Nawaunga Mkono Madaktari

Ikiwa serikali inatoa billioni 90 kila mwaka kwa kanisa mlitegemea itapata fedha wapi zaidi za kuboresha Hospital zake..

Kanisa gani hilo?
Sikuwahi kudhani kwamba na wewe ni mdini kiasi hiki.
Afu umeanzisha thread ya kulalamika JF imechange kumbe na wewe
ni sumu kiasi hiki?
 
ukiumwa sasa hivi ukawa serious ndio utamjua kalumekenge ni nani
 


Matatizo ya madaktari na Kanisa vina ingiliana vipi mkuu?
Hapa una jaribu kufunika funika uharo ulio toa lakini wala sioni point
ya kujitetea kwa chuki zako na udini.
Duh
 
well said

uchungu wa banda la mbuzi lisiloezekwa kipindi cha mvua hauwezi kuzungumziwa na paka anayelala chumbani kwa mwenye nyumba. Acha tuzungumzie sie wenyewe! Kwani unafikiri madaktari hawajui kwamba ndugu zao wanaweza ugua huko waliko wakati huu wa mgomo na kukosa huduma? Na wao kwani ni vyuma? Wachache wafe kwa manufaa ya wengi watakaobaki. Tunataka hospitali zetu ziboreshwe. Hospitali ya taifa inakosa hata xray films! This cant be.
 

Kwa hiyo una maana makanisa ndiyo yanaendesha hospitali zote nchini pamoja na za serikali? Una maanisha nini unaposema, "kwa nini iwe jukumu la serikali wakati makanisa yalipewa hizo hela kuboresha huduma"?
 
Mkandala uliwahi kulalamika kuhusu jukwaa la siasa,....

Leo katika mada tofauti kabisa,isiyo husisha mambo ya dini wala udini,ukiwa mchangiaji
wa kwanza katika thread hii ukaanza kwa kusema:-

Ikiwa serikali inatoa billioni 90 kila mwaka kwa kanisa mlitegemea itapata fedha wapi zaidi za kuboresha Hospital zake..

Now,unabisha kwamba hujaongelea udini na wewe ndio ume chafua topic kabisa tofauti na
hoja uliyo itoa jukwaa la ulalamikaji kuhusu kuyumba kwa Jukwaa la siasa.



Kwanini tusiamini kwamba Una ID nyingi ambazo unatumia kueneza chuki za kidini humu
na ID nyingine una jidai mtakatifu?
 

Hauhitaji nakala yoyote ile.
Unacho hitaji ni kuonesha hospitali zilizojengwa na serikali
na zinatoa huduma bora ili ku-prove kwamba hospitali za ki kristo hazina umuhimu kiasi
hicho.
 

mm naisubiri hii ya walimu hata kesho mkuu.
Tatizo CWT wamekua watu wa porojo sana. Itafika wakati nitaamua kudai haki zangu mwenyewe bila kupitia CWT.
 

Sasa mkuu nimekuelewa, naungana na wewe kwa 100% inawezekana kabisa watu wenye tabia hizi za kuwa na ID maalum kwa ajili ya uchochezi huwa wanajisahau kama yupo online kwa ID nyingine ambayo watu wanaifahamu kwa ya member mwenye upeo mkubwa, ndio maana akichangia pumba ni lazima ujiulize huyu kulikoni? kudos!
 

Wewe goto,maendeleo au mabadiliko lazima yaje na maumivu,so kama wewe unatibiwa apolo poa,ila madoctor ni sahihi kugoma tumechoka na huu utawala wa kisanii,leo ukienda nje kujitambulisha kama mtz unao aibu,tunadharaulika sana
 
Raisi watu hawakuogopi,ndio maana uliowateua wanawatukana watumishi wa umma,
 
huyu ni Mkandara kweli!!?? this is too low kwa level yako, hivi hapa tunaweza kukutofautisha na Maralia Sugu? kwa hiyo solution ya matatizo haya ni kuwa na Mahakama ya kadhi na tujiunge na OIC?
Nilijua tuu,mstari wa Mkandara kuna mtu utamgusa moyoni. Kheri useme kweli upate lawama,kuliko kusema uongo upate sifa...
 
Mimi ni mmoja ya watu nisiyeunga mkono MGOMO wa madaktari.
Labda useme kwamba, wewe Gwota, huungi mkono MGOMO wa aina yoyote ile na sio ule wa madaktari peke yao, hapo labda nitaweza kukuelewa.
Nakubaliana kwamba madai yao ni ya msingi sana na serikali ndio kiini cha yote na inatakiwa iyashughulie haraka sana.
Hii si kweli, ni unafiki. Huwezi kusema unaunga mkono madai yao halafu hapo hapo unapinga hatua yao ya kuchukua the only option ambayo ina nafasi ya angalau kuwapatia ufumbuzi kwani ni the most effective.
watu wamekuwa wanaunga mkono kwa ushabiki tu na sio kwa kuangalia uhalisia na uzito wa jambo, hv utajisikia mama yako au baba yako akifa kisa mgomo wa madaktari?
Sasa hapa wewe ndiye unaleta ushabiki wa kipuuzi labda kwa kuwa wewe huyo mama yako hata unao uwezo wa kumfikisha hospitalini au nje ya nchi akatibiwe. Watanzania wangapi wanakufa kila siku bila hata hiyo huduma? Asilimia ngapi ya Watanzania hawataona tofauti yoyote madaktari wagome wasigome. You cant make an omelette without breaking some eggs!
ushauri wangu:
Km kweli sisi wananchi tunaumizwa na madai ya madaktari inatakiwa sisi ambao ni wazima tufanye maandamano nchi nzima kushinikiza serikali iwatatulie madai yao huku wao wakiwa wanaendelea na matibabu.
Hapa ndipo unapoturudisha kule kule ulikoanzia, je unajua ripple effect ya mgomo wowote ule. Hao madaktari watafanyaje kazi kama hawawezi kufika hospitalini kwa sababu wanaotoa huduma ya usafiri wamegoma, watatoaje huduma kwa wagonjwa kama watu wa utilities (maji, umeme n.k.) nao watagoma...
au wa kumkomoa kati ya serikali na madaktari tujue tunachekelea vifo vya wajawazito, vikongwe, wagonjwa wa moyo etc.
Anayechekelea hivyo vifo unavyovitaja ni serikali na si wananchi, serikali ambayo kiongozi wake mkuu anaenda kutalii huku wananchi wake wanakufa - hizo milioni 300 wanazochoma kila leo huko majuu zingeweza kabisa kuwapunguzia makali ya maisha madaktari na wakaendelea kutoa huduma japo kwa shida.
Tuache ubinafsi na ushabiki usio na maana juu ya swala muhimu la afya zetu. sidhani km muda huu ukipata ajali mbaya na ukapelekwa ICU utaendelea kuchekelea mgomo wa madaktari.
Hivi unajua waziri akipata ajali mbaya hapelekwi ICU Muhimbili, anakimbizwa India...! Anayekupeleka Muhimbili ama hajali sana hata ukipoteza maisha kwani kama wanavyodai madaktari, huko kuna ukosefu mkubwa wa vifaa na dawa. Ni asilimia ngapi ya wanaopata ajali hufa kama mbwa kwa sababu hata hiyo zahanati wanaisikia tu!
wengi mnachekelea kwa kuwa ni wazima wa afya.\
Hapa ndugu yangu umechemsha na kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, asante kwa ujasiri wako. Ukweli ni kuwa wananchi wengi kila wakiamka salama asubuhi wanamshukuru Mungu, kwani wanajua fika jinsi utoaji wa huduma mahospitalini ulivyo duni na hapa hakuna wa kulaumiwa bali serikali.
 
Hivi ina make sense kuona wabunge wanaongezwa posho mpaka Tsh. 200,000 kwa siku na wakati huo huo serikali inashindwa kuwalipa madaktari madai yao? Kweli hii serikali ni ya kipuuzi kabisa!! JK na Pinda wakiugua na familia zao wanapelekwa India ndio maana hawajali, walalahoi ndio tutazidi kufa!! Wanaotakiwa kuanzia maandamano ni Tucta ingawa hata vyama vya siasa na wanaharakati wengine inabidi wajitokeze kuunga mkono kwa sababu ni suala la kitaifa lisilojali itikadi, chama wala dini!!
 
Tatizo la mtz ukimuambia ukweli ananuna...pole sana.
 

Ukweli ni kuwa pamoja na hiyo ruzuku ndogo ya serkali ni ghali sana kuendesha hospitali na kutoa huduma kwa viwango vinvyotolewa. Kama watu wangelipia gharama zote basi ingekuwa ni mara mbilli ya bei za sasa. Hiyo ziada ni sadaka zinazotoka huko makanisani msikotaka kusikia. Baniani mbaya kiatu chake dawa. Kama unataka kupinga kutolewa kwa ruzuku kwa hospitali za kanisa kwanza zigomeeni kwenda huko kisha dai wasipewe ruzuku. Wewe mwenyewe unajua wanatoa huduma bora ndiyo maana masheikh wote wanakimbilia huko!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…