Nawezaje kuwa Vegetariani (Kuacha kula nyama)

Binafsi nakula nyama lakini sijawahi kuchinja hata kuku na ikitokea nikashuhudia mnyama yeyote akichinjwa mbele yangu,count me out kwenye hicho kitoweo.

Nina huruma na ni muoga wa kuona damu kitu kilichofanya enzi hizo nibadili gear angani kwenye kusoma PCB, hapa nilipo sijawahi shuhudia hata mwanangu akichomwa sindano, ikitokea nahisi nitatokwa chozi. Huwa najikalia zangu nje ya chumba cha daktari..
 
Ulaji wa nyama unahusishwa sana na magonjwa ya moyo na cancer. Nimeishi baadhi ya nchi zenye walaji wa nyama sana na nimeshuhudia. Nyama kwa asili ni chakula chenye asidi nyingi na uwepo huo wa asidi unaongeza hatari ya mwili kushambuliwa na magonjwa.

Anayeweza kuacha ulaji wa nyama anajiongezea umri wa kuishi, kuonekana mdogo tofauti na umri wake, kuongeza performance hasa kwenye michezo (Ronaldo na Messi pamoja na wanamichezo wengi ni vegetarians), na zaidi kujisikia fit siku zote.
 
Wana JF Habari,

Naomba kupata mawazo yenu hapa,,nimekuwa nikijaribu mara nyingi sana kuacha kula nyama yaani kuwa vegetarian lakini nimeshindwa. Kuna kipindi nilijitahidi kuacha kwa wiki mbili tu lakini bado nikarudi kula nyama choma ya ng'ombe na mbuzi na makange ya kuku kama kawaida. Napenda kuacha kula nyama kabisa sababu;

1.Huwa kuna nyakati naona kama kuchinja wanyama ni ukatili na kuwasababishia maumivu

2.Wanyama wakati wa kuchinjwa huwa wanakuwa na hofu sana hivyo kusababisha adrenaline kusambaa mwilini mwao ambayo sio afya kwa mwili wa binadamu. Ndio maana nyama huwa zinapuliziwa madawa zikiwa machinjoni ili zisiharibike mapema zikiwa buchani (sababu adrenaline hufanya nyama ianze kuharibika mara baada ya mnyama kuchinjwa)

3. Wanyama wengi hukuzwa kwa madawa makali siku hizi; ni kama kuona ng'ombe ambaye hajazaa na anatoa maziwa mwaka mzima!!! hii ni hatari sana....

4.Virutubisho tunavyovitafut kwenye nyama vipo kwa wingi sana kwenye vyakula vingine kama maharage,choroko n.k.

5.Nyama za wanyama huwa zinakuwa na magonjwa mengi ambayo mnyama alikuwa nayo mfano rift valley fever, mafua ya ndege, n.k

Kwa wale ambao wamefanikiwa kuacha kabisa kula nyama anipe njia nzuri na mimi niache nyama kabisaaaa...
kila kitu kinahitaji maamuzi ya kwako mkuu, ukiona unashindwa kusimamia unachokitaka au kukiamua una matatizo ambayo daktari ni ww mwenyewe.
 
Acheni mambo ya wazungu. Wanyama waliwekwa waliwe na huwezi kumla bila kumchinja. Unamuoneaje huruma ng'ombe aliechinjwa vingunguti we umekuta nyama buchani.

Kuna wanyama wa kufuga tu na kuishi nao kirafiki na kuna wa kuliwa. Wa kuliwa kula tu. Weka na pilipili kwa mbali.
 
Kukamata Mnyama na Ukamuuwa na kumla ni kitendo cha Ukatili sanaa..

Mleta Mada Upo sahihi kabisa Mnyama yeyote ni Rafiki wa Binadamu na Pia ni msaidizi wa Binadamu..
 
Kuna hekalu LA Marastafarian Kigamboni kajiunge pale,utakuwa unavuta bangi na utafanikisha ulaji was mbogamboga kwa wingi
 
Ukiacha kula Nyama utakuwa na uhakika wa kuwa na miaka angalau 100 huku unameno yote na mgongo hujapinda bila magonjwa yoyote ya uzeeni
 
Back
Top Bottom