NBAA Aibu, asilimia 84 wafeli

Pengine hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya wengi wao kufeli. System mzima ya mitihani ya NBAA/CPA imeundwa kwa watahiniwa ambao wana experience ya accounting field angalau ya mwaka mmoja. Sasa kutoka fresh-from-school mpaka ku-tackle hiyo mtihani kunaweza kuwa ni mlima mmoja mrefu sana kuupanda.

Pia tusisahau kuwa mitihani hiyo iko very intimidating. Unaweza kujiandaa vilivyo, lakini jinsi mazingira ya mtihani yalivyowekwa, ni rahisi 'kuwehuka.'

Nakumbuka nilivyo-sit for CPA exam (U.S. system), nilipata headache moja ya nguvu sana. Tena afadhali siku hizi, mitihani iko computerized na wanakuruhusu kufanya one part at a time. Mimi nili-sit mtihani wa mwisho wa paper-and-pencil (Nov. 2003). Yaani ilikuwa unafanya part zote nne kwa wakati mmoja (Sat and Sun: 8am - 5pm). Kamwe sitosahau weekend ile.

Hahahahaaaa...Mazee sasa hapo unataka ku impress watu au? Maana ni kama unasema wewe ni CPA (even though you didn't specifically say that)....sawa bana mi ngoja niendelee na janitorial work yangu hapa....
 
Kufuata watasha ni kansa kwetu ukiangalia mfumo wa elimu toka msingi mpaka chuo ni madudu ya wazungu tu.lakini basi tuwajue wazungu(CPA) kwanza ili nasi tujijue kama hatutajua hata kanuni za Debit na Credit za wazungu sidhani kama tutaweza kuwa na zetu..
Maswali yako sibishi kitu na yanahitaji thread nyingine ya mfumo wa elimu walitaka kuanza kufundsha vyuo vikuu kwa kiswahili...........sijui yaliishia wapi BTW mfumo wetu africa ni tegemezi.....

Nimefurahi kwa wewe kutambua "facts (ukweli)" na kutokuwa mbishi mbishi....
 
Hahahahaaaa...Mazee sasa hapo unataka ku impress watu au? Maana ni kama unasema wewe ni CPA (even though you didn't specifically say that)....sawa bana mi ngoja niendelee na janitorial work yangu hapa....

Ha ha haaa...ingefaa ungeniuliza kama nili pass kwanza kabla hujanipiga dongo....lol

Hapana NN, mimi sio CPA. Nilichemsha vibaya mno. Nilipass parts mbili na nikavutwa parts mbili. Sijui siku hizi system ikoje, lakini wakati huo, ili upass CPA ulitakiwa kupata at least 75% kwa kila part. Na kama umepata chini ya hapo kwa angalau part moja, utapaswa kurudia ile part uliyofeli ONLY, kama umepata angalau 50%. Chini ya hapo utapaswa kurudia parts zote (including zile ulizopata 75% au zaidi). Sasa mimi, moja ya parts nilizofeli nilipata 42% (ile nyingine nilipata just over 50%), basi nikapaswa kurudia parts zote. Nikaona upuuzi....kwani hata ukibeba boksi utapata paycheck vile vile.
 
Ha ha haaa...ingefaa ungeniuliza kama nili pass kwanza kabla hujanipiga dongo....lol

Hapana NN, mimi sio CPA. Nilichemsha vibaya mno. Nilipass parts mbili na nikavutwa parts mbili. Sijui siku hizi system ikoje, lakini wakati huo, ili upass CPA ulitakiwa kupata at least 75% kwa kila part. Na kama umepata chini ya hapo kwa angalau part moja, utapaswa kurudia ile part uliyofeli ONLY, kama umepata angalau 50%. Chini ya hapo utapaswa kurudia parts zote (including zile ulizopata 75% au zaidi). Sasa mimi, moja ya parts nilizofeli nilipata 42% (ile nyingine nilipata just over 50%), basi nikapaswa kurudia parts zote. Nikaona upuuzi....kwani hata ukibeba boksi utapata paycheck vile vile.

Nili assume kuwa kama ulifeli basi hata usinge mention kuwa ulifanya mtihani huo......either way, it's all good.
 
Mimi nimepata bahati ya kufanya mitihani yote miwili yaani CPA-T na ACCA. CPA nilimaliza mwaka 2000 na ACCA mwaka 2007. Nikilinganisha mitihani hii naweza kusema kuwa ni rahisi kufaulu ACCA kuliko CPA (kabla ya CPA kubadili mitaala yao). Kwa kila stage ya CPA (Partmbili za mwisho zenye paper 4 kila moja) nilihudhuria madarasa full time (Jumatatu mpaka Jumamosi) kwa muda wa miezi 3 na kubahatika kufaulu bila ya kurudia paper. ACCA nilijisomea mwenyewe baada ya kununua vitabu vya BPP na kufaulu paper zote bila ya kurudia hata moja.

Kwa harakaharaka matatizo ya CPA kwawakati huo ni kama ifuatavyo:
1- Kulikuwa hakuna vitabu maalum kwa mitaala ya CPA ukilinganisha na wenzao wa ACCA.
2- CPA ya wakati wetu (2000) kulikuwa hakuna topic ambayo ilikuwa inajulikana lazima ije kwenye mtihani tofauti na ACCA ambayo unajua kabisa baadhi ya topics lazima zije kwenye mtihani. Kwa mfano ACCA Financial Accounting F7 swali la kwanza ni Group accounting, swali la pili ni preparation of financial statements etc. Hii kidogo inarahisha kazi ya mwanafunzi.
3- Muda wa kujiandaa kwa CPA ni mdogo kwa walio wengi ambao wanatoka makazini.

I stand to be corrected.
 
Kwa harakaharaka matatizo ya CPA kwawakati huo ni kama ifuatavyo:
1- Kulikuwa hakuna vitabu maalum kwa mitaala ya CPA ukilinganisha na wenzao wa ACCA.
.
Sina uhakika kama sasa hivi pia wana vitabu maalum.....
Mkuu wewe umefanya CPA kwa kaungalia apart namatatizo hayo uliyosema suala la kuwa CPA wanabana ni sahihi nasikiaga kuwa vile vizee NBAA vinapanga watu wa kufaulu....
 
Hivi kwa nini watu wengine wanaona CPA kuwa big deal?
Muulize Shazulu faida za CPA
Median-Salary-by-Job---Certification-Certified-Public-Accountant-CPA-United-States_USD_20081230075728-v1.0.jpg

Sijui unaulizia dili kivpi kamanda?
 
Hivi kwa nini watu wengine wanaona CPA kuwa big deal?

Kama nakumbuka vizuri zamani kidogo (miaka mitatu au minne hivi back) kuna mzungu mmoja pale muhimbili (au MOI kama nimesahau!) alipoteza kazi kwa kukosa sifa hii (CPA). Kuna kazi nyingi tu kwenye medani za uhasibu/fedha huwezi kupewa (au kuajiriwa) kama huna CPA. Makazini pia kuna stage unaweza kukosa promotion ikiwa huna CPA.
 
Guys,

Kuna mapungufu mengi kwa upande wa wanofanya mitihani ya CPA nchini Tanzania na hata kwa watanzania wanaofanya ACCA.Maandalizi yetu wengi ni ya zimamoto na tunaweka mkazo katika kukariri maswali ambayo huulizwa mara nyingi na kusoma majibu yake badala ya kuweka mkazo wa concept zaidi ambazo ndiyo hasa tunazopaswa kuzitumia katika kazi zetu za kila siku kama wahasibu.Matokeo yake ni kuwa na kizazi cha wahasibu wenye CPA na ACCA lakini ambao uwezo wao katika taaluma ya uhasibu ni mdogo.

Wito ni kwa wote wanaofanya mitihani ya CPA,ACCA na hata CIMA wajitahidi kuweka mkazo mkubwa zaidi katika kuelewa concept za uhasibu badala ya kukariri,hiyo itaweza kuboresha uwezo wao katika kazi na kuinua heshima ya taaluma hii nchini.

Asanteni.
 
Hao jamaa wanacomplicate tu kuna watu wamegraduate juzi but wakifanya CPA wanapass modole E wakija F lazima wakamatwe
Ukiwa na CPA ndio unaonekana ACCOUNTANT/AUDITOR wa ukweli
 
Hili tatizo solution yake nini?

Mitihani ya NBAA inahitaji maandalizi mazuri sana. Mimi naamini kabisa ukijiandaa vyema utapita, na kama una uelewa mzuri wa uhasibu, yaani kama hujadandia gari la wahasibu njiani then naamini kabisa utapita. Ila ni kweli watu wengi wanashindwa kabisa kujiandaa vyema.

Na hii haitokani na kuzembea maandalizi tu, bali zaidi ni mazingira. Kama wadau wengine walivyosema, watu wengi wanaofanya CPA Exams wanakuwa wako makazini - yaani kwa education system ya TZ ambayo serikali wamei-complicate, lazima utafika Final Stage ukiwa ushaajiriwa. Na mwajiriwa siku zote huwezi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma, unarudi nyumbani uko hoi.

Na sababu nyingine kuu, ni lack of standardized materials. Yaani mtu unafanya CPA as if unafanya paper ya NECTA form four. Ambapo hujui hata ni upande gani hawa watu watakamua, na wala huna nyanga kama wenzetu wa ACCA.

Ushauri wangu ni kwa bodi kuandaa standardized materials (study kits pamoja na exam kits) kama ACCA then waone ni watu wangapi watapass mitihani. Lazima pass rate itaongezeka kwa kasi kubwa sana. Manake hata kama uko bize kazini and you have all the materials, unaweza ukajibana kumaliza maandalizi. But kwa sasa, mtu uko kazini, then unasoma bila direction ya kutosha zaidi ya kale kakitabu ka syllabus, hapo sijui utakuwa unategemea nini zaidi ya kunyakwa.
 
CPA inafanywa kama tiketi ya kwenda Mbinguni ambayo vizee pale NBAA ndio vinatoa ruhusa......Shonge analysis yako nimekubali lakini pamoja na hayo yoote sidhani kama ndio haswa sababu ya kufeli more than 80%.....kwa taarifa yako ni kuwa wengi wanaofanya CPA siku hizi hawapo kazini ni vijana wenye Adv Diploma na Degree za accountancy ambao wengi wao hawan kazi so wako busy na kusoma tu tangu wamalize chuo....
Mbona Open Univer wanafunzi wake wengi ni wafanyakazi lakni hawafeli namna hii......ukweli ni kuwa vile vizee vina roho mbaya vikiona kijana under 30 anakula CPA uku wenyewe walisotea miaka zaidi ya 20......

Pia suala la kuchoshwa sio mkuu nasikia majuu watu wanabeba box masaa kibao an wanakula buku na wanafaulu iweje Tz isiwezekane?


Kijana ume spesholaizi kwenye fani gani?
Umewahi kusoma tz elimu ya juu?

YoYo from what I read in your comments it's like you want to make people believe that NBAA wana idadi au age limit ya watu kuwa CPAs. I'm not personally going to subscribe to that because I have done the exams myself and I had to change my original position on the matter. hata mie nilikuwa na mtizamo hasi ingawa sio kama ulikofikia wewe.
1. There are many people who get CPAs at the age below 30. I got mine when I was 25.
2. Kufanya kazi kunatakiwa kuhesabiwe kama advantage na sio disadvantage kwenye kufaulu hiyo mitihani, as long as kazi unazofanya ni za kihasibu. Sio kushinda unahesabu cash [bank teller] then unataka kuelewa uhasibu. There is a practical element built into the exam questions.
3. Kulinganisha wanafunzi wa Open University na CPA candidates ni upotoshaji. I've had a chance to understand [and participate] in the system of open University in different capacities. Hao jamaa mfumo wa coursework upo [just like for other colleges/universities]. But then hizo assignments zao there are cases where wanawalipa watu a small amount of money wanawafanyia. But then hata aina ya maswali wanayoulizwa they are not that much practical.

4. Hao jamaa waliomaliza ADA halafu wanakomaa tu na CPA na hawapati si watafute vitu vingine vya kufanya. There is no point kuendelea ku'invest' kwenye issue ambayo hamna dalili ya favorable payoff.

5. Sina evidence kwamba kuna hao unaowaita 'vizee' huko NBAA, but kama wapo basi tungependa kuwatembelea. It would be an interesting tour. Could you organize it?
 
kuna watu wamegraduate juzi but wakifanya CPA wanapass modole E wakija F lazima wakamatwe

Belo nadhani hapa hauko informed vya kutosha. In fact kwa CPA [T] (final stage) syllabus ya sasa [current] ni rahisi ku'clear' [kufaulu] module F kuliko kufaulu module E.
 
wabongo tunakariri na CPA hawataki kukariri wanataka kupata Mamenager ambao wataleta manufaa kwenye taasisi Mtu unaulizwa Function za Interna Auditor General ni nini? wewe unaanza kukariri badala ya kutoa self explanational za kitaaluma then wewe unaanza kukariri kwa Mfano MA maswali yanahitaji uelewa and assumtion zako na individual skills na conclution jitu linatoa micalculation tu linaacha wazi so wewe ni manajor utakuwa unatengeneza cost control report then unaidistribute to kwa board of director bila kutoa ufafanuzi kamili sasa wakupe CPA ukavurunde na unajua ya kuwa CPA ndo mambo yote Tanzania Jamani Wabongo Acheni Taaluma na Siasa yasitukute ya shule za kata Jamani.
 
wabongo tunakariri na CPA hawataki kukariri wanataka kupata Mamenager ambao wataleta manufaa kwenye taasisi Mtu unaulizwa Function za Interna Auditor General ni nini? wewe unaanza kukariri badala ya kutoa self explanational za kitaaluma then wewe unaanza kukariri kwa Mfano MA maswali yanahitaji uelewa and assumtion zako na individual skills na conclution jitu linatoa micalculation tu linaacha wazi so wewe ni manajor utakuwa unatengeneza cost control report then unaidistribute to kwa board of director bila kutoa ufafanuzi kamili sasa wakupe CPA ukavurunde na unajua ya kuwa CPA ndo mambo yote Tanzania Jamani Wabongo Acheni Taaluma na Siasa yasitukute ya shule za kata Jamani.

wengi wamezoea kukariri na kuzima moto...
 
mimi naomba kujulishwa.....je madaktari au ma engineeer au walimu wanafanyaga mitihani ya kuwapima kama hii ya CPA(T)???? na kama hawafanyi kwa nini?
 
Back
Top Bottom