MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,596
Kwani kuna mtu aliyeletwa duniani kuokoa roho za watu? hawa madr ni kama ww na mm na udr kwao ni kaz kama uhasibu ama uhandis. wanafanya kaz kuendesha familia zao na wana mahitaji sawa na watu wa profsn zingine. Tuache ingiza suala la vifo na maslai yao. kwahiyo ni bora familia zao zife kwa kutujali sisi? kama ni lawama bac ziende kwa serikali yetu inayoongozwa na viziwi wanaoamini ktk karne hii bado udaktari na ualim ni wito. nilitegemea tuwashinikize waziri wa afya na katibu wake mkuu wajiuzulu kwa kushindwa kuzuia mgomo kutokea ambao unaleta madhara mengi kwa watz. Hapa serikali inatakiwa kuwajibika. MM nashindwa kuelewa watz cjui katuloga nani. hapa uchaguzi ukija kesho utaona watu hawa hawa wanaolalamika huku wametinga nguo za kijani wakikimbia barbarani na kuimba maisha bora kwa kila mtz. Kama haya ndo maisha bora we better shut our mouth as we have got nothn to discuss here
Salute.
Hata hivyo suala la kujiuzuru Tanzania ni msamiati wa kichina ndugu yangu. Walishindwa kujiuzuru wakati wa mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto itakuwa hii.
Dk. Mponda asema mishahara ya madaktari imerekebishwa kiasi kwamba wao sasa hivi wanapata mishahara mikubwa zaidi kuliko watumishi wengine wowote wa sekta za uma. Source: Jambo, TBC
Hivi nani kawaambia kuwa tatizo ni suala la mishahara peke yake?
Hivi nani kawaambia kuwa tatizo ni suala la mishahara peke yake?
Katika taarifa hiyo fupi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari nimeona amezungumzia mishahara na nyumba tu ambapo amesema kuhusu madai ya madaktari ya kutaka kujengewa nyumba karibu na vituo vyao vya kazi, serikali imepata pesa kutoka mfuko wa dunia (Global Fund) na imetoa kipaumbele kwa madaktari walioko mikoani, wilayani na vijijini ambako hali ni ngumu kulinganisha na za madaktari walioko mijini.
Taarifa hiyo ilimalizia na Dr. Mponda kuwaomba warudi makazini na kuwatibia wagonjwa ambao wengi wao ni wananchi wa hali ya chini wanaotegemea zaidi huduma za afya zzitolewazo na serikali kwani hawana uiwezo wa kuafford zile za binafsi.
Yeah alisema wameamua kuanza na wilaya 18 kwa kujenga nyumba 8! Kwanini hawakuanza na nyumba mbili walipowajengea mawaziri?
Na hilo swala la wananchi wa chini hivi hawa wananchi wa chini wanaanda kupata huduma mbaya sasa wakati madaktari wanagoma kwa vile huko nyuma walikuwa wanapata huduma nzuri?
Naunga mkono madai ya madaktari lakini napinga mgomo wao n
whaat? unaunga madai ya mfungwa kutaka kuwa huru lakini asigome kufanyishwa kazi kwa nguvu? kwa vile itamletea matatizo bwana wake?
Kweli Tanzania inaongoza kwa wajinga na bado hujui kuwa ni mjinga, KUTETEA UFISADI kisa unafanywa na kanisa,
Acha story za Muheza ukijidai as muheza ni mbali sana mimi naijua muheza in out, gharama za muheza ni kubwa kupita hospitali zote za serikali kwa gharama pamoja na kwamba wanapokea ruzuku; kujidai tu kwamba wewe ndio unaufahamu kupita wengine ndio UKILAZA wenyewe?? UFISADI wa KANISA kwako lazima utoke mapofu kwasababu unafaidi without auditing (goverment auditors)..
MoU ni sawa tu RICHMOND in making lakini hiyo ni kati ya kanisa na serikali na wanaofaidi hayo malipo wanajuana wenyewe???
Nenda ulizia bei ya diagnosis muheza halafu uliza pale mwananyamala ndio utaona UWIZI wa mwaka..
mimi napinga madai yao kuleta madhara ya vifo kwa raia masikini lakini kama wakiweza kudai bila ya madhara kwa wagonjwa masikini basi waendelee ata wakiweza wakarushe mawe ikulu au wafanye mapinduzi ya utawala wa serikali waongoze wao ni sawa lakini nitaendelea kupiga harakati zitazoacha vifo kwa masikini
Niambie ni lini uliona kitu kinadaiwa tanzania hii kwa
kuongea tu na kika fanikiwa bila mgomo?
kuna vitu vya msingi ambavyo wewe huvioniUnajua tumefika mahala jamani tutazame kwanza maslahi ya wananchi. Sote hapa tunaweza kubaliana na madaktari ktk hoja yao lakini maamuzi waliyofikia kuyafanya kusema kweli binafsi siyakubali kwa sababu wanawatumia wananchi maskini ya Mungu wagonjwa kupigania haki yao. Ni sawa kabisa na Al qaeda ambao wanaenda angusha jumba la Twin Tower ili ipate kusikilizwa na serikali ya Marekani kwa madai ya kuwatakaWaamerika waondoke Saudi Arabia.
Ukiweza kunisoma mtazamno wangu nadhani hatutakuwa na ubishi mkubwa hapa. Mimi ningeomba san madaktari pamoja na asasi zote za utumishi na ajira iwe serikalini au masirika ya Umma waungane na madakatari kufanya maandamano ambayo yatakuwa ya Taifa zima kupinga na kuweka madai kama yao maana sehemu zote za utumishi zina matatizo hayo. Lakini wagonjwa wataendelea kuhudumiwa na hasa wale walioko ICU, wodi ya watoto, na wanawake wajawazito, HIV na cancer, pamoja na upasuaji.
Nasikitika tu kusema kwamba wengi ya watu hapa wanadshabikia lakini hawajui madaktari wanalipwa kiasi gani na kwa mwezi daktari anaweza kuingiza kiasi gani. Nashukuru Mungu mimi nina jamaa zangu ambao ni madaktari na najua vizuri jinsi wanavyotengeza mbali kabisa na mishahara. halafu kibaya kuliko yote ambacho kimenisikisha zaidi ni kugoimbea ongezeko la Posho!...
Jamani posho kweli unaweza ijengea hoja na kufanya mgomo au ilitakiwa usifike ktk vikao ambavyo ulitakiwa kufika na kulipwa Tsh 10,000. Yes, kama kuna dawa ya kutaka posho zaidi acha kuhudhulia vikao vya posho unless serikali inakulipa kiasi unachokitaka. Na kama swala la viongozi mkwenda India.. msiwapokee waacheni watafute safari za India hata wakiumwa mafua halafu watawajibu wananchi..
Kusema kweli nimezisoma sababu zote walizozitoa madaktari haziniridhishi kiasi cha wao kugoma kutoa huduma kwa wananchi kwa madai ya haki yao. Hivi kweli kuna mtu anaweza kunipa hesabu kamili ya Daktari anatakiwa kulipwa kiasi gani? hivi kweli tunaweza kuweka mahesabu ya fedha kwa malipo ya Madaktari au Walimu na kusema huu ndio mshahara au posho wanazotakiwa kupewa!. Mimi sidhani ila najua fika kwamba mishahara yote nchini haifai na haitoshi ktk sekta zote za utumishi na kwa ujumla wa watumishi hawa kupitia Union zao wangepanga maandamano ya pamoja na wakaomba kibali ikajulikana wazi kwamba maandamano ya madaktari yatatokea siku kadhaa wakadhaa..
Hapa Canada mgomo wa madaktari ni kinyume cha sheria. Daktari hawezi kugoma kwenda kazini na kwa kupitia union yao wana hatua kama 4 za kupitia kbala ya kufikia makubaliano... mara nyingi kama sii zote huwa hawafiki hata hatua ya 3 na kama kuna mgomo basi huenda kwa vitengo lakini zipo sehemu ambazo hawaruhusiwi kabisa kuziacha wazi bila kuhudumia. Na pengine kinachowasaidia hapa ni kwamba serikali inalipa mishahara mikubwa kuliko sehemu yoyote ya binafsi iwe udaktari au hata front desk secretary ktk ofisi ya serikali.
Madaktari wanaweza kuomba ongezeko au punguzo la kazi kulingana na masaa wanayofanya kazi. Mishahara yao imepangwa kwa saa ambazo wanakuwa kazini na the more wanavyokuwa na masaa mengi ndivyo mshahara wake unapanda kama Ma pilot wa ndege.. Hivyo pengine tubadilishe mfumo wa mishahara iwe daktari atalipwa Tsh 5,000 kwa saa, kisha wajitume wenyewe kulitumikia Taifa kwa kuweka masaa mengi saidi wanaongeza pia pato lao.
Kwa hiyo kufanya mjadala hu uwe mfupi, Nyie wananchi mnaowaunga mkono madakati? kwa nini hamko nao pamoja kufanya nayi mgomo kama wenzenu. Kwa nini Tanzania ya leo kila mtu anabeba msalaba wake. Ule umoja wenye nguvu umeishia wapi kiasi kwamba mnawatazama tu madaktari wakigoma na kesho wakifunkuzwa kazi mtawacheka na kuwaita wajinga, na hata wakiomba maji ya kunywa majumbani mwenu mnawafukuza..Je huu sii unafiki wa Mtanzania!
mimi napinga madai yao kuleta madhara ya vifo kwa raia masikini lakini kama wakiweza kudai bila ya madhara kwa wagonjwa masikini basi waendelee ata wakiweza wakarushe mawe ikulu au wafanye mapinduzi ya utawala wa serikali waongoze wao ni sawa lakini nitaendelea kupiga harakati zitazoacha vifo kwa masikini
Niambie ni lini uliona kitu kinadaiwa tanzania hii kwa
kuongea tu na kika fanikiwa bila mgomo?