Nawashukuru Watanzania-Waasia hawa; historia itawakumbuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawashukuru Watanzania-Waasia hawa; historia itawakumbuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 28, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yawezekana tumeshasahau au kama tunakumbuka basi tunakumbuka walichokifanya lakini hatukumbuki ni nani walifanya kitu hicho. Wengi wetu letu tumedandia garimoshi la vita dhidi ya ufisadi na kuwataja watu kwa majina lakini hatujui gari moshi hilo lilitiwa funguo na kina nani.

  Wengine tumesahau pia kuwa JF ilipata umaarufu mkubwa na kuwa kero na kikwazo kwa baadhi ya wanasiasa ambao leo wamegeuka na kuwa upande wetu (Sitta alibeza nyaraka za kwenye mitandao!) lakini tumewasahau wale ambao walianzisha moto huu.

  Sijawasahau.

  Ni kundi la Watanzania wenye asili ya Kiasia ambao walikusanya taarifa mbalimbali juu ya "wenzao" na watu wengine ambao walihusika na mtandao wa ufisadi wa kimataifa wenye mfanano wa kundi la Kimafia la Sisilia kule Italia.

  Aidha kwa kuzidiana kete, wivu, kisasi au chochote kile kilichokuwa nyuma ya malengo yao ukweli ni kuwa walichokifanya kimebadilisha kabisa mjadala wa mahusiano kati ya watawala na watawaliwa, walao na waliwa, wanasiasa na wapiga kura, wananchi na wageni. Walitoa kile kinachojulikana kama taarifa ya mtandao wa ufisadi iliyopewa jina la "Tanzania Mafia". Hii ililikuwa ni kabla ya sakata la Mwembe Yanga.

  Ilikuwa kama utani na majungu lakini data walizomwaga, kuunganisha majina ya watu na makampuni, na kutuonesha mtandao huu ulivyofanya kazi ulisababisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Ballali, atimke na asirudi milele; ulisababisha mtikisiko wa aina yake huku walioatajwa humo ndani wakitafuta kila namna ya maelezo ya kufafanua vitendo vyao.

  Ni katika ripoti hiyo tulifahamishwa kwa undani:

  - mahusiano ya Ballali, Jeetu Patel, na Mkapa
  - mahusiano ya kina Maregesi na kina Pateli
  - Suala la Alex Stewart na kina Basil Mramba
  - Kina Lukaza na Bank M
  - Kampuni ya Negus ya huko Uswisi (hii hata hatujaanza kuiangalia!)
  - Mradi wa Meremeta na wizi wa Benki Kuu
  - N.k

  Ilikuwa ni ripoti iliyomfichua mfalme kuwa yu uchi; ilikuwa ni ripoti ambayo inasimama kama uthibitisho wa kazi nzuri iliyofanywa na watu wa kawaida huku wanaolipwa kufanya kazi hiyo wakitafuta mbinu na njia ya kuizima. Ndugu zetu waasia hao (pamoja na washirika wengine) waliweza kufanya kile ambacho kimewashinda usalama wa taifa kwa miaka arobaini! Waliweza kufichua kile kilichowashinda kuanzia kina Solomon Liani hadi leo kina Mwema wanahangaika nacho!

  Uwezo wao wa kukusanya na kuchambua data na kuziweka katika kurasa chache ulifanywa kwa gharama ya chini kweli kushinda vikao vya kamati mbalimbali za Bunge ambazo hutumia mabilioni kutafuta suluhisho la matatizo ya nishati bila ya mafanikio na kuandika ripoti lukuki zisisofanyiwa kazi zaidi ya kusababisha kuandikwa kwa ripoti nyingine.

  Hivyo, ninatambua hisia za watu mbalimbali dhidi ya Watanzania wenye asili ya Asia (Wahindi n.k) na jinsi gani tunawashuku juu ya uzalendo wao na kujitoa kwao kwa ajili ya taifa.

  Kwa hili moja nimejikuta leo nikiamua kuonesha shukrani za dhati kwa mchango wao mkubwa katika vita ya ufisadi kwani pasipo ripoti ile kali, labda leo tungeendelea kuchezeshwa "tiari bado" huku tukikimbizwa mchaka mchaka wa "Chinja". Leo hii tungeendelea kuwa na Benki Kuu ile ile ikifanya kazi zake kwa mtindo ule ule.

  Ndio siyo kwamba tumefika na siyo kwamba ripoti ile imesababisha mabadiliko katika vichwa vya watawala wetu; hapana! Ripoti ile imetupa nguvu wananchi zaidi kuweza kubisha na kuwakatalia watawala; imetupa nguvu ya kuweza kutambua jinsi tunavyoibiwa kwa jina la "uwekezaji" na imetupa nguvu kuelewa kuwa siyo wote wavaao suti na kujiita wanasiasa na viongozi wanastahili mambo hayo.

  Hivyo, kama nilivyofundishwa kushukuru nimejikuta nami nioneshe shukrani kwao. Kwani ni wao pia walituonya kuhusu TRL tukawakatalia na leo tunakiona cha moto. Sina budi kuwashukuru kwa sababu walikuwa na uchaguzi wa kukaa kimya na kufumba macho yao na kumalizana kimya kimya. Waliamua kusema na kutupa nguvu sisi wengine kupiga kelele!

  Kwa niaba ya kijiji changu na wale wote ambao wanasimama leo kama majemedari dhidi ya vita hii ninawashukuru sana na ninaisubiria kwa hamu ripoti yao ijayo kabla ya uchaguzi mkuu. Kwani kwa mara nyingine tena, kuta za vyumba vya wanasiasa wetu na wale waliojinyanyua juu yetu zitatikisika na wale tuliowadhania siyo kumbe ndio hao hao!

  Nimeona utangulizi wake, nimeipenda.

  Project X-2010
  In initiating stage...
  "Change is coming; be part of it, don't wait for it"!


  Well, kwa wale ambao hawajui ninazungumzia nini, nimeiambatanisha.
   

  Attached Files:

 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndio mkuu you have done the noble thing a gentleman is supposed to... Mkuu umenikumbusha that day Sita anahojiwa na Tido Mhando TBC1 akitoa majibu ya kejeli na vitisho and in just one yr amedandia meli ile ile aliyoiona ni ya kizushi na kufikirika. Kama nchi yetu na uongozi wetu ungekuwa makini na for the well-being of the people hawa jamaa zetu waliotoa taarifa hii walistahili zawadi nono kabisa.......

  It is a shame kwa uwt kuona kwamba baadhi ya mambo kwenye hiyo summarized report possibly hawayajafanyia kazi mpaka leo.
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tunaomba majina yao tafadhali ili tuwafikishie pongezi rasmi...
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  1. The truth aka nyama hatari
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Thats my point: What makes us sure they are/were Tanzanians of Asian origin?
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hivi ka-inzi kana rangi au kabila?
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunaomba ututajie tuwape ponezi zao za pekee kwa uzalendo wa nchi hii
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hey Companero i like you quote ,ila mbona sijaelewa unamaanisha nini mkuu?
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uzushi mtupu, gari moshi lilianzia stesheni namba moja, chanzo cha matatizo yote ya Tanzania ya leo ni Nyerere, Ujamaa ulikuwa ni chanzo cha matatizo na hilo halipingiki.

  "[FONT=Verdana,Arial,Helvetica]But the Tanzanian experiment offers good evidence that saints do not really make very good presidents"[/FONT]
   
 10. w

  wasp JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji kwanza nikushukuru kwa kutukumbusha habari hiyo. Hata mie nilikuwa na copy ya hiyo taarifa ambayo niliipata kwenye mtandao. Lakini mpaka leo sijui ni watu gani walio itayarisha. Kama ni Watanzania waasia basi nawapa hongera sana kwa kazi nzuri waliofanya ya kumwaga "mboga".
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Lady Dai namaanisha kwa nini tunaanza kuweka rangi na mbari kwenye haya mapambano - kwani tuna uhakika gani kuwa hawa walipuaji wa mafisadi ni Watanzania wenye asili ya wapi? Ufisadi hauna rangi wala kabila. Vivyo hivyo, mapambano dhidi ya ufisadi hayana rangi wala kabila!

  Mwanakijiji tafadhali badili bandiko lisomeke hivi: Nawashukuru Watanzania Wazalendo hawa; historia itawakumbuka.
   
 12. w

  wasp JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Dar Es Salaam", What are you talking about? Are you crazy? Can really follow what Mzee Mwanakijiji is informing us. The Loliondo saga, Goldmining contracts, EPA scandal, construction of Twin Towers by BOT, privatization of NBC, TRC, NASACO, selling of Government houses etc have nothing to do with Mwalimu Nyerere. Please let our beloved Mwalimu Nyerere rest in peace.
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Are you serious? Mbona mnapowakaanga hamsiti kuwaita kwa rangi zao? Hamsiti kuwaunganisha watanzania-waasia wote na vitendo vya wakina RA bila kujali kuwa hata Issa Shivji ni mmoja wao! Leo wanapotendewa haki napo mnataka kuwanyang'anya hilo? Soma hiyo ripoti utaona waandishi wamejitaja kuwa ni wa asili ipi! Badala ya kulalamika hapa ungeanza pale wanapohukumiwa wote kwa vitendo vya wachache. Ni nyinyi mliogeuza neno mtanzania mzalendo limaanishe mtanzania-mweusi. Waache nao wajisikie kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Ni nafasi adimu sana.

  Asante na shukurani Mzee Mwanakijiji.

  Amandla......
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee MWanakijiji Hakuna haja ya kutaja majina yao kwa watu hapa, maana watashindwa siku nyingine kutoa habari kama hizi, hivyo kuna haja ya watu hawa kuwapongeza japo walikuwa wanatoa habari kwa wivu na fitina tu
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Na sisi tunatoa pasipo wivu na fitina?

  Amandla......
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Their origin notwithstanding, hawa ni wazalendo wa kweli.
   
 17. Companero

  Companero Platinum Member

  #17
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Umeniona nikifanya hivyo? Wazalendo wapo 'weusi' kwa 'weupe'. Na mafisadi wapo 'weusi' kwa 'weupe'. Tuzingatie lililo la msingi: Vita dhidi ya mafisadi kwa maana ufisadi hauna rangi wala kabila.

  Nawapongeza wapinga mafisadi wote wa kweli!
   
 18. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  well, i dont quite like them, but give credit where it is due.
   
 19. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,998
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  mwanakijiji bana mara mooja mooja anakua ana akili.......ahhahahahhh kwa hili i like it.....ila watch out your coming project they might ruin it
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hii mbona ni TABIA na HULKA ya wana wa ADAM wote duniani hasa wanapohisi "wamedhulumiwa", hawakupata kabisa au wamepata kidogo kuliko walivyotarajia, ile roho ya kwa nini ni fulani tu na sio mimi, kutambiana kunapozidi hasa toka kwa waliopata, kwa nini huyu apewe mimi ninyimwe, na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo.

  Angalia RICHMOND, pamoja na kwamba wamo akina Gire, fitna zilianzia kwa watumishi weusi tii wa Serikali.
   
Loading...