Nawezaje kuwa Vegetariani (Kuacha kula nyama)

Wana JF Habari,

Naomba kupata mawazo yenu hapa,,nimekuwa nikijaribu mara nyingi sana kuacha kula nyama yaani kuwa vegetarian lakini nimeshindwa. Kuna kipindi nilijitahidi kuacha kwa wiki mbili tu lakini bado nikarudi kula nyama choma ya ng'ombe na mbuzi na makange ya kuku kama kawaida. Napenda kuacha kula nyama kabisa sababu;

1.Huwa kuna nyakati naona kama kuchinja wanyama ni ukatili na kuwasababishia maumivu

2.Wanyama wakati wa kuchinjwa huwa wanakuwa na hofu sana hivyo kusababisha adrenaline kusambaa mwilini mwao ambayo sio afya kwa mwili wa binadamu. Ndio maana nyama huwa zinapuliziwa madawa zikiwa machinjoni ili zisiharibike mapema zikiwa buchani (sababu adrenaline hufanya nyama ianze kuharibika mara baada ya mnyama kuchinjwa)

3. Wanyama wengi hukuzwa kwa madawa makali siku hizi; ni kama kuona ng'ombe ambaye hajazaa na anatoa maziwa mwaka mzima!!! hii ni hatari sana....

4.Virutubisho tunavyovitafut kwenye nyama vipo kwa wingi sana kwenye vyakula vingine kama maharage,choroko n.k.

5.Nyama za wanyama huwa zinakuwa na magonjwa mengi ambayo mnyama alikuwa nayo mfano rift valley fever, mafua ya ndege, n.k

Kwa wale ambao wamefanikiwa kuacha kabisa kula nyama anipe njia nzuri na mimi niache nyama kabisaaaa...Vegans tuje hapa

Mkuu kuacha kula nyama sio jambo zuri kwa afya yako.

Nyama unayotakiwa kutoila ni kitimoto na nyama za wanyama wakali.

Umetoa sababu kwamba kuchinja wanyama ni ukatili hiyo ikiwa ni moja ya sababu za kuacha kula nyama, ni hivi hata hizo mbogamboga (vegies) unazotaka kuwa unakula nazo zina uha, unapovuna mmea ni sawa na kutoa uhai wake na hapo pia kutakuwa na ukatili kwa maoni yako.

Kuhusu sumu; unadai wanyama huzalisha adrenaline na hivyo nyama kuwa a madhara kwa mtumiaji; ni hivi, hata baadhi ya mimea tunayokula pia inayosumu ya mojakwamoja (inherent) au ya kuwekwa (artificial), sumu ya moja kwa moja ni kama sumu ya kwenye mihogo na uyoga na sumu kuvu iliyopo kwenye karanga kavu na mahindi makavu, sumu ya kuwekwa ni zile dawa za viwandani zinazotumika kuhifadhia hivyo vyakula katika maghala nk, ambazo huwa hazimaliziki kabisa kwa kuoshwa, kuna sumu zingine katika mimea huwa ni za kijenetic kama GMO (genetic.modified) na sumu zingine hutokana na mbolea za viwandani na ndio maana sikuhizi watu wengi waneamua kuachana na mbolea hizo na kuingia katika mbolea za asili (organic fertilizers) kama Vinyesi vya wanyama na mboji.

Ninachitaka kusema ni kwamba; hata huko unapotaka kwenda kwenye mimea nako hakuna usalama 100% kwani hata kwenye hewa na maji tunayokunywa kuna sumu kibao.

Mwanadamu kiasilia ni "omnivorous" yeye ameumbwa kula vyakula mbalimbali ili kujenga afya yake (a balanced health) hivyo inampasa ili akidhi mahitaji ya afya ya mwili wake ni lazima ale "balanced diet" ambayo inapatikana kwa kula vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na protein ya wanyama.

Wataalamu wa chakula na lishe wanasema; "we are what we eat" yaani: Tabia na hulka zetu zinatokana na vyakula tunavyokula, mfano ukipendelea sana kula nyama ya ng'ombe, maziwa, kisusio nk, basi tabia yako utakuwa ni mtu wa hasira zaharaka na magomvi na usiyependa suluhu katika mambo madogo halikadhalika ukipendelea sana kula mbogamboga wewe utakuwa ni mtu mpole na khofu kiasi kwamba unaweza kudhulumiwa haki zako na ukashindwa kupigania hizo haki, mfano halisi ni huu, wanyama wanaokula nyama kama simba, chui, nk ni wakali ki silka (instinctive) na wanyama wanaokula majani (mbogamboga) ni wapole ki silka.

Mwanadamu anatakiwa awe mkali pia mpole inapostahili hivyo binadamu ameumbwa ale mchaganyiko wa vyakula vyote, nyama, Mbogamboga, matunda nk.

Kifupi ni kwamba sio vizuri kwa afya yako kuacha kabisa kula nyama.
 
Asante bro..ila umepinga hoja zangu kwa kuzilinganisha na mimea...najua pande zote haziwezi kuwa sawa kwa madhara...pia swala la kuchinja siko sawa nalo.
 
Sikia mkuu, kuna kuchinja kwa aina nyingi.

Kuchinja kunakotakiwa kwa wanyama, kuku nk, ni kukata koo la mnyama hadi kukata mishipa miwili mikubwa ya damu inayopeleka damu kichwani, damu inapokuwa imeisha ndipo inatakiwa kukata shingo lote, wataalamu wa Biology wanasema unapochinja koo hadi kwenye hiyo mishipa mnyama anapata maumivu kidogo sana kuliko kuchinja kwa kukata shingo lote kwa maramoja. Shingo linatakiwa kumaliziwa pale ambapo damu yote ya.mnyama imemalizika kutoka hapo ndipo mawasiliano kati ya ubongo na mwili yanapotoweka na hivyo kwa wakati huo ukikatashingo lote.mnyama hapati maumivu.

Kumbuka kwamba hao wanyama na viumbe wengine tumeumbiwa sisi na Mungu, they are at our disposal, na Huyo Mungu ndiye aliyetumbia tunaweza kuwachinja na kuwala, na njia ya kuwachinja kistaarabu bila mateso ndiyo hiyo niliyoisema.

Kumbuka tena kwamba hata mimea nayo ni viumbe hai, huwezi kula Maharage, Mahindi, mchicha, karoti bila kwanza kutoa uhai wake, kwa msingi huo huwezi kukwepa JINAI YA KUUA kwa vyote wanyama na mimea.
 
Ni uamuzi tu.

Ni sawa na maisha, maisha utakayochagua kuishi ndio maisha utakayokuwa nayo
 
Wana JF Habari,

Naomba kupata mawazo yenu hapa,,nimekuwa nikijaribu mara nyingi sana kuacha kula nyama yaani kuwa vegetarian lakini nimeshindwa.
Eboo, aliyyekuambia u-vegetarian unajilazimisha nani? Either you are or you are not.

Lakini kama unataka kujilazimisha, tafuta picha ya nyama ya mtu - au mtu aliyeraruliwa, uwe unatembea nayo. Kila ukitaka kula nyama angalia hiyo picha. Hutakaa utake kula nyama tena!

Ngoja nikusaidie kidogo hapa chini

1604866682639.png
 
Wana JF Habari,

Naomba kupata mawazo yenu hapa,,nimekuwa nikijaribu mara nyingi sana kuacha kula nyama yaani kuwa vegetarian lakini nimeshindwa. Kuna kipindi nilijitahidi kuacha kwa wiki mbili tu lakini bado nikarudi kula nyama choma ya ng'ombe na mbuzi na makange ya kuku kama kawaida. Napenda kuacha kula nyama kabisa sababu;

1.Huwa kuna nyakati naona kama kuchinja wanyama ni ukatili na kuwasababishia maumivu

2.Wanyama wakati wa kuchinjwa huwa wanakuwa na hofu sana hivyo kusababisha adrenaline kusambaa mwilini mwao ambayo sio afya kwa mwili wa binadamu. Ndio maana nyama huwa zinapuliziwa madawa zikiwa machinjoni ili zisiharibike mapema zikiwa buchani (sababu adrenaline hufanya nyama ianze kuharibika mara baada ya mnyama kuchinjwa)

3. Wanyama wengi hukuzwa kwa madawa makali siku hizi; ni kama kuona ng'ombe ambaye hajazaa na anatoa maziwa mwaka mzima!!! hii ni hatari sana....

4.Virutubisho tunavyovitafut kwenye nyama vipo kwa wingi sana kwenye vyakula vingine kama maharage,choroko n.k.

5.Nyama za wanyama huwa zinakuwa na magonjwa mengi ambayo mnyama alikuwa nayo mfano rift valley fever, mafua ya ndege, n.k

Kwa wale ambao wamefanikiwa kuacha kabisa kula nyama anipe njia nzuri na mimi niache nyama kabisaaaa...Vegans tuje hapa
...Hivi hapa
 
Ningemshauri hivi,atafute na kujiunga na kanisa la waadventista wasabato,atafundishwa njia na mbinu za kuacha ulaji wa nyama, Ova
 
Back
Top Bottom