Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Yawezekana tumeshasahau au kama tunakumbuka basi tunakumbuka walichokifanya lakini hatukumbuki ni nani walifanya kitu hicho. Wengi wetu letu tumedandia garimoshi la vita dhidi ya ufisadi na kuwataja watu kwa majina lakini hatujui gari moshi hilo lilitiwa funguo na kina nani.
Wengine tumesahau pia kuwa JF ilipata umaarufu mkubwa na kuwa kero na kikwazo kwa baadhi ya wanasiasa ambao leo wamegeuka na kuwa upande wetu (Sitta alibeza nyaraka za kwenye mitandao!) lakini tumewasahau wale ambao walianzisha moto huu.
Sijawasahau.
Ni kundi la Watanzania wenye asili ya Kiasia ambao walikusanya taarifa mbalimbali juu ya "wenzao" na watu wengine ambao walihusika na mtandao wa ufisadi wa kimataifa wenye mfanano wa kundi la Kimafia la Sisilia kule Italia.
Aidha kwa kuzidiana kete, wivu, kisasi au chochote kile kilichokuwa nyuma ya malengo yao ukweli ni kuwa walichokifanya kimebadilisha kabisa mjadala wa mahusiano kati ya watawala na watawaliwa, walao na waliwa, wanasiasa na wapiga kura, wananchi na wageni. Walitoa kile kinachojulikana kama taarifa ya mtandao wa ufisadi iliyopewa jina la "Tanzania Mafia". Hii ililikuwa ni kabla ya sakata la Mwembe Yanga.
Ilikuwa kama utani na majungu lakini data walizomwaga, kuunganisha majina ya watu na makampuni, na kutuonesha mtandao huu ulivyofanya kazi ulisababisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Ballali, atimke na asirudi milele; ulisababisha mtikisiko wa aina yake huku walioatajwa humo ndani wakitafuta kila namna ya maelezo ya kufafanua vitendo vyao.
Ni katika ripoti hiyo tulifahamishwa kwa undani:
- mahusiano ya Ballali, Jeetu Patel, na Mkapa
- mahusiano ya kina Maregesi na kina Pateli
- Suala la Alex Stewart na kina Basil Mramba
- Kina Lukaza na Bank M
- Kampuni ya Negus ya huko Uswisi (hii hata hatujaanza kuiangalia!)
- Mradi wa Meremeta na wizi wa Benki Kuu
- N.k
Ilikuwa ni ripoti iliyomfichua mfalme kuwa yu uchi; ilikuwa ni ripoti ambayo inasimama kama uthibitisho wa kazi nzuri iliyofanywa na watu wa kawaida huku wanaolipwa kufanya kazi hiyo wakitafuta mbinu na njia ya kuizima. Ndugu zetu waasia hao (pamoja na washirika wengine) waliweza kufanya kile ambacho kimewashinda usalama wa taifa kwa miaka arobaini! Waliweza kufichua kile kilichowashinda kuanzia kina Solomon Liani hadi leo kina Mwema wanahangaika nacho!
Uwezo wao wa kukusanya na kuchambua data na kuziweka katika kurasa chache ulifanywa kwa gharama ya chini kweli kushinda vikao vya kamati mbalimbali za Bunge ambazo hutumia mabilioni kutafuta suluhisho la matatizo ya nishati bila ya mafanikio na kuandika ripoti lukuki zisisofanyiwa kazi zaidi ya kusababisha kuandikwa kwa ripoti nyingine.
Hivyo, ninatambua hisia za watu mbalimbali dhidi ya Watanzania wenye asili ya Asia (Wahindi n.k) na jinsi gani tunawashuku juu ya uzalendo wao na kujitoa kwao kwa ajili ya taifa.
Kwa hili moja nimejikuta leo nikiamua kuonesha shukrani za dhati kwa mchango wao mkubwa katika vita ya ufisadi kwani pasipo ripoti ile kali, labda leo tungeendelea kuchezeshwa "tiari bado" huku tukikimbizwa mchaka mchaka wa "Chinja". Leo hii tungeendelea kuwa na Benki Kuu ile ile ikifanya kazi zake kwa mtindo ule ule.
Ndio siyo kwamba tumefika na siyo kwamba ripoti ile imesababisha mabadiliko katika vichwa vya watawala wetu; hapana! Ripoti ile imetupa nguvu wananchi zaidi kuweza kubisha na kuwakatalia watawala; imetupa nguvu ya kuweza kutambua jinsi tunavyoibiwa kwa jina la "uwekezaji" na imetupa nguvu kuelewa kuwa siyo wote wavaao suti na kujiita wanasiasa na viongozi wanastahili mambo hayo.
Hivyo, kama nilivyofundishwa kushukuru nimejikuta nami nioneshe shukrani kwao. Kwani ni wao pia walituonya kuhusu TRL tukawakatalia na leo tunakiona cha moto. Sina budi kuwashukuru kwa sababu walikuwa na uchaguzi wa kukaa kimya na kufumba macho yao na kumalizana kimya kimya. Waliamua kusema na kutupa nguvu sisi wengine kupiga kelele!
Kwa niaba ya kijiji changu na wale wote ambao wanasimama leo kama majemedari dhidi ya vita hii ninawashukuru sana na ninaisubiria kwa hamu ripoti yao ijayo kabla ya uchaguzi mkuu. Kwani kwa mara nyingine tena, kuta za vyumba vya wanasiasa wetu na wale waliojinyanyua juu yetu zitatikisika na wale tuliowadhania siyo kumbe ndio hao hao!
Nimeona utangulizi wake, nimeipenda.
Project X-2010
In initiating stage...
"Change is coming; be part of it, don't wait for it"!
Well, kwa wale ambao hawajui ninazungumzia nini, nimeiambatanisha.