Nawezaje kuwa Vegetariani (Kuacha kula nyama)

Ule nyama usile...utakuf tuu.
Hao wanyama nani awale?
Kutana na kitimoto safi....halafu uje
 
Ulaji wa nyama unahusishwa sana na magonjwa ya moyo na cancer. Nimeishi baadhi ya nchi zenye walaji wa nyama sana na nimeshuhudia. Nyama kwa asili ni chakula chenye asidi nyingi na uwepo huo wa asidi unaongeza hatari ya mwili kushambuliwa na magonjwa.

Anayeweza kuacha ulaji wa nyama anajiongezea umri wa kuishi, kuonekana mdogo tofauti na umri wake, kuongeza performance hasa kwenye michezo (Ronaldo na Messi pamoja na wanamichezo wengi ni vegetarians), na zaidi kujisikia fit siku zote.
Huu ni uongo. Ronaldo anakula nyama na anatumia animal products. Vegetarian Ronaldo na huwa anaangalia bullfights. Na mbaya zaidi keshafanya matangazo ya KFC.
 
Kila jambo linaanzia kwako,maamuzi. Hakuna mtu atakusaidia mbinu,bila wewe kuamua. Sili nyama mwaka wa 11 sasa. Isipokuwa nakula samaki. Chakula changu kikuu ni matunda,hasa usiku
Umetuzidi nini sasa sisi tunaokula nyama mazee? Tusitishane aisee!
 
Kuchinja kunakotakiwa kwa wanyama, kuku nk, ni kukata koo la mnyama hadi kukata mishipa miwili mikubwa ya damu inayopeleka damu kichwani, damu inapokuwa imeisha ndipo inatakiwa kukata shingo lote, wataalamu wa Biology wanasema unapochinja koo hadi kwenye hiyo mishipa mnyama anapata maumivu kidogo sana kuliko kuchinja kwa kukata shingo lote kwa maramoja. Shingo linatakiwa kumaliziwa pale ambapo damu yote ya.mnyama imemalizika kutoka hapo ndipo mawasiliano kati ya ubongo na mwili yanapotoweka na hivyo kwa wakati huo ukikatashingo lote.mnyama hapati maumivu
Mkuu katika uchinjaji kuna kitu tunaita "Humane slaughter" hii ni njia ya kuzuia maumivu wakati wa kuchinja. Hapa mnyama tunamfanyi stunning kwa kutumia bunduki ya umeme au ya Baruti. Hapo mnyama anazimia ndipo anachinjwa bila kujua!
 
Sijui utakuwa uliletwa hapa duniani kwa ajili ya nini aisee! Mungu alipotuweka hapa dunia alitufanyia kila kitu cha kula sisi na kufaudu matunda ya uumbaji! Mimi siachi nyama abadan!
Mi nawashangaa sana hawa vegetarians


Mungu hata hakukataza kula nyama ni kanuni za kujitesa walizojiwekea wao



Wengi sometimes wanakumbwa na healths complications za ajabu
 
Back
Top Bottom