NBAA Aibu, asilimia 84 wafeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NBAA Aibu, asilimia 84 wafeli

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Babuji, Jan 4, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Jan 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WATAHINIWA wapatao 2,602 wamefeli mtihani wa bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu [NBAA]

  Tarifa iliyotolewa na bodi na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Pius Maneno ilisema jumla ya waliofanya mtihani huo walikuwa 3,125 na kati yao watahiniwa 523 tu sawa na asilimia 16.7 walifaulu.

  Source: Nifaamishe
   
 2. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,265
  Likes Received: 4,238
  Trophy Points: 280
  Mkubwa mbona hao ni wengi kuna kipindi walikuwa wanafaulu hata 30 hawafiki
  BTW-Hao jamaa wa CPA wanacomplicate sana
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Tangu Utoah atoke pale angalau wameanza kufaulu kwa wingi kidogo....kweli hapo kabla ni balaa sana...sijui kuna fixed no ya candidate kupata cpa ama kweli hawafiki viwango vya kufaulu...
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Aibu

  Kwa wahadhiri, wanafunzi na Taifa... kwa ujumla... naomba kujua watahiniwa wa ACCA kutoka Tanzania nao wanashindwa mitihani kwa kasi hiyo hiyo?
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ACCA ni fedha yako ya mitihani na hard work tofauti na CPA(T) ukiritimba mwingi.Kuna jamaa kaanza kufanya CPA tangu niko sekondari nasikia mpaka leo.........nilimwambia bora akafanya CPA(somalia) atafaulu
   
 6. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hiyo CPA inatolewa na wao tu Tanzania nzima?Kuna jamaa aliniambia kuwa kwa bongo wenye CPA ni wachache sana Mengi akiwa mmojawao,hivi hiyo kitu ni mali sana ndiyo mana jamaa wanabana?Naomba wakuu mnichanganulie jinsi ya kuipata hiyo CPA na ujiko wake!
   
 7. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Nadhani kuna haja ya kutafuta namna ya kuhusisha ufanisi wa wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na Mitihani mingine inayotolewa na Bodi kama NBAA na ufanisi wa Walimu/Wahadhiri wa Wanafunzi hao. Iweje Walimu wa shule za Msingi na sekondari tu ndiyo wanaotakiwa kuwajibika kwaajili ya matokeo ya mitihani ya Wanafunzi wao ambayo hata hivyo wao hawaitungi?. Kule shinyanga imetangazwa kuwa kuna Walimu Wakuu kadhaa wamevuliwa nyadhifa zao kwaajili ya matokeo mabovu ya wanafunzi wa darasa la saba yaliyotoja Desemba 2008 na kupelekea Mkoa wa Shinyanga kuwa wa mwisho kitaifa. Kwa vile watu wa NBAA wamekataa watu kufanya mitihani yao kama hawajajiandikisha na kusoma review katika vituo wanavyovitambua, kuna haki ya kuona namna gani hao wanaoendesha reviews wanaweza kuwajibishwa kwa matokeo mabovu ya wanafunzi wao. Isije ikawa ni chuma ulete
   
 8. s

  shonge Member

  #8
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2007
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Licha ya mapungufu ambayo yanaweza kuwa ya kimfumo [systematic] katika hili, nadhani ni vema pia tuangalie upande wa watahiniwa wenyewe wa mitihani husika. Wengi wa watahiniwa [hasa wa final stage modele E and F] ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu. Hawa ni watu ambao wakiwa vyuoni husoma semester moja kwa wiki 15, hupimwa kwa Coursework pamoja na final examination, tena examiner anakuwa yule yule ambaye hufundisha, hivyo ukimjulia angle anazopenda tu umefaulu. Lakini haishangazi kuona mtu ana supplementary moja au mbili kwa semester.
  Anapofika kwenye mitihani ya NBAA:
  Kwanza: anayetunga/sahisha mtihani si rahisi kutokea coincidence kuwa ndiye aliyemfundisha
  Pili: Syllabus [at least for core subjects in the final stage] inashauri mtahiniwa apate 9 months of full time training ili aweze kufanya mtihani. Most of us tumefanya 3 months of weekend/evening trainings.
  Tatu: Hata hizo weekend/evening training tunahudhuria tukiwa tumeshachoshwa na waajiri, na pia mahudhurio yanakwamishwa na foleni, vikao vya arusi, semina za kikazi, n.k.
  Nne: watahiniwa wengine hawafanyi kazi za kihasibu maofisini mwao hivyo wanaishia kukariri

  Sasa tujiulize, Je wakifeli tushangae??, mie naona hata hiyo 16% iko juu sana.

  Naomba kuwasilisha!!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hao waliofeli hawana akili, period....
   
 10. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #10
  Jan 5, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SHONGE UMEKUWA MUWAZI MPAKA NIMEFURAHI. mAANA WATU WANATAKA WALETE SIASA KWENYE TAALUMA.
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  CPA inafanywa kama tiketi ya kwenda Mbinguni ambayo vizee pale NBAA ndio vinatoa ruhusa......Shonge analysis yako nimekubali lakini pamoja na hayo yoote sidhani kama ndio haswa sababu ya kufeli more than 80%.....kwa taarifa yako ni kuwa wengi wanaofanya CPA siku hizi hawapo kazini ni vijana wenye Adv Diploma na Degree za accountancy ambao wengi wao hawan kazi so wako busy na kusoma tu tangu wamalize chuo....
  Mbona Open Univer wanafunzi wake wengi ni wafanyakazi lakni hawafeli namna hii......ukweli ni kuwa vile vizee vina roho mbaya vikiona kijana under 30 anakula CPA uku wenyewe walisotea miaka zaidi ya 20......

  Pia suala la kuchoshwa sio mkuu nasikia majuu watu wanabeba box masaa kibao an wanakula buku na wanafaulu iweje Tz isiwezekane?

  Kijana ume spesholaizi kwenye fani gani?
  Umewahi kusoma tz elimu ya juu?
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  jamaa wanabana?Naomba wakuu mnichanganulie jinsi ya kuipata hiyo CPA na ujiko wake!
  Tangu ianzishwe mwishoni mwa miaka ya 70 mpaka leo CPA holder hawajafika 2000! aibu kubwa CPA vile vizee vinaona mali ndio maan vinabana lakini majuu na sehemu zingine CPA sio ishu kuipata na sio mali kihivyo kamanda.
  Jinsi ya kuipata angalia site yao hapa na hapa
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Nime-specialize kwenye Janitorial Science na nina PhD.
  Sijawahi kusoma Tanzania elimu yoyote ya juu na wala sitaki na sijawahi kutaka kusoma huko elimu yoyote ya juu.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani sababu kubwa ya watahiniwa kufeli ni kutofanya maandalizi ya kutosha, (Zima moto) na pia waalimu pia huchangia wanafunzi kutofaulu. Mimi huamini kunapokuwa na mass failure basi ni indication kuna shida kwa waalimu na mfumo mzima wa ufundishaji.

  Ushi
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sababu kubwa ni wanafunzi kutokuwa na uwezo wa kuelewa wanayofundishwa. Sasa hapa kuna mawili. Aidha ni hawana akili au hawaelewi lugha itumiwayo katika kufundishia masomo hayo.
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu elimu ya bongo yenyewe ina mushikeri long time.....lakini iweje miaka yoote CPA wafeli wakati masomo mfano Module E na F ni marudio waliokwisha yasoma Undergraduate zao?

  Janitor fafanua uwezo wa kuelewa kivipi kama mtu kasoma Taxation second yr akaielewa na akaifaulu then akaikuta Module E iweje asielewe hata kama alikariri basi akifundishwa tena itakuwa rahisi kwake kulielewa somo kiundani.Lugha ni ngeli rahisi ya minus,plus deduction,trading and profit na vitu kama hivyo hakuna lolno longo za ngwini.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Matatizo yetu sisi tunafuata tu yale yaliyopangwa na wadhungu. Dhana (concepts) karibu zote zinazofundishwa ziliasisiwa na wadhungu. Unabisha?

  Hivi kuna waasisi gani weusi Waafrika waliovumbua mikanuni ya uhasibu? Hata hiyo CPA ilianzia wapi? Nina uhakika sio Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Unabisha?

  Halafu "Module E na F" zinaitwaje kwa Kiswahili au Kinyantuzu? Jibu ni haziitwi chochote. Kwa nini? Niambie wewe.....
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Seriously this issue its paining me we must come with concrete reasons why wafeli mnajua makampuni mengi ya kigeni nowadays hapa na wakitangaza kazi za accountants wanahitaji CPA or ACCA holders ambayo wabongo CPA ni kama mbinguni ndio maana unakuta wakenya na CPA(K) zao wapo kibao maofisini.
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kufuata watasha ni kansa kwetu ukiangalia mfumo wa elimu toka msingi mpaka chuo ni madudu ya wazungu tu.lakini basi tuwajue wazungu(CPA) kwanza ili nasi tujijue kama hatutajua hata kanuni za Debit na Credit za wazungu sidhani kama tutaweza kuwa na zetu..
  Maswali yako sibishi kitu na yanahitaji thread nyingine ya mfumo wa elimu walitaka kuanza kufundsha vyuo vikuu kwa kiswahili...........sijui yaliishia wapi BTW mfumo wetu africa ni tegemezi.....
   
 20. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Pengine hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya wengi wao kufeli. System mzima ya mitihani ya NBAA/CPA imeundwa kwa watahiniwa ambao wana experience ya accounting field angalau ya mwaka mmoja. Sasa kutoka fresh-from-school mpaka ku-tackle hiyo mtihani kunaweza kuwa ni mlima mmoja mrefu sana kuupanda.

  Pia tusisahau kuwa mitihani hiyo iko very intimidating. Unaweza kujiandaa vilivyo, lakini jinsi mazingira ya mtihani yalivyowekwa, ni rahisi 'kuwehuka.'

  Nakumbuka nilivyo-sit for CPA exam (U.S. system), nilipata headache moja ya nguvu sana. Tena afadhali siku hizi, mitihani iko computerized na wanakuruhusu kufanya one part at a time. Mimi nili-sit mtihani wa mwisho wa paper-and-pencil (Nov. 2003). Yaani ilikuwa unafanya part zote nne kwa wakati mmoja (Sat and Sun: 8am - 5pm). Kamwe sitosahau weekend ile.
   
Loading...