Naweza kupata wapi mjusi mwenye kichwa chekundu?

Naweza kupata wapi mjusi mwenye kichwa chekundu?

Wana jamvi poleni na harakati!!naombeni mwongozo nitapata wapi yule mjusi mkubwa mwenye kichwa chekundu anaependa kujianika juu ya mawe makubwa!huyu mjusi kwa jina la kitaalam sijui ila kilugha namjua huwa anapenda sana kuota jua kwenye mawe mtoni au kwenye miamba mikubwa!!na nakumbuka kipindi nawinda huko vijijini ukimpiga na manati anakwepa kama anaakili vile!msaada pliez naweza mpata wapi!!!

Naona unajitafutia kesi ya kupatikana na nyara za serikali bila kujua, na hao unaowaomba wakuletee unawaingiza kwenye mtego wa kosa la unlawful dealing in government trophies, pengine naamini una kibali husika
 
Hao wanapatikana kwa wingi maeneo ya ipogolo Iringa maarufu kwa jina la kimangala
 
Wakuu wala msinichukulie mchawi au mshirikina wala niko kwenye utafiti fulani wala sina nia mbaya hofu yenu tuu!![emoji86] [emoji86] [emoji86]
 
Kumbe unajua anapatkana kwenye mawe mton na miamba mikubwa mkuu

Vip karumanzira kakuagiza nini, tumegeane siri mkuu, ni wa utajir au kumtia kilema mwiz wa mkeo.. Awe kutwa anaota jua tu mtoni...[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wako wengi sanaa ila sema wanapatikana ndani ya hifadhi which obviously itakua ni nyara tuuuu
 
aah we unasema SANGULAMANGE,sema huyo mjusi ni noma akikuuma mpaka ukambandue dada ako wa damu ndio unapona.
 
Wana jamvi poleni na harakati!!naombeni mwongozo nitapata wapi yule mjusi mkubwa mwenye kichwa chekundu anaependa kujianika juu ya mawe makubwa!huyu mjusi kwa jina la kitaalam sijui ila kilugha namjua huwa anapenda sana kuota jua kwenye mawe mtoni au kwenye miamba mikubwa!!na nakumbuka kipindi nawinda huko vijijini ukimpiga na manati anakwepa kama anaakili vile!msaada pliez naweza mpata wapi!!!

Bei maelewano ila naanzia Tshs 25000/- @ mjusi mmoja.

Unataka mmoja tu?
Unataka aliye hai au hata aliye kufa poa tu?
Upo wapi ? kama upo Dar es salaam ni Free delivery!!
Wa Mikoani gharama za usafiri ni kidogo Elfu kumi kwa Mjusi mmoja kama ni hai ila aliye kufa ni 20000/- gharama nyingine ni ya kumprocess asiharibike.

NB: kuepuka gharama za kusafirisha mjusi aliye kufa nashauri ununue mjusi aliye hai na umuue ukisha mpata.

Regards,
pH 7.
 
Wewe wa stendi hatupaswi kukuuunga mkono! Kiufupi unachofanya ni uhalifu, hizo unazotangaza humu kila siku kuzihitaji ni nyara za Serikali kama ilivyo Tembo, Faru nk. Mod angalieni hili, maana kesho mwanaJF mwingine atatangaza humu kuhitaji Pembe ya Faru kwa mamilioni na matokeo yake ni kuhamasisha Uwindaji haramu. Pls tuangalie hivi vitu kwa jicho la tatu. Lkn ktk upande mwingne kama anatumia kwa Uganga hawa viumbe Je, kesho akiweka humu bandiko la kuhitaji MFUPA WA ALBINO??? mtasema nini? Tuchukue hatua kabla chunusi haijawa jipu.
Maandishi yako yana ukakasi.
 
Back
Top Bottom