Nawezaje kupata watoto mapacha?

Nawezaje kupata watoto mapacha?

Hi guys,
Nawezaje kupata watoto mapacha?, ikiwa kuna mtu ana uelewa juu ya jambo hili naomba kufahamishwa tafadhali.

Najua humu jukwaani kuna ma great thinkers wa kutosha.

Naomba kuwasilisha.
Kuna mikao wakati wa kungonoka, kuna mkao wa kutafuta mtoto wa kike, wa kiume na mapacha...Natoa darasa kuhusu hizo makitu na unalipia.
 
Alhamdulillah Mimi mwanamke wangu wa kwanza nilizaa nae watoto mapacha kike na kiume but walifariki walikuwa njiti ila baadae tukapata mmoja yupo mpaka sasa na mwanamke wa pili nimezaa nae pia mapacha kiume na kike wapo mpaka sasa

Asili yetu mwanamke akiwa mjamzito na ikatokea akapewa vitu vilivyoshikana viwili kwa pamoja kama ndizi au karoti huwa wanazaa mapacha maana hao wote wanawake zangu ilitokea hivyo kipindi cha ujauzito sasa sijui ni hali ya ukoo au ni bahati tu sijui
 
Pacha Raha kama hutaki kubeba mimba mara nyingi, ila nilisikia mwanamke akila sana magimbi huleta pacha, sisi bibi alizaa pacha nne ila watoto wake hamna hata Mmoja mwenye pacha, ila wajukuu ni Mmoja TU ndo kabahatika Hadi sasa
 
Pacha Raha kama hutaki kubeba mimba mara nyingi, ila nilisikia mwanamke akila sana magimbi huleta pacha, sisi bibi alizaa pacha nne ila watoto wake hamna hata Mmoja mwenye pacha, ila wajukuu ni Mmoja TU ndo kabahatika Hadi sasa
Mitano tena kwa Bibi
 
Mambo haya yana mchango wa hiko kitu kwa asilimia walau tisini na tano .

#Mambo ya kimaumbile kati ya jamii moja na nyingine ,jamii na jamii hasa kwa upande wa wanawake inautouti katika urutibishaji wa yai la uzazi hasa ukizingatia baadhi ya jamii mfano jamii fulani huko Nigeria wana uwezo wa kurutubisha zaidi ya yai moja hali inayopelekea jamii yao kuwa na watoto mapacha wengi .


#Wanawake waliowahi kuwa na uzao zaidi ya mmoja kwa kipindi fulani basi wanao uwezo wa kupata zaidi ya mtoto mmoja hasa mapacha sababu wanao uwezo wa juu wa kuweza kurutubisha zaidi ya yai moja .

#Matumizi ya dawa za ovulation yanaweza kupelekea uzalishaji wa yai zaidi ya moja hasa matumizi ya IVF ,kwa wanawake walio wengi kati ya asilimia mia moja basi ni asilimia 78 ,wengi wamefanikiwa kupata mapacha .

#Historia ya mapacha katika familia ya mwanamke ,hii imekuwa katika asilimia 65 kati ya kila mwanamke aliyetoka familia yenye historia ya mapacha basi anao uwezekano mkubwa wa asilimia 65 za kuweza kupata mapacha .

#Umri wa mwanamke kuna muda unambeba na kumsaidia yeye kupata mapacha lakini wanawake wenye uwezekano huo ni wale walau walio katika umri wa miaka 31_mpaka 43 ,kulingana na via vyao vya uzazi ni rahisi sana kupata urutubishaji wa yai zaidi ya moja .

Ila sitaki kuzungumzia kwa dawa fulani ya kingoni yenye uwezekano wa asilimi 98 kwa usahihi wa upataji wa mapacha ambayo nimeshuhudia mwenyewe japo sayansi yake sina uwezo wa kuieleza .

Hapo sijagusia dawa ya kiganda ya akabende " yenye uwezekano huo kwa asilimia 82 kwa maharibio niliyoana .

Ahsante kwasasa nimechoka kutype nitasema mengine badaye
 
Back
Top Bottom