Wewe dereva au mmiliki, huwezi kupata LATRA ya gari yako kama dereva wako hajajisajili LATRA

MGODOLO

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
209
172
1. HALI IKOJE MKOANI KWAKO
Ndugu Madereva au Mmiliki? Nataka kuuliza kuhusu mfumo huu, katika mikoa yenu ukoje, Kanda ya kaskazini, Gari yeyote ya biashara ambayo Dereva husika mwenye Leseni Daraja C1, C2, C3, C, na E.

Latra itakapoisha Muda wake katika gari hio, Mmiliki wa chombo hicho hawezi kupata Latra ya chombo chake, mpaka dereva wake akajisajili latra, ndipo gari hio ipewe leseni au kibali cha usafirishaji, Na dereva huyo ni lazima awe na cheti au vyeti husika vyenye uwezo wa kuibeba leseni yake.

2. HASARA KWA WAMILIKI WA VYOMBO
Mfumo huu moja kwa moja utawaumiza baadhi ya wamiliki wengi wenye vyombo vya biashara vinavyo endeshwa kwa leseni yenye madaraja hayo. Kwasababu asilimia 70% ya madereva wetu nchini, hawana vyeti vya udereva. Hivyo mmiliki wa chombo hatopata latra kama dereva wake hana cheti/vyeti vya udereva, hivyo mmiliki anaweza kulazimika kumwaga mpunga mwingi ili apate latra ya chombo chake ili kazi iendelee, au mmiliki amfukuze dereva kisha atafute Dereva mwenye vyeti vya udereva... Kuna usemi usemao TAJIRI HANA HASARA, ila kwa hili lazima litamghalimu.

3. HASARA KWA MADEREVA
Mfumo huu, unakwenda kupoteza ajira nyingi sana kwa madereva ambao hawana cheti/vyeti, kwasababu tajiri hawezi kulaza chombo chake. Ili kusubiri wewe ukasome udereva kisha upate cheti, ndipo gari yake ipate latra. Mmiliki wa aina hii hayupo, hivyo madereva wengi watapigwa chini, hivyo kama wewe ni dereva na unaendesha magari ya biashara ambayo una leseni yenye madaraja hayo, basi Fanya mpango wa kupata cheti haraka iwezekanavyo, kabla ya latra yako kuishi au kabla ya tarehe 31/07/2023 (UKOMO WA KUJISAJILI LATRA)

4. HESHIMA NA FAIDA KWA MADEREVA
Mfumo huu, Kama kweli utashikiliwa kindakindaki kama wanavysema, Basi itakua faida na heshima kwa madereva wenye Cheti/Vyeti,... Kwanza kabisa madereva wenye Cheti/Vyeti ni wachache sana, Hivyo heshima ya UDEREVA itarudi kwasababu, Kila mmiliki hatokubali kuajiri dereva ambaye hana Cheti/Vyeti, Kwahio kuna uwezekano mkubwa wa matajiri kupanda dau kwa madereva, yaani mfano dereva mwenye Cheti/Vyeti Anaweza Kupandiwa dau na mmiliki mwingine, ilihali yupo katika kazi nyingine. Kama unalipwa 400K, Mmiliki mpya anapanda dau atakulipa 600K hivyo TOROKA UJE. Hivyo kwa hisia zangu, Nahisi heshima itarudi kwa staili hii.

5. FAIDA KWA MADEREVA VILAZA
Mfumo huu, Nahisi utakwenda kuibua Madera ambao hawana uzoefu barabarani, Kwasababu Serikali yetu, inaridhishwa na Uwepo wa Cheti/Vyeti tu basi, Serikali yetu haitaki kujua una uzoefu gani ama una ubora gani katika taaluma yako,. Wao wanacho amini ni hizo karatasi tu, Hivyo madereva vilaza ambao wana uwezo wa darasani lakini barabarani ni hovyo, Watapata kazi sana, Hivyo mmiliki wa chombo hatomuacha dereva huyo hata kama kayaona mapungufu yake, kwasababu hawezi kulaza chombo chake kwasababu ya kutafuta dereva mzoefu na mwenye Cheti/Vyeti... Na hapo ndipo ajali nyingi zitatokea kwasababu serikali inaamini vyeti ndio kila kitu kwenye kazi.

6. MBAYA ZAIDI KUHUSU LATRA
Mfumo huu, Pia unaweza kuwapoteza baadhi ya madereva wenye vyeti. Kwasababu Latra wamechukua jukumu la ukufunzi kwa madereva hao wanaokwenda kujisajili, Ukisha jisajili Utapewa Control Number ya kulipia Tsh 20,000/= Ukisha lipia, unasubiri kufanya mtihani wa udereva, ili wakupatie cheti cha umahiri kutoka LATRA

Sasa kwa tetesi, naskia kufeli kupo njenje, na ukifeli unapokonywa leseni yako na inafutiliwa mbali,.... Hapo ndio balaa kwa wale tutakaokwenda kujisajili latra, hivyo hata ukiwa n cheti, pia utakutana na mtihani kutoka latra, hivyo jiandaeni.

7. USHAURI KWA MADEREVA
Ndugu madereva wenzangu, Tusipuuze haya mambo, kwasababu hatujui lengo la serikali yetu, kwani kwa sasa sisi madereva tumebanwa na POLISI, na LATRA.. Polisi wao wametoa miezi mitatu ya uhakiki wa Vyeti na Leseni... Lakini pia Latra wametoa miezi mitatu ya kujisajili mpaka tarehe 31/07/2023, Na polisi pia tarehe ni hio hio... Hivyo kuanzia hapo kunaweza kuamka kivumbi, japo sina uhakika, lakini tusipuuze ndugu zangu. Someni/tafuteni hayo makaratasi yao ili waridhike kupitia ubora wa karatasi na sio umahiri.

NDUGU MADEREVA WENZANGU

Nimeongea haya kwasababu mimi ni mmoja kati ya waliokwenda kujisajili Latra, na baada ya kupata baadhi ya habari, nikaona niwanyapie madereva wenzangu ili kazi iendelee... Mimi hapa nasubiri kwenda kwenye mtihani wa latra.

TUSIPUUZE MANA HATUWEZI KUSHINDANA NAO (mana naskia eti wana mkono mrefu)

Nawakilisha:- Karibuni tujadili hili swala.

IMG_20230607_115102_149.JPG
IMG_20230607_115114_183.JPG
 
Fuata sheria. Mbona issue ndogo.

Kumbe kuna madereva wa magari ya abiria hawana vyeti? Walipataje izo leseni za juu ivyo C na E?
 
Mkuu, nnavyojua leseni za juu lazima mtu uwe na cheti. Sisi wenye D tu, tunavyeti ingawa vya kanjanja.
Nakubaliana na wewe, na hata mimi nina madaraja ya juu, na nina vyeti, ila huoni itapunguza ajira nyingi sana nchini
 
Nakubaliana na wewe, na hata mimi nina madaraja ya juu, na nina vyeti, ila huoni itapunguza ajira nyingi sana nchini
Nakuelewa lakini ni bora ipunguzee ili tusiendelee kuishi kwa mazoea unao watete wana experience lakin ndio wanaongoza kwa fujo barabarani
 
Back
Top Bottom