta hakutegemei kupungua, lakini tatizo kubwa la chakula duniani litaendelea kupanda, wameeleza ndugu zangu wengine wengi sana,” alisema.

‘‘Nilikuwa na interest (nia) ya kuangalia hivi karibuni research (utafiti) moja inaitwa happiness index (faharisi ya furaha) duniani. Kwamba katika kila nchi duniani siku hizi wanapima watu wa nchi fulani wana furaha kiasi gani na nchi gani ina furaha kuliko nyingine.

‘‘Kwa wastani na katika huo utafiti, wanaonyesha kwamba watu wa Denmark wameonekana ndio wananchi wenye furaha kuliko wote duniani na wa mwisho kabisa ni ndugu zetu wa Zimbabwe. Bila shaka tunaelewa kilichowapata na tunawapa pole sana.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, siku hizi kuna hili jambo la wananchi wenye hasira. Sehemu nyingi sana ukienda Kariakoo wanasema akikusingizia mtu kwamba wewe ni mwizi, umekufa, kwa sababu kinachotokea ni kwamba mtu anachukua jiwe, chochote alichonacho anakupiga, baadaye ndiyo anasema oooh, ilikuwa makosa, lakini wakati huo tayari umevunjika mguu au umekufa na hili tatizo la wananchi wenye hasira limeendelea kuongezeka kutoka miji mikubwa hadi miji midogo,” alisema.

Alisema ili kupunguza wimbi la hasira za wananchi, kuna mambo mawili ambayo serikali inapaswa kufanya, nayo ni kusimamia haki na wajibu.

Mbunge huyo kijana alisema ni wajibu wa serikali kuwaambia wananchi kila kitu inachofanya, huku ikisimamia haki ya kila mwananchi bila ubaguzi.

‘‘Mfano mzuri ambao nauangalia kila siku katika safari zangu, hauhitaji hata fedha, mwananchi anaondoka na mihogo yake Morogoro anapeleka Dar es Salaam, yuko kwenye Fuso, anaweza kusimamishwa na hivi vizuizi vya Polisi mara kumi.

Mwananchi aliyetoka Mwanza, minofu ya samaki au dagaa, mpaka atakapofikisha hao dagaa Dar es Salaam atakuwa amesimamishwa zaidi ya mara 25, na wakati mwingine mtu anasimamishwa, lakini baada ya kilomita kumi tu anasimamishwa tena, bila kujua kwamba tunasimamisha kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa hili,” alisema.

Naye Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja, alisema ili kuondokana na umaskini, serikali lazima iwekeze katika kilimo.

“Lazima tuwekeze katika kilimo na katika hili sote tunakubaliana, anayekataa ni nani? Kwa nini serikali isikubali sasa kukaa na kutazama suala hili upya na kutuwekea utaratibu utakaohakikisha kwamba tunatekeleza? “Tumezungumza juu ya benki ya kilimo, inaelekea tunakaribia kuelewana. Tumezungumza juu ya bodi ya mazao mchanganyiko, sina hakika tumefikia wapi. Lakini ni lazima tuwekeze katika sekta hii na tukiwekeza katika sekta hii ndipo wananchi wetu watakapopata unafuu na kuondokana na umaskini uliokithiri,” alisema.

Alisema ili taifa liwe na maaendeleo, lazima matatizo ya msingi kama ya umeme yapatiwe ufumbuzi wa kudumu na kuachana na mitambo aina ya Kampuni ya Richmond, aliyodai ina nguruma na kusababisha joto bila kuzalisha umeme.

‘‘Tuna vyanzo vya umeme ambavyo ni vya uhakika kama Stigler’s Gorge kwenye Mto Rufiji, tukakope tujenge, halafu tukishajenga tutapata umeme, tutajenga hivyo viwanda vya mbolea na vya kila kitu, ili kuweza kuinua uchumi huu, vinginevyo tutaendelea kutamani kuendelea lakini tutabaki tumekwama hapa hapa tulipo,” alisema Keenja ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Kilimo.

Alisema serikali ipo mahala pagumu kwa sababu haijafanya maamuzi ya msingi ya kuwapeleka Watanzania mahali laini. Alibainisha kuwa nchi ina rasilimali za kila namna, lakini wananchi hawajawezeshwa kuzitumia rasilimali hizo.

“Ukienda Morogoro pale kuna mito mia moja sabini na sita isiyokauka mwaka mzima. Ukienda Kigoma usiseme wana mito mikubwa yenye maji yasiyokauka. Sasa tuwezeshe hii mikoa izalishe na tuwekeze kwa makusudi kabisa ili kuiwezesha izalishe,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA) alisema serikali ilipaswa kufanya bajeti ya kitu chenye uwezo nacho.

‘‘Natoa mfano, simple economics tu, nyumbani kwako, unamwambia mkeo kesho nenda kanunue kitoweo, kanunue hiki na hiki, unampa sh 5,000. Bei ya soko kesho yake sh 5,000, haifai na wala hawezi kununua hata vitunguu. Sasa bajeti tunafanya na hali ya dunia iko kwenye hali ya hatari, hasa kufuatana na mfumuko wa bei ya petroli na chakula, ambacho hakipo duniani, kwa hiyo bajeti hii tunavyoizungumza tuwe makini, tuelewe tunaizungumzia bajeti ambayo hatuna uhakika nayo kama itatufikisha hata miezi miwili,” alisema.

Kuhusu kilimo, Ndesamburo alisema ili kilimo kiwe na tija na kichangie pato kubwa la taifa, si kila Mtanzania anaweza kuwa mkulima bali kuwe na watu maalumu wa kufanya kilimo cha kisasa.

Ndesamburo alisema Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inapaswa kubuni vyanzo vipya vya kodi na si kuongeza kodi kwenye bidhaa zile zile, na kutolea mfano wa kodi za bia na sigara kwamba hazikustahili kuongezwa, kwani inachochea unywaji wa gongo kwa kasi mpya.

Naye Mbunge wa Bahi, William Kusilla (CCM), alisema zana za kilimo ndilo tatizo linaloathiri kilimo nchini.

‘‘Kwenye miaka ya 70, tulifika mahali nchi hii tulikuwa na matrekta 18,000 nchini kwa mwaka mmoja. Sasa mwaka 2007 tuna matrekta 7,200, sasa tunakwenda mbele au tunarudi nyuma? Matrekta 7,200 nchi nzima, hivi unategemea kilimo kiweze kuendelea katika kasi hii?” alihoji na kuitaka serikali kuonyesha nia ya dhati ya kuendeleza kilimo.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe, aliitaka serikali kuanzisha tena Benki ya Wakulima ili ikopeshe vifaa vya kilimo.

‘‘Mkulima tunayesema mkulima enzi zile za nyuma miaka ya 80 na 90, wakulima walikuwa wana thamani, unamkuta mkulima ana ekari 100 ana trekta ambalo CRDB wakati huo ikiwa ni Rural Bank amekopeshwa, analima, anapata mazao mengi. Akiitwa mkulima alikuwa mkulima kwelikweli na unajua kabisa huyu kweli ni mkulima na ulikuwa ukisema unapelekwa kwa mkulima, kweli ni mkulima, lakini mkulima wa sasa hivi ni maskini,” alisema.





Maoni ya Wasomaji

Hongera Mheshimiwa Nyarandu kwa maono yako kuhusu mwenendo wa Serikali yetu hasa kuhusu uchumi unaofaidisha watu wachache serikalini huku mwananchi wa kawaida akiachwa hoi bin taaban. Huu ni mwanzo mwma na pia ni ishara nzuri kuigwa na wabunge wa CCM ambao hawataki kuikosoa serikali yao.

Rai yangu kwa wananchi ni kwamba uchaguzi ujao tuchague vijana wengi katika ngazi za udiwani na ubunge kwani vijana wameonekana kuwa 'socital centred'kuliko wazee hasa wale wa CCM. Mfano chukulia wabunge kama Kabwe, Nyarandu,Wanwe,Slaa, nk. ni mwiba kwa serikali hasa pale inapolala usingizi.

Wakati ndo huu tubadilike, tuamke, tukomboe nchi yetu toka mikononi mwa mafisadi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

na Jafari, B, Toronto, Canada. - 19.06.08

Tunaiweka nchi kwenye maombi hasa viongozi wetu kwani wanadhamini sana zawadi wanapewa na wawekezaji na wanaweza kuiuza nchi kwa sababu ya hizo zawadi.Tunaamini kila chenye mwanzo kinamwisho.Mungu ibariki Tanzania.

na Amina, uk, - 19.06.08
Tanzania kweli inauzwa kwa wageni wanotoa vijisenti. Huko ZnZ eneo la zaidi ya eka 220 na Ufukwe zaidi ya kilomita 3 Muyuni, wamepewa warabu wa UAE bure kujenga hoteli za wageni. Watajenga nyumba na kuziuza kwa wageni na kupata faida kemkem. Kaulize ardhi ya bure Mauritius au Seychelles, watu watakucheka. Walalahoi walie tu. Ardhi iliotaifishwa wakati wa Mapinduzi leo wanarejeshewa mabepari ili wapate kustarehe, na wenyeji watabakia watwana (maboi) kutumikia mabwana. Kila tukiimba CCM hoyee, warabu matajiri wanachekea ******. Poleni kwa ujinga.
na Issa Macho., Ughaibuni., - 19.06.08


Hongera sana Mh. Nyalandu angalau umesema kweli sijui itashughulikiwa.

Kwa kweli la Muhimu zaidi kilimo. Kwa kweli hata serikali ikinunua matrekta elfu moja na nakuyagawa kwa mkoa ya Rukwa Mbeya na Ruvuma, Kigoma na Kagera kwenye rutuba na mito mingi kisha mwaka unaofuata ya Mikoa ya Morogoro Tanga Arusha na Kilimanjaro na pia kujaribu kusaidia wakulima hasa kwa kuwapa mbegu na mbolea zenye bei nafuu kabisa kwa miaka hii mitatu iliyobaki kutakuwa hakuna haja ya kampeni kubwa CCM kwani mwaka wa tatu Mwanza Shinyanga na Tabora yangu kweli angalua yale mashamba ya mpunga yatalimwa vizuri. Ni vizuri hata kawasaoma kwenye internet jinsi ya kutumia tractor ndogo sana zipo kwa wingi thailanda na Vietnan kwa kweli zina lima vizuri na kuvuna vizuri hasa mpunga naelewa Tanzania sasa maeneo mengi unaweza kupanda mpunga na mahindi tuachane na umasikini wa chakula ili tuweze kufikiria elimu na tecknologia ya kisasa. Tuache Uchawi mambo ya kijingajinga yanachosha hayo.

Ndugu wabunge jamani kweli mpaka lini Taifa letu lipata benki za kweli sio kukopesha wafanyabiashara wa kariakoo kujenga Magorofa Marefu na kutoza kodi kubwa ili kulipa mikopo sasa iwe hivi nayewekeza kwenye kilimo cha chakula apewe kipaumbele kabisa hata ikiwezekana apewe eneo la kulima Handeni,Morogoro kwani mbona watu wa madini wao wanakumbatiwa mpaka Ikulu hebu tujaribu sasa kufanya kweli wakiingiza machine za kilimo iwe mojakwamoja bure kabisa mradi ziwenamanufaa kwa kilimo cha kweli na kieleweke.

Mbona tutafungua soko la Afrika la Chakula hapa nyumbani wao Zimbambwe walifika huko lakini kwa sababu ya Siasa Chafu na ubabe wa kijingajinga ndio hao sasa ndio watu wasiona furaha kuliko wote dunia.

jamani tusifike huko kabisa kwani kukiwepo chakula hata watoto wa mtaani watapungua na pia mahudhurio mashule yatakuwa na taifa litaendelea
na linambasha, Hongkong, - 19.06.08

Mh. Nyalandu wasilisha huu mswaada haraka kweni nyingine zinatia masikitiko kwani zilijengwa kwa fedha nyingi tunabaki hatuna kazi na hakuna chochote cha maana kilichofanyika
na linambasha, Hongkong, - 19.06.08

Mmmh,ngoja nifikirie kwanza.

na katochi, Tanzania, - 19.06.08

nadanganya tuu maoni yangu hayana ukweli wowote na wal hayatoki moyoni,kwanza mimi siko HOngkong ya far east niko manzeseeeee kwa mfuga mmmmmmmmmm.CCM hoye

na linambasha, Hongkong, - 19.06.08

Hongera sana Mh. Nyarandu. Nadhani tukiwa na Wabunge 50 kama wewe nchi itakwenda. Ni kweli kwamba viongozi wetu wa Serikali wamejaa tamaa ya kujilimbikizia mali. Hawana nia njema na nchi yetu hata kidogo. Jaribu kufikiria mikataba feki mingapi iliyosainiwa kwa manufaa ya wachache?...IPTL, Buzwagi,Kiwira, Meremeta, Richmond, RADA, Songas etc
Mipango yote ni feki..haiko kwa ajili ya kumkomboa Mtanzania bali matumbo ya wachache. Nchi (TZ) si masikini hata kidogo. Hali hii inasababishwa na wachache tuliowapa mamlaka! Jaribu kuangalia sera ya uwekezaji ilivyo jaa utumbo!!!! Kwa nini pawepo na grace period? Sera na mazingira nyenyekevu ya uwekezaji tuliyojenga yanatoa mwanya kwa baadhi ya makampuni kubalisha majina kila kukicha kwa jinsi wananvyotaka.

Kwa mtazamo wangu MATATIZO ya Nchi hii ni matokeo ya UDHAIFU wa viongozi kuanzia Rais hadi wasaidizi wake. Kama viongozi wangekuwa na nia ya kutumia rasilimali zetu kwa umakini na kwa manufaa ya Taifa; Nchi hii ingesonga mbele. Tuchukue mfano mdogo kwa nchi kama Botswana na Namibia zinapiga hatua kiuchumi na kijamii ni kwa sababu ya nia ya dhati ya viongozi kukomboa wananchi wao kwa kutumia vizuri rasilimali zao.

Ukoloni huu wa sasa unaletwa na viongozi wetu. Wawekezaji wanabebwa na viongozi----RUSHWA.

Utendaji kazi katika ofisi nyingi za serikali ni kujuana na uzoefu si kwa kuzingatia utaalamu na ufanisi.Tumekosa viongozi waadilifu wenye uchungu na hali ngumu ya maisha ya Watanzania. Fuatilia suala la UFISADI linavyoshughulikiwa kisiasa! pasipo kujali maslahi ya Taifa.Akina Nyarandu na wenzako (Annie Kilango, Aloyce Kimaro, Dk.Slaa, Zitto Kabwe, Dk. Mwakyembe, Mh. Lucy nk) tupo nyuma yenu. Hata kama tupo ICU tunafarijika sana jinsi mnavyojitahidi kupambana na uozo huu serikalini. Tuna IMANI kubwa juu yenu, kwamba yanawezekana na umefika wakati wa kutanguliza MASLAHI ya TAIFA badala ya kung'ang'ania maslahi ya chama fulani au kundi fulani la watu wachahche huku waliowengi wakiendelea kuteseka.

Ninatoa wito kwa Watanzania wenzangu, tuache ushabiki katika kutetea maslahi ya WATANZANIA, Nchi hii ni yetu sote. Tuamke sasa wakati umefika. Tusimame imara kwa maslahi ya nchi. Jumuiya za Dini, makundi mbalimbali (NGOs, Civil Societies) yawe active kutetea huu udhalimu unaoendelea nchini kwetu. Tuache kufanya kazi kwa undugu undugu na kufahamiana hatuta fika kamwe.Tusitarajie mtu au taifa fulani la nje litatusaidia kutatua kwa dhati matatizo yetu....Umasikini na matatizo mengine yanayotukabiri yataondoka kwa kwa nguvu zetu weneyewe si kwa misaada kutoka nje inayoambatana na masharti ya KIFISADI. Kumbuka, kwa kiasi kikubwa misaada hii ndiyo inayochangia kuongezeka kwa umasikini na madeni kwa nchi masikini kama Tanzania. Isitoshe misaada mingi huishia mifukoni mwa wachache!

Kikwete Nchi imekwenda mrama sera zako zote zimeoza....hakuna dalili ya MAISHA BORA kwa kila mtanzania; Tulichoshuhudia ni Kasi, Nguvu, na Ari Mpya ya UFISADI.Hatima ya Mtanzania BADO ni tete! Utendaji kazi wa Serikali yako ni MBOVU sana tena ni kinyaa! Mfano umeshindwa kulishughulikia suala nyeti la ufisadi!na kuongeza tija na ufanisi serikalini..angalia Bandari ya DSM inavyofanya kazi!

WANANCHI TUAMKE: TUKEMEE KWA KAULI MOJA. HAKUNA JESHI DUNIANI LENYE NGUVU KUSHINDA NGUVU YA UMMA (POPULAR POWER). Kiza ni kinene, nyika ni kubwa sana na tumezungukwa na wanyama wakali wa kila aina. SAFARI NI NDEFU JAPO YANAWEZEKANA


na Donald , Australia, - 19.06.08

Ahsante sana Nyarandu, hayo uliyoyasema ni ya kweli nami niongezee kidogo kwenye kipengele chako kisemacho:

Ili kupunguza wimbi la hasira za wananchi, kuna mambo ambayo serikali inapaswa kufanya, nayo ni kusimamia haki na wajibu. Vituo vyetu vya polisi havitutendei haki wananchi hata kidogo, mfano pale kituo cha polisi cha kirumba mwanza vibaka na majambazi wanapofikishwa huamini kabisa watatoka kwa kuwa OCD ni swahiba wao! Fika mitaa ya Kilimahewa, mkudi, mji mwema, watu hawalali kwa kuwa mama Matola amekuwa akiwaacha vibaka pindi wanapofikishwa kituoni hapo kwa kupata kitu kidogo, haki na wajibu wake kama mkuu wa kituo uko wapi? Jibu ni kwenye pesa.

na Johari, Mza, - 19.06.08

CCM HOYEEEEEEEE

na katochi, Tanania, - 19.06.08

Naamini muda wa mabadiliko umewadia. Na katika hali kama hii utagundua kutokana na jinsi mambo yanavyokwenda. Mfano sahihi wa mabadiliko ya kweli kimaisha unaweza kuungalia katika mazingira ya familia. Ikitokea familia inamtegemea mmoja wao karibu kwa kila kitu, na inatokea hakuna jitihada za mwamko wa hawa tegemezi kuonyesha dalili za kujiimarisha ili waweze angalau kupunguza utegemezi walionao, na ama huyo anayetegemewa haonyeshi nia ya dhati ya kuondoa au kupunguza hali hiyo, mara nyingi familia za namna hiyo huwa na maisha ya kuganga njaa zaidi kwa kumuachia mmoja wao kuwa na sauti isiyokuwa na kikwazo hata kama itakuwa na walakini katika familia.

Yote hiyo ni kwa sababu yeye ndio huangaliwa atatoa wazo gani atakaloweza kulishughulikia hata kama litakuwa na gharama au madhara makubwa zaidi ya wazo linaloweza kutolewa na wanafamilia wenzake ili mradi isionekane wazo hili hakulitoa yeye na wakati yeye ndio mwenye uwezo wa kufanikisha. Ikitokea kikwazo cha kupinga lile analopendekeza, atawasusia ili awaone jinsi mtakavyoweza kutekeleza. Cha ajabu zaidi muda wa mabadiliko unapowadia hujikuta muhusika akipingwa waziwazi tena na watoto wake ambao hujitoa mhanga kuona familia inapata mabadiliko yanayohitajika kwa wakati.

Ni wakati huu ndio hutokea vitisho vya mpaka kutolewa radhi au kutengwa nae. kwa wale wenye moyo mwepesi huogopa na kuacha harakati zao. Na wale waliojaliwa moyo wa kutenganisha uongo na ukweli hujitoa moja kwa moja pasipo kuangalia athari za hasira za huyo anayempinga. wakati huohuo ukiangalia familia ambayo maamuzi ya jambo hushghulikiwa kwa kuwajumuisha wanafamilia au hakuna utegemezi wa mtu mmoja ndani ya familia, utaona familia za namna hii zikiwa na maisha bora zaidi ya hizo zingine. Yote hii ni kwa sababu hakuna wa kumnyenyekea mwenzake zaidi ya kutunziana heshima. hawa pia huenda mpaka kufikia hapo nao walipitia katika za kupambana na magugu maji. Kwa taifa letu kama TANZANIA hali yake ya kimaisha ni kama ile ya familia tegemezi.

CCM imejitangaza kama mhimili wa mawazo na utekelezaji wa jambo lolote linalotakiwa kufanywa nchini mwetu bila kujali mawazo ya wanafamilia wengine (watanzania)wasio CCM. Hii inatufanya tuwe na maisha ya kuganga njaa tofauti na wenzetu wanaojitahidi maamuzi ya nchi na utekelezaji wake yawe na mchango wa wadau mbalimbali. Muda wa mabadiliko uliowadia ni huu unaoonekana sasa wa watoto wa CCM wenyewe kuona mzazi wao anachokifanya sasa kinaelekea kuwadhuru hata wao wenyewe kama si huruma ya kweli waliyonayo kwa watanzania wengine. wameamua kubadilisha upepo kwa lazima bila kujali athari zitakazowakuta mbeleni za eidha kufukuzwa au kunyimwa nafasi wanazoshikilia kwa sasa. Kwa mawazo ya Mh, Nyarandu ni moja ya harakati za watoto wapenda mabadiliko katika familia waliodhamiria kuubadili upepo kwa gharama yeyote itakayowakuta.

Wito kwa watanzania ni kuwa sasa tunapata nguvu kutoka ndani ya watoto wa Bw mkuu CCM, tuitumie nafasi hii kumshinikiza afanye kile tunachokitaka. Sumu ya kwanza kwake ni kumshinikiza abadili katiba na pili akubali asikubali kuwe kuna mgombea binafsi ili tuone hao wanajitokeza kumkosoa atawahukumu vipi wakati wanapendwa na wananchi wa majimbo wanayoyashikilia. Akumbuke ya kuwa siku zote kauli ya busara yenye vitendo ndio dawa ya kumteka mwenzako utakavyo. ukileta ujanja wa mitaani kama anaofanya Makamba na Mzee aliyepoteza Mboni ya Uungwana ni vitendo Nd Kingunge jua utayamaliza maisha kwa aibu.

Ee Mungu tunakuomba uendelee kumjalia afya njema Rais wetu ambaye kimsingi kuwepo kwake madarakani mpaka sasa ni kutokana na upendo wa watanzania kwake ingawaje yeye anajaribu kuwakwepa kama si wenzake waliozoeana na aliowaahidi kula, kucheza na kulala nao pamoja wakati wote wa maisha yake ya uongozi, tunakuomba pia uendelee kuwajalia watanzania moyo mshupavu wa mapambano ya kulikomboa taifa lao kutoka kwa vibaraka wa matumbo ambayo kamwe hayaishi shukrani.

na ElianGz, TANZANIA, - 19.06.08

Kuna kila sababu ya kuwapongeza wabunge wanaojali maslahi ya taifa na kuwajali wananchi bila ya kutizama itikadi zao za kisiasa. Ni vema wabunge wakafahamu kuwa, ukweli wao na kuwazi wao ndio utakaowafanya wananchi wawafuate popote walipo, bila ya kujali ni chama gani.

Tumchukue huyu mbunge kijana, Mh. Nyanda, aalivyothubutu kuongelea jambo ambalo takriban miaka minne hakuna mbunge aliyeliongelea. Ubinafsishaji usio wa maslaha kwa taifa. Hivi kweli mahoteli haya manne, yamenunuliwa kwa thamani gani? Hivi waliyoyauza, PSRC na wengine, walijali maslahi ya taifa na wanaichi au walikuwa wanakamilisha uuzaji wa idadi ya mashirika waliyotakiwa kuuza kabla ya muda wao kuisha? Hebu waheshimiwa wabunge warudi nyuma, Lake Manyara iliuzwa kwa thamani gani, Ngorongoro Wildlife loge, Seronera na lobo nazo je?

Ni yapi masharti ya uuzaji. Yametekelezwa kwa kipindi kilichotakiwa? Kama la, sababu zilizotolewa zilikuwa ni za msingi? Hivi hawakuwepo wanunuzi wengine waliokuwa na malengo mazuri kwa taifa kuliko huyo aliyepewa? Ni sababu zipi zilizofanya wasipewe? Ni uwezo wa kuziendesha, mtaji, menejiment, au ni rushwa? Je sera ya kuongeza na kuboresha ajira ya wafanyakazi wa kizalendo imetimizwa? Je wapo watanzania walioandaliwa kuchukuwa ajira za wageni ambao tayari wengine wamefanya kazi kwa takriban miaka minne na mengineyo.

Wazalendo waliopo hawana uwezo wa kufanya hizo kazi zinazoshikwa na wageni? Wabunge pia watazame kwa m iaka hii minne mwekezaji amezalisha kiasi gani na amewekeza kiasi gani. Je wabia wa utalii, tour operators wanatendewa haki au wananyonywa na kudhalilishwa? Je wafanyakazi wanalipwa kulingana na jasho lao n.k

Endapo tathimini ya kina itafanyika, ni wazi iko haja ya kurudi sokoni na pia kudai fidia.

na bill wa ars

na bill - 19.06.08

Huyu mbuge ni mnafiki mkubwa.
Huwapongeze kwanini huyu alikuwepo tangu awali alikuwa wapi kusema?
Kama anawajali waTz sana mbona hiyo posho yake hakatai kusign
Hiyo posho ingejenga vyoo vingapi kwenye shule za jimbo lake

Aache uongo huyo naye ni F....tu ana lolote.

na Mapalala, Mwanza, - 19.06.08

nyarandu wadanganye wasokujua,wewe si ndo ulokuwa unakusanya pesa za vijana unawaambia unawapeleka summer camp marekani alafu unaingia mitini,wewe ni fisadi number moja,umewadhuumu vijana wengi sana dar na arusha,kujidai agency wa summer camp,baada ya marekani kuzuia summer camp ndo ukachukua pesa kupeleka singida kuwanunulia wananchi michele wakupe kura.bora unyamaze maana umeshakula jasho la watu sana,wewe ni fisadi mkubwa.

na msema kweli - 19.06.08
kikwete hatufai na mawaziri wake wote kwani hawana mipamgo ya maendeleo kwa wananchi waliowapa kura.

Ninasema hivyo kwa sababu bei inafumuka kila siku na wala haipungui
mshahara hautoshelezi mahitaji ya kila siku.

Hivi mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha na mishahara hamuongezi mnatarajia nini?

Matokeo yake mnaongezana mishahara na posho zenu kwanini? Ina maana hii nchi ni yenu na sisi ni wafanyakazi wenu eti?

Hata kama ni hivyo boss mwema hufikilia maslahi ya mfanyakazi wake pia ili ajikite kwenye kazi zako wewe je mnafanya hivyo

MLAANIWE NA MSHINDWE IPO SIKU MTAJUTIA UAMUZI WENU WA KIPUUZI WENYE HUSUDA NA CHOYO

UONGOZI WENU UTAISHA NA HAMTAONDOKA MADALAKANI MLIPO NA SIFA YEYOTE BALI VICHWA CHINI NA AIBU TELE
NA NYINYI MTAISHIA KUANDAMWA KAMA MKAPA NA VIONGOZI WENZIE

HAMTAKAA MUIPATE SIFA KAMA YA BABA WA TAIFA HILI AU MUASISI MNAEJISIFIA KUFUATA NYAYO ZAKE

CCM SIO ILE YA NYERER HIIIIIIIIIIIIII NI YA WEZI WATUPU AMBAO HAWANA MPANGO NA MWANACHI WA KAWAIDA AU MUAJILI WAO
MNAKIMBILIA KUJILIMBIKIZIA MALI AMBAZO HAMUWEZI HATA KUZIONESHA HAZALANI

ENDELEENI KUMEZA PANADOL ILI KUVITULIZA VICHWA VINAVYOUMA KWAAJILI YA KUTAFUTA PA KUFICHA VIJISENTI VYENU ILI TUSIJUE NA KUUA WATU ILI KUIFICHA SIRI ISIYOFICHIKA KAMWE

NINYI NA VIZAZI AMBAVYO MNAVIANDALIA FEDHA CHAFU HAMTAKAA MKAPATA AMANI KAMWE KAMA ALIETUUMBA ANASIKIA KILIO CHETU WANANCHI MATAJILI WA RASILIMALI LAKINI MASIKINI KWA TAMAAAAAAAAAAAAAAAA ZETU WALAFIIIIIIIIIII

na NGOSHA, kaaaaa hama, - 19.06.08

Tanzania kweli inauzwa kwa wageni wanotoa vijisenti. Huko ZnZ eneo la zaidi ya eka 220 na Ufukwe zaidi ya kilomita 3 Muyuni, wamepewa warabu wa UAE bure kujenga hoteli za wageni...Issa Macho unajua mradi huo Mh Aman Karume ana 30%? habari ndo hiyo

na pandu, Mjini Magharibi, - 19.06.08

Nampongeaza Kijana Nyarandu kwa kua nguvu ya kusema kuhusu kuuzwa nchi.Lakini angesema pia ni nani alieuza hii nchi Tajiri,amtaje.Huwezi ukasema kitu kimeizwa ni lazima umtaje.Na kuhusu waarabu kununua ardhi si hapa Tz tuu wananunua ulimwenguni mzima tena wewe shukuru wamekuja kununua huu muozo wa TZ.Tembea Gulf countries uone maendeleo si hapa maendejana.
na Mti Mkavu, Moshi/TZ, - 19.06.08
 
Back
Top Bottom